Saturday, August 17, 2013

WAKILI WA PONDA ANENA JUU YA SHEIKH PONDA

Wakili wa Sheikh Ponda

Wakili wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Nassor Jumaa, amesema kuwa amesikitishwa na hatua  ya vyombo vya dola kumuondoa Ponda aliyekuwa  amelazwa katika wodi ya Kitengo  cha Taasisi ya Tiba  ya Mifupa  na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu(MOI)  alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumwamishia katika gereza la Segerea.


Wakili Jumaa alisema amesikitisha na kitendo hicho kwani hakimu Hellen Riwa juzi muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea shitaka Ponda, hakimu Liwa alitoa amri ya Ponda aendelee kukaa chini ya ulinzi lakini cha kushangaza leo,wanausalama wamemtoa wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Thursday, August 15, 2013

WATUMIA MIFUKO YA RAMBO BADALA YA KONDOMU KWA WATAKAOPATA WANACHANGIA......!!!


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi mk o a n i Ki l ima n j a r o , wamelazimika kutumia mifuko ya plastiki (malboro) kujikinga na maambukizo ya ugonjwa wa Ukimwi, huku wengine wakichangia kondomu, jambo ambalo ni hatari na linaelezewa kuwa moja ya chanzo cha ongezeko la maambukizo mapya ya ugonjwa huo mkoani humo.  

Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizo ya ugonjwa wa Ukimwikatika Mkoa wa Kilimanjaro, kimepanda kutoka asilimia 1.9 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 3.8 mwaka 2011/2012. 
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali, linalojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi mkoani Kilimanjaro (KACA) Faraji Swai alisema wananchi wa maeneo ya vijijini wako hatarini zaidi kupata maambukizo ya ugonjwa ya ukimwikutokana na kwamba wengi bado hawajafikiwa. 

Alisema Shirika la Kacakatika utoaji elimu ya mapambano dhidi ya Ukimwi kwa jamii, wamefika katika baadhi ya vijiji mkoani Kilimanjaro na kuwakuta wananchi wakitumia mifuko ya plastiki (malboro) kama kinga ya kujikinga na maambukizo ya Ukimwihuku wengine wakichangia kondomu jambo ambalo liliwashangaza.

HIZI NDIZO NCHI 25 MASKINI ZAIDI DUNIANI

 
TAKWIMU za nchi masikini dunian,Tanzania mwaka 2010 ilishika nafasi ya tatu kwa umaskini duniani, lakini Tanzania kwa sasa imepiga hatua hata na kwenye 25 Tanzania haimo katika nafasi ya nchi masikini duniani.

BARNABA NA AMINI WALITAMBULISHA KUNDI LAO JIPYA LIITWAYO 'GEMENIH'


Wale wakali toka jumba la vipaji Tzee- THT walioishi kama pacha kwenye jumba hilo (Amini & Barnaba) wameungana na kuunda crew yao mpya kimziki iitwayo “GEMENIH” wakimaanisha wao ni kama mwezi na nyota angani. 
 
“Yap, Tumeungana kufanya kazi pamoja kama kundi nje ya THT tukiwa ni matunda ya THT na tumeamua kujiita hivyo kutokana na kutegemeana kwetu kwenye kazi na umuhimu wa uwepo wa kila mmoja kwenye mziki wa bongo kama umuhimu wa nyota na mwezi angani.” Barnaba alilidokeza BK. 
 
Kundi hilo kwa sasa lina-bang hewani na ngoma yao ya ‘Why me’ huku wakiwa na mipango mingi ya utendaji wao wa kazi kama Gemenih. Pia waliongeza kitu juu ya Gemenih na THT.
“Kikubwa ni kwamba, watu wasidhani tumetoka au tuna ugomvi na THT ila tumehitimu mafunzo pale na kutunukiwa vyeti nasi ni matunda ya THT na bado tunashirikiana nao kwa kuwapa ushauri hata kuwatungia nyimbo. Kwa ufupi tumewaachia wengine nafasibaada ya sisi kufuzu mafunzo pale.” Amini aliongeza. 
 
Gemenih ipo chini ya meneja aitwaye Moses Clemence ambaye ndiye ana-control mambo yote yahusuyo vijana hao.

HATARI!! MAGUNIA 405 YA BANGI YAKAMATWA KATIKA OPARESHENI YA KUSHITUKIZA ARUMERU, ARUSHA....!!!


Katika Operesheni ya Kuzuia Uhalifu na Madawa ya Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha liliingia kijijini hapo majira ya saa 2 za asubuhi Agosti 13 mwaka huu.

Ilikuwa ni ziara ya kushtukiza katika kijiji hicho hali iliyowafanya wanakijiji kutaharuki na kuanza kukimbia na kutokomea milima wakiziacha nyumba zao zikiwa wazi.

Uongozi wa Kijiji hicho nao ulitoweka kusikojulikana kwa kuhofia mkono wa Jeshi la Polisi.
Kamishna wa Operesheni hiyo ACP Ngonyani alisema safari hii waliamua kwenda baada ya mavuno kutokana na ukweli kwamba zikiwa bado shamabni ni kazi nzito sