Friday, August 23, 2013
MUNGU ALINIAMURU NIJIUZULU, ASEMA PAPA BENEDICT XVI
Jana, vyombo vya habari vilimkariri Papa Mstaafu Benedict akimweleza mgeni wake kuwa aliitwa na Mungu kwa miujiza.
P.T
Kiongozi huyo ambaye alishangaza watu kwa uamuzi huo wa Februari 8, mwaka huu, hata hivyo alisema sauti ya Mungu imejibu kupitia kwa mfuasi wake, Papa Francis.
Papa Benedict alitangaza uamuzi wa kujiuzulu Februari 11, maelezo yake yalielekeza katika afya yake.
Alisema nguvu zake zilikuwa zimepungua kiasi cha kutokuweza kumudu majukumu yake ipasavyo.
ANGALIA PICHA ZA RAIS ROBERT MUGABE WA ZIMBABWE ALIPOKULA KIAPO JANA
Rais
wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akila kiapo cha kuongoza nchi hiyo
kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa
Taifa wa Michezo wa Harare Agosti 22, 2013
Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe akivishwa shada na medali baada
ya kula kiapo cha kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo katika
sherehe zilizofana sana katika Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare
Agosti 22, 2013
MKENYA AKIRI KUUA NA KULA MOYO NA UBONGO WA MAREHEMU, MAREKANI
Alexander Kinyua (kushoto) na mwanamume aliyekuwa akiishi naye nyumba moja Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie. Picha/MAKTABA
Mwanafunzi kutoka Kenya aliyekuwa akiishi Marekani amekiri kwamba
alimuua mwanamume waliyekuwa wakiishi nyumba moja na kula moyo wake na
ubongo wake.
MWANAFUNZI
kutoka Kenya aliyekuwa akiishi Marekani amekiri kwamba alimuua mwanamume
waliyekuwa wakiishi nyumba moja na kula moyo wake na ubongo wake.
Alexander Kinyua, 22, alikiri mashtaka ya mauaji ya Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie, 37, katika jimbo la Maryland mwaka jana lakini Jaji akasema hafai kulaumiwa aliposhtakiwa Jumatatu wiki hii.
Alexander Kinyua, 22, alikiri mashtaka ya mauaji ya Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie, 37, katika jimbo la Maryland mwaka jana lakini Jaji akasema hafai kulaumiwa aliposhtakiwa Jumatatu wiki hii.
Thursday, August 22, 2013
HATIMAYE MWANAMUZIKI MKONGWE WA DANS MUHIDIN GURUMO AKUBALI YAISHE NA SASA ASTAAFU RASMI MUZIKI
Mwanamuziki
mkongwe wa muziki wa dansi wa bendi ya Msondo Ngoma, Mzee Muhidin
Gurumo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake wa
kustaafu rasmi kazi ya muziki aliyoifanya kwa muda wa miaka 53 sasa.
Gurumo alitoa kauli hiyo leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo
jijini Dar es Salaam. Picha na Magreth Kinabo.
************************************
Na Jennifer Chamila, Maelezo.
MWANAMUZIKI
mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo amestaafu rasimi
kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mzee Gurumo mwenye
umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake
mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
“Muziki
kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu
kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki
yeyote atakayetaka ushauri wangu,”alisema Mzee Gurumo.
MAAFISA WA JESHI LA POLISI WAVULIWA MADARAKA NA KUSIMAMISHWA KAZI
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ya kuwavua madaraka
Maafisa wanne wa Jeshi la polisi nchini na kumsimamisha kazi mmoja
kutokana na kukiuka maadili na taratibu za Jeshi la Polisi.
……………………………………………………………….
Na Lydia Churi, MAELEZO
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na kumsimamisha kazi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka maadili na taratibu za jeshi hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na kumsimamisha kazi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka maadili na taratibu za jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es salaam leo, Waziri Nchimbi amesema hatua hiyo ni
katika kuendeleza vita ya kuhakikisha kuwa jeshi la polisi linakuwa na
nidhamu, linatekeleza wajibu wake wa kutenda haki na kuwalinda raia na
mali zao.
Alisema amewachukulia hatua
Maafisa hao baada ya kuridhia maoni ya kamati aliyoiunda kufanya
uchunguzi wa matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari polisi katika
mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma kati ya Desemba 2012 na
Mei, 2013.
FILAMU YA “FOOLISH AGE” YAIKUTANISHA LULU NA BODI YA FILAMU...!!!
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe pamoja
na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa
marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya “Foolish Age” katika Bodi ya
Filamu kwa ajili ya ukaguzi.
Msanii
wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi
ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni yake ya Proin Promotions
ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi.
Msanii
wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana
na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu
yake ya “Foolish Age”.
NEY WA MITEGO SASA KUPELEKWA MAHAKAMANI NA MADAM RITA.....!!!
