MKAGUZI
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema
taarifa ya Sh bilioni 252 zilizokuwa zimeoneshwa katika taarifa ya
Wizara ya Ujenzi, zilihamishwa kwenda Wakala wa Barabara (Tanroads)
kulipia madeni ya wakandarasi na kwamba hapakuwa na ufisadi.
Kihasibu fedha hizo zilipaswa kuoneshwa kwenye hesabu za mtumiaji halisi wa fedha ambaye ni Tanroads na siyo Wizara hiyo,” alisema Utouh.
Kihasibu fedha hizo zilipaswa kuoneshwa kwenye hesabu za mtumiaji halisi wa fedha ambaye ni Tanroads na siyo Wizara hiyo,” alisema Utouh.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Utouh alisema vyombo vya
habari viliripoti suala hilo tofauti, baada ya Kamati ya Hesabu za
Serikali (PAC) kukutana na wizara na kuhoji juu ya matumizi ya fedha
hizo.
Utouh
alisema baada ya PAC na Kamati ya Kudumu ya Serikali za Mitaa (LAAC)
kupitia ripoti ya Wizara ya Ujenzi, kumejitokeza upotoshaji wa taarifa
kuhusu hesabu za wizara hiyo na taarifa zisizo sahihi, zikidai kulikuwa
na ufisadi.
Alisema
fedha hizo zimeoneshwa kwenye taarifa ya hesabu za Wizara hiyo, kama
vile ni miradi mipya ya mwaka 2011/2012 tofauti na uhalisia wake.
“Fedha
hizi zilijumuishwa kimakosa kwenye hesabu za Wizara kama matumizi ya
akaunti ya maendeleo, hivyo kuongeza matumizi ya Wizara kimakosa kwa
kiasi hicho
Utouh
alisema uhalisia wa fedha hizo ni kuwa mara baada ya kupokewa na Wizara
ya Ujenzi kutoka Hazina, zilihamishwa kwenda Tanroads kulipia madeni ya
wakandarasi wa miradi ya barabara, iliyotekelezwa na wahandisi
washauri, ambao walikuwa hawajalipwa kwenye mwaka wa fedha 2010/2011.