Monday, August 19, 2013
SIRI ZA TRAFIKI FEKI ZAFICHUKA, YADAIWA ALIANZA KAZI MKOANI SINGIDA,AKAJIPA UHAMISHO WA KIKAZI HADI DAR...!!!
SIKU chache baada ya kukamatwa kwa
askari 'feki' wa Usalama Barabarani mwenye cheo cha Sajini, akifanya kazi ya
kuongoza magari eneo ya Tabata Kinyerezi, Dar
es Salaam, mambo mapya yamezidi kubainika juu ya
sababu za mtu huyo kujiingiza katika kazi hiyo bila kutambuliwa na Jeshi la
Polisi.
Habari
zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vya kuaminika, zinasema trafiki huyo
'feki', ambaye inadaiwa jina lake
halisi ni James Juma
Hussein (45), mkazi wa Kimara Matangini, alianzia kazi hiyo mkoani Singida
kabla ya kujipa uhamisho wa kikazi kwenda Dar es Salaam.
Chanzo
chetu kilieleza kuwa, trafiki huyo alikuwa na shemeji yake aliyeitwa Shaban
ambaye aliajiriwa na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani aliyekuwa
akifanyia kazi mkoani Tabora.Vyanzo
vyetu viliongeza kuwa, baada ya shemeji yake kufariki mkoani Tabora, trafiki
huyo alipata mwanya wa kuchukua nguo za kazini alizokuwa akizitumia shemeji
yake.
MECHI YA NGAO YA JAMII YA YANGA NA AZAM YAINGIZA MIL 208
Mechi
hiyo ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi wa msimu
mpya wa 2013/2014 iliyochezwa jana (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 208,107,000. Washabiki 26,084
walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Yanga
kushinda Azam bao 1-0.
Mgawanyo
wa mapato ya mechi hiyo uliokuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 31,745,135.59, asilimia 10 ya mchango wa
kusaidia jamii sh. 20,810,700, gharama ya tiketi sh. 7,309,866.
Uwanja
sh. 22,236,194.76, gharama za mchezo sh. 13,341,716.86, Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,188,445.44, TFF sh.
13,341,716.86 na Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
6,670,858.43. Kila klabu imepata mgawo wa sh. 43,731,183.03.
MAJINA YA WALIOKOSEA KUJAZA FOMU ZA MIKOPO KWENDA CHUO KIKUU
Tizama majina kwa kubofya hapa chini
DEREVA DALADALA AFUMANIWA GESTI AKIWA NA BINTIYE.....!!!
Za mwizi 40:Temba baada ya kufumaniwa na mkewe akiwa na bintiye.
AMA kweli za mwizi arobaini! Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Temba, mkazi wa Kimara-Rombo, Dar ambaye ni dereva wa daladala amefumaniwa laivu na mkewe akiwa gesti na binti yao wanayemlea.
NI MTEGO
Tukio hilo la aina yake lilijiri wiki iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo maeneo hayohayo ya Kimara-Rombo, majira ya saa 10:00 jioni ambapo Temba ambaye ni dereva wa daladala inayofanya safari kati ya Kimara na Kariakoo alinaswa kiulaini baada ya kuwekewa mtego.
OFM YATAARIFIWA
Baada ya mke wa Temba kuweka mambo vizuri aliitaarifu Oparesheni Fichua Maovu ya Global Publishers ambapo alihojiwa maswali muhimu kisha kutakiwa kuwajulisha polisi ili kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.
MWANZO WA YOTE HADI FUMANIZI
Kwa mujibu wa mke wa Temba, siku kadhaa nyuma aligundua kuwepo kwa mawasiliano ya kimapenzi kati ya mumewe na binti yao hivyo akalazimika kufanya uchunguzi wa kina.
BARCELONA YAFANYA KUFURU, YAIGONGA LEVANTE 7-0
Wachezaji wa Barcelona wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Alexis Sanchez dakika ya tatu.
Lionel Messi kama kawaida yake katupia mbili katika mechi ya leo.
Sunday, August 18, 2013
HII NDIO SABABU ILIYOFANYA AGNESS MASOGANGE KUSHTUKIWA NA POLISI NA HATIMAE KUKAMATWA NA UNGA AFRIKA KUSINI
Kilichomponza Masogange kukamwatwa ni pale alipochelewa kutoka uwanjani hapo kutokana na kujiremba, kitu ambacho kilisababisha kufanyiwa upekuzi wa dharura na askari ambaye hakujua kuhusu mpango huo. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
Taarifa zinabainisha kwamba, baada ya Masogange na wenzake kufanikiwa kupita katika maeneo ya ukaguzi ya uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini, mwenzake waliyesafiri pamoja aliyetajwa kwa jina la Mangunga alifanikiwa kuondoka uwanjani hapo na mabegi matatu yenye jumla ya kilo 60 za madawa hayo ya kulevya bila kujulikana.