Baada ya Ney Wa Mitego kutoa Track ya Salam Zao, Kuna tetesi Kuwa
Muandaaji wa BSS Madam Rita anampango kumfungulia Kesi ya Madai Ney wa
Mitego kwa Kumchafua (Defamation)
kwani eti alisema Madam Rita huwa
hatoi zawad anazoziahidi kwa washindi wa shindano
lake la kusaka Vipaji, Je Kama ni kweli kuhusu Kesi hii Ney wa mitego
ataweza kulipa milioni 500? Tayari msanii huyo amesema yuko tayari
kwenda mahakamani na ataweka mwanasheria wa kumtetea.
HII NDO KAULI KUTOKA KWA NDUGU WA AGNES MASOGANGE, KUHUSU NDUGU YAO KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA
Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa familia hiyo aliyeomba jina lake lisitiriwe, wameamua kumwachia Mungu ishu hiyo kwani ndiye anayejua ukweli. “Unajua baba wa Masogange (mzee Gerald Waya) ni mlokole, sasa amekabidhi ishu nzima mikononi mwa Mungu kwa hiyo hayuko tayari kusemasema maneno ambayo hayatakuwa na faida,” alisema ndugu huyo.
Habari zinazidi kudai kwamba, mzee huyo aliwahi kuchukizwa na kitendo cha binti yake huyo kujiingiza kwenye sanaa, hadi kuonekana akinengua kwenye muziki.
Hilo liliwahi kubainishwa na Masogange mwenyewe miaka ya nyuma alipohojiwa na gazeti ndugu na hili (Ijumaa) kupitia safu ya Ten Questions (Maswali Kumi) ambapo ilikuwa hivi:
TQ: Inasemekana umetokea kwenye familia ambayo imeiva kidini, walokole, wao wanachukuliaje suala la wewe kuingia kwenye mambo ya kuuza sura tena wakati mwingine kwenye mavazi ya kimitego?
WATUMISHI WA ZAHANATI WATUHUMIWA KUFANYA MAPENZI NA WAGONJWA.
WATUMISHI wawili katika zahanati ya Mwanhala wilayani Nzega, wamekumbwa na kashfa ya kufanya mapenzi na wagonjwa hospitalini.
Kutokana na kashfa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bitun Msangi, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa watumishi hao.
Agizo la mkuu huyo limetolewa hivi karibuni, baada ya Diwani wa kata ya Utwigu, Sawaka Shita kuwalalamikia watumishi hao mbele ya Baraza la Madiwani, kwa kukithiri kufanya mapenzi na wagonjwa nyakati za kazi, licha ya kuonywa kwa mara kadhaa.
Diwani huyo aliliambia baraza hilo kuwa vitendo hivyo vina hatarisha maisha ya watumishi hao na ya wananchi, hususani waliotembea nao na kutishia kuvunja ndoa za wananchi.
Alidai kuwa taarifa hizo za malalamiko, zilishafika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, tayari kwa utekelezaji, lakini wananchi wa kata hiyo walitaka kuifunga zahanati hiyo, baada ya kukithiri vitendo hivyo vya kufanya mapenzi katika wodi zilizopo.
MKE AFUMANIWA AKILIWA URODA CHOONI NA RAFIKI WA MUMEWE
Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Juma, mkazi wa Tegeta A, Dar amejikuta akikamuliwa faini ya Sh. laki tano kufuatia kufumwa ugoni na mke wa mtu.
Katika tukio hilo lililojiri Kimara-King’ong’o, Dar, Jumapili iliyopita, Juma alifumaniwa na mke wa mwanaume aitwaye Swai aliyetajwa kwa jina moja la Cesilia, mkazi wa maeneo hayo.
Ilidaiwa kuwa Cesilia alimwachia mumewe mtoto na kumuaga kuwa anakwenda harusini ambapo mumewe alimkubalia bila kujua kumbe anakwenda kuzini.
Ilisemekana kuwa muda mfupi baadaye, kuna vijana walimfuata Swai na kummwagia ‘upupu’ kuwa mkewe alikuwa akisaliti ndoa yao.
Ilifahamika kuwa vijana hao walimchukua Swai na kumpeleka hadi kwenye nyumba ambayo wenyewe hawajahamia iliyopo karibu na biashara yao ya duka ambapo baada ya mwenye mali kuingia, alimkuta Juma akiwa amevaa ‘singlendi’ na bukta ambapo alizidi kuangaza macho huku na kule ili amuone mkewe.
RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU WAKE.... !!!
Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za Serikali katika ngazi hizo za juu,” alisema Balozi Sefue.
Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo:
- Dk Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
- Joyce Mapunjo amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.
RWANDA NA UGANDA WAJITOA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.
Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.
“Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Hanspope.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... “Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.”
Subscribe to:
Posts (Atom)