Moto huo wa wabunge uliwalazimisha
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chizza na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema kusalimu amri na kukubali mapendekezo
ya wabunge.
Msimamo wa wabunge hao katika kuibana
Serikali, pia ulililazimisha Bunge kutengua kanuni zake na kuendelea na
shughuli za kupitia muswada huo hadi saa 7:35 mchana, badala ya
kusitishwa saa 7:00 kwa ratiba ya kawaida.
Serikali ilikubali mapendekezo ya
wabunge hao na kurekebisha vifungu ambavyo sasa vinampa mmiliki wa ardhi
itakayotangazwa eneo la umwagiliaji kuwa mwanahisa na kulipwa fidia.
Saturday, August 31, 2013
SERIKALI YASALIMU AMRI YA WABUNGE
Muswada wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji wa mwaka 2013, jana ulipita kwa mbinde bungeni mjini Dodoma, huku Serikali ikisalimu amri kwa wabunge na kukubali kurekebisha baadhi ya vifungu vyake.Bila kujali tofauti zao za kisiasa, wabunge jana walisimama kidete na kuonyesha uzalendo wa hali ya juu, wakitaka sheria hiyo imlinde mzawa badala ya mwekezaji.
M23 YATANGAZA KUSITISHA MAPIGANO KURUHUSU UCHUGUZI
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lambert Mende, ameiambia DW mjini Kinshasa kuwa serikali ya nchi hiyo haijashangazwa na hatua hiyo ya M23, lakini akasisitiza kuwa wanachotaka wao ni kuona waasi hao wakiweka silaha chini, kama wanavyotakiwa na jumuiya ya kimataifa na pia serikali ya Kongo.
Jana, Rwanda ililishutumu jeshi la
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kile ilichokiita uchokozi wa
makusudi, baada ya kombora linaloaminika kutoka upande wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kuanguka nchini Rwanda, na kumuuwa mwanamke mmoja
na kumjeruhi vibaya mtoto wake mchanga.
Friday, August 30, 2013
DIAMOND AMKABIDHI MZEE NGURUMO GARI AINA YA FUNCARGO
Msanii
Diamond Platnum amefanya kufuru usiku huu kwa kutoa zawadi ya Gari kwa
Mzee Ngurumo Mwanamziki wa miaka mingi na mkongwe nchini aliyestaafu
majuzi kufanya kazi za mziiki.
Tukio
hilo limetokea usiku huu ndani ya ukumbi wa SERNA HOTELkatikati ja jiji
la DSM ambapo Diamond Platnum anazindua video yake ya wimbo wa #one fun.
Mzee
Ngurumo amesema"Haamini macho na masikio yake,hanachakusema zaidi ya
ASANTE kwa msanii huyo"Lakini pia amesema hajui hata mke wake atasemaje
baada ya kumwona akiingia na gari ndani ya nyumba yake.
Mzee ngurumo amekuwa na matatizo ya
kiafya siku za karibuni nakupelea kustaafu mziki kabisa.Wazee wa
msondongoma ndio wanajua makali ya Mzee Ngurumo."KAJALA NDIO KILA KITU KWANGU KWA SASA, YEYE NI ZAIDI YA MUME KWANGU"......WEMA
KASUMBA ya wanawake wengi kuwaambia mashoga zao siri zao nzito
inadaiwa kumfanya msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu kufunguka
kuwa, bila kuwa karibu na Kajala Masanja itakuwa ni kama kuamua kutembea
mtupu.
“I always call my poch and I fell so naked without, I need her everywhere with me. I hope that’s how they out each other.” Aliandika kimombo, alimaanisha nini?
Tafsiri ya maneno hayo ni kwamba, Wema anamchukulia Kajala kama pochi yake na bila yeye anajihisi yuko uchi kiasi kwamba anataka kila sehemu wawe wote. Kajala amjibu
Baada ya Wema kutundika ujumbe huo, Kajala naye alijitutumua na kutupia maneno ya kumshukuru (Wema) huku akieleza kuwa, kama ni hivyo yeye hana la kusema.
“Nimeyapenda maneno hayo, kama ni hivyo mimi sina la kusema,” aliandika Kajala kwenye mtandao huo.
Kwa nini Wema aseme hivyo?
Yawezekana Wema alimaanisha vingine lakini wachambuzi wa mambo wamekuwa na maoni yao huku wengi wakieleza kuwa, inawezekana Wema anasema hivyo kutokana na ukweli kwamba Kalaja anajua siri zake nyingi.
Wema Sepetu na Kajala Masanja.
Wema alifikia hatua ya kutoa maneno hayo katikati ya wiki hii kwa
kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha yeye, meneja wake
Martin Kadinda na Kajala huku akisindikiza na ujumbe mzito uliosomeka:“I always call my poch and I fell so naked without, I need her everywhere with me. I hope that’s how they out each other.” Aliandika kimombo, alimaanisha nini?
Tafsiri ya maneno hayo ni kwamba, Wema anamchukulia Kajala kama pochi yake na bila yeye anajihisi yuko uchi kiasi kwamba anataka kila sehemu wawe wote. Kajala amjibu
Baada ya Wema kutundika ujumbe huo, Kajala naye alijitutumua na kutupia maneno ya kumshukuru (Wema) huku akieleza kuwa, kama ni hivyo yeye hana la kusema.
“Nimeyapenda maneno hayo, kama ni hivyo mimi sina la kusema,” aliandika Kajala kwenye mtandao huo.
Kwa nini Wema aseme hivyo?
Yawezekana Wema alimaanisha vingine lakini wachambuzi wa mambo wamekuwa na maoni yao huku wengi wakieleza kuwa, inawezekana Wema anasema hivyo kutokana na ukweli kwamba Kalaja anajua siri zake nyingi.
KATIBA YATAKIWA IRUHUSU WAFUNGWA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA NA WENZA WAO ILI KUPUNGUZA USAGAJI NA USHOGA GEREZANI
BAADHI ya
wadau wa masuala ya jinsia wamependekeza kuwa ili kukabiliana na masuala ya
ushoga na usagaji, Katiba Mpya iruhusu wafungwa kukutana kimwili na wenza wao,
kwani vitendo hivyo chanzo chake ni gerezani hasa kwa vijana wanaokula 'unga'
na kuvuta bangi.
Hayo yalisemwa juzi kwenye
kikao cha maboresho ya Rasimu ya Katiba Mpya, kilichofanyika siku tatu kwenye
Kijiji cha Makaburini kwa kuratibiwa na asasi ya Tanzania Environment Relatives
Organization (TERO) ya mjini Korogwe kwa ufadhili ya Shirika la The Foundation
for Civil Society la jijini Dar es Salaam.
"Mfungwa akubaliwe
kukutana kimwili na mume au mke wake. Kitendo cha kuwakatalia wafungwa kukutana
kimwili na wake au waume zao kunachochea vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia
moja na vijana wengi wameharibikia gerezani na kujikuta vitendo hivyo vinaingia
mitaani"
RAIS KIKWETE AMUOMBA RAIS WA UGANDA AONGEE NA KAGAME ILI KUMALIZA UGOMVI ULIOPO
RAIS Jakaya Kikwete, amewasiliana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ili azungumze na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa nia ya kumaliza mvutano wa maneno kati yao kwa busara.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hayo jana bungeni, alipokuwa akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema).
“Tunataka suala hili limalizike kwa njia ya busara, ili watu waendelee kuchapa kazi, ninaamini busara zitatumika kumaliza tatizo hilo,” alisema.
Akiuliza swali katika kipindi cha maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu jana, Mbowe alitaka kujua kauli ya Serikali na mikakati iliyopo kupata suluhu katika mvutano wa maneno uliojitokeza kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame.
Pia Mbowe alitaka Serikali kuunda jopo la ushawishi wa kimataifa, kutokana na Rwanda kuonekana kushawishi nchi za Uganda na Kenya, jambo ambalo linaashiria kuitenga Tanzania katika shughuli mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Mbowe, kitendo cha marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana katika mikakati ya kuanza kutumia bandari ya Mombasa ambayo ingekuwa ya nchi za Afrika Mashariki, ni dalili kuwa Tanzania imeanza kutengwa.
Thursday, August 29, 2013
SHILOLE: MADEE AU OMMY DIMPOZ..?KILA MMOJA ANASWA NAE CHOBINGO....!!!
Shilole akiwa na Madee.
Kwanza paparazi wetu alimfotoa Shilole picha kadhaa akiwa anafungwa zipu na Madee.
...Akiwa na Ommy Dimpoz.
BAADA YA KIMYA KIREFU, GK AIBUKA NA NGOMA MPYA
MSANII mahiri katika anga za muziki wa Bongofleva, Gwamaka Kaihura 'King Crazy GK' leo ameibuka na singo yake mpya iitwayo Baraka au Laana aliyomshirikisha msanii Yuzo. aka sita baada ya kuwa busy na masomo kitendo kilichopelekea kuupa kisogo muziki kwa muda na kuwafanya mashabiki wake kum-mis katika fani hiyo. Memba huyo wa East Coast Team ameachia ngoma yake mpya leo na anataraji kuachia video yake siku ya Ijumaa Agosti 30, mwaka huu.
GK alisema kuwa amerudi kwenye game kwa nguvu zote na amewashukuru
baadhi ya wadau kama Eric Shigongo, Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa
kumtia hamasa ya kurudi kwa nguvu mpya baada ya kupotea kwa muda.
ETO'O AWASILI LONDON KUFANYIWA VIPIMO NA KUJIUNGA NA CHELSEA
Eto'o akiwasili London (HM)
Eto'o, 32, amekubali kupunguza dau lake alilokuwa akilipwa na Anzhi kiasi cha £17m kwa mwaka na sasa atasaini atasaini akiwa huru.
Pamoja na hilo, lakini inaeleweka kwamba Anzhi wamemlipa Eto'o millioni kadhaa ili kuweza kumuondoa katika listi wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ndaniya klabu ya Anzhi.
Eto'o aliwasili jijini London jana usiku na anategemewa kufanyiwa vipimo vya afya mchana wa leo katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham. Chanzo: Shaffihdauda
MAPYA YAIBUKA KUHUSU TRAFIKI FEKI, KUMBE ALIKUWA MFUNGWA ALIYETOROKA JELA.... !!!
MAZITO tena yameibuka kuhusu yule
trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es
Salaam ambaye yuko Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya
kujifanya askari wa usalama barabarani.
Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.
Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda.
“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha.
Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.
Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.
Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda.
“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha.
Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.
Subscribe to:
Posts (Atom)