"Kilichomponza Masogange ni pale alivyokuwa anajiremba baada ya kuruhusiwa kupita katika vizuizi vyote. Kiuhakika hakukamatwa katika mashine, bali ulikuwa ni ukaguzi usio rasmi uliofanywa na Polisi. Nadhani huyu Askari aliyewashika hakujua kuhusu mpango huo." kilisema chanzo kimoja ndani ya jeshi la Polisi kama ilivyonukuliwa katika gazeti la Tanzania Daima la Tarehe 17/8/2013
NEWS OF RWANDA WAANDIKA KUWA RAIS JAKAYA KIKWETE ANAWEZA KUWA NA ASILI YA GITEGA BURUNDI....!!!
Mtandao wa News of Rwanda juzi umeandika
makala yenye kichwa cha habari, ‘If President Kikwete is Tanzanian,
then most Rwandans being expelled are Tanzanians too’ na kuandika kile
linachodai kuwa Rais Kikwete anaweza kuwa na asili ya Burundi.
Kwa mujibu wa wazee wa Burundi waliohojiwa na mtandao huo, umedai Rais Kikwete anaweza kuwa na asili ya Giteka, Burundi.
“They are of Rwandan origin, but speak Kirundi and solely prefer to be viewed as Burundians. By virtual of that country’s laws, they are indeed Burundians,” limeandika. So where did President Jakaya Mrisho Kikwete come from? There are no original residents of Bagamoyo in Tanzania where Kikwete’s parents are traced. Most people from that area are remnants of slaves who were seem as unfit for the market during the slave trade era.
“They are of Rwandan origin, but speak Kirundi and solely prefer to be viewed as Burundians. By virtual of that country’s laws, they are indeed Burundians,” limeandika. So where did President Jakaya Mrisho Kikwete come from? There are no original residents of Bagamoyo in Tanzania where Kikwete’s parents are traced. Most people from that area are remnants of slaves who were seem as unfit for the market during the slave trade era.
KIWEWE, MATUMAINI WAOKOKA.....!!!
MSANII wa Kundi la Ze Komedi, Robert Augustino ‘Kiwewe’ na mwenzake
Tumaini Martin ‘Matumaini’ wameamua kuacha anasa na kumrudia Mungu kwa
kuokoka.
Wakizungumza
na paparazi wetu kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema
kilichosababisha kuchukua uamuzi huo kwa wakati mmoja ni kutokana na
manzingira waliyolelewa tangu wakiwa wadogo, yaani kumjua Mungu.
“Niliamua kufanya uamuzi sahihi ambao naamini utanibadilishia maisha yangu kwa kiasi kikubwa, kwa kufuata mambo yanayompendeza Mungu na siyo starehe za ujana,” alisema Kiwewe huku akiungwa mkono na Matumaini. Wakabainisha kuwa wanasali kwa Mchungaji Josephat Gwajima.
Wasanii hao walisema, ili kuhakikisha wanaungana na Mungu katika kila jambo, wameamua kuanzisha kundi lao la muziki wa Injili, Comedians Gospel linaloundwa na wao pamoja na Mkono.
“Niliamua kufanya uamuzi sahihi ambao naamini utanibadilishia maisha yangu kwa kiasi kikubwa, kwa kufuata mambo yanayompendeza Mungu na siyo starehe za ujana,” alisema Kiwewe huku akiungwa mkono na Matumaini. Wakabainisha kuwa wanasali kwa Mchungaji Josephat Gwajima.
Wasanii hao walisema, ili kuhakikisha wanaungana na Mungu katika kila jambo, wameamua kuanzisha kundi lao la muziki wa Injili, Comedians Gospel linaloundwa na wao pamoja na Mkono.
LIST YA VIGOGO MAFISADI WA ARDDHI HII HAPA....!!!
Getrude Lwakatare |
WAMO DEWJI,
LWAKATARE, RUTABANZIBWA
WABUNGE Mohamed Dewji wa Singida mjini na
Mchungaji Getrude Lwakatare wote wa CCM pamoja na mfanyabiashara maarufu jijini
Dar es Salaam Robery Mugishagwe wametajwa kuwa vinara wa uvamizi na uuzaji wa
viwanja jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, naye ametajwa kumkingia kifua mmoja
wa wavamizi wa viwanja kwa kumuwekea dhamana alipofikishwa polisi.
Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,
Dk. Tereza Huviza ndiye aliyewataja vigogo hao jana jijini Dar es Salaam,
alipokuwa akizungumza na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maliasili,
Ardhi na Mazingira, iliyokwenda kutembelea ofisi za Baraza la Mazingira
(NEMC).
Huvisa alikuwa akihofia kutaja majina ya vigogo
hao, lakini Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli, alimkasirikia na kumhoji
ni nani hapa nchini aliye juu ya sheria kiasi cha kumfanya aogope kumtaja licha
ya kuvunja sheria.
Lembeli alimtaka Waziri Huvisa kuyataja majina
hayo kwani akiendelea kuwahofia watu wa aina hiyo, wataendelea na uvamizi huo na
watakapofika 100 wenye tabia hizo nchi haitatawalika.
“Huna sababu ya kuogopa kuwataja watu waovu,
kamati hii ina mamlaka kisheria…usihofie chochote, wataje tujue namna ya
kuwashughulikia,” alisema Lembeli.
Shinikizo hilo la Lembeli liliungwa mkono na
wajumbe wote wa kamati hiyo waliomuhakikishia usalama Waziri Huvisa aliyeonekana
kuwa na hofu wakati akiulizwa maswali.
Baada ya kuhakikishiwa usalama, alianza kumtaja
Dewji ambaye alisema anashinikiza kupewa eneo la ufukwe karibu na zilipo ofisi
za ubalozi wa Urusi hapa nchini huku akijua ni kinyume cha sheria.
YANGA YAILAMBA KIMOJA AZAM, TAIFA JANA... SHUHUDIA MATUKIO YALIYOJILI KATIKA PICHA
Wachezaji wa
Yanga wakiiibusu ngao ya jamii waliyotwaa baada ya kuifunga Azam bao 1-0
katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jana. |
BIA YA TUSKER YAZINDUA SHINDANO LA 'TUSKER PROJECT FAME'....!!!
Meneja
wa Bia ya Tusker kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti, Sialouise Shayo
(katikati) akizungumza na wanahabari leo kuhusu TUSKER PROJECT FAME.
Kushoto ni Meneja Masoko Tusker, Anitha Msangi na msanii mahiri Zahira
Zoro.
Kutoka kushoto ni Anitha Msangi,
Sialouise Shayo, Mwanamuziki mahiri Zahira Zorro, na mzao wa Tusker
Project Fame, Aneth Kushaba.
FOOLISH AGE YA LULU KUZINDULIWA MWISHO WA MWEZI HUU NDANI YA MLIMANI CITY
Msanii mwenye
kipaji cha Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael
"LULU"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tokea alipotoka
Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengezwa na Kampuni ya
Proin Promotion Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika
Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam.
Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya LULU ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu.
Filamu hiyo inayoelezea Maisha ya LULU ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika Uzinduzi huo wa Filamu hiyo ya Lulu Wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi Band anatarajiwa kushusha bonge moja la burudani ya kufa mtu.
ARSENAL YAANZA LIGI KWA KICHAPO, YAPUMZISHWA 3-1, BENTEKE NOMA!, LIVERPOOL, SOUTHAMPTON, FULHAM, WEST HAM ZACHINJA
Mtaalamu wa kufunga: Nyota wa Arsenal, Olivier Giroud, kushoto, akiandika kimiani bao la kwanza kwa Arsenal
Kikosi
cha Arsenal: Szczesny 4; Sagna 5 (Podolski 90), Koscielny 5,
Mertesacker 5, Gibbs 5 (Jenkinson 28, 5); Wilshere 6, Ramsey 5, Rosicky
6; Walcott 6, Chamberlain 6 (Cazorla 46, 5); Giroud 6.
Wachezaji wa Akiba: Fabianski, Frimpong, Gnarby, Sanogo.
Villa: Guzan
7, Lowton 7, Vlaar 7, Baker 6 (Clark 17, 7), Luna 7; El Hamadi 7,
Westwood 7, Delph 8; Agbonlahor 7, Weimann 8 (Bacuna 88); Benteke 8
Subscribe to:
Posts (Atom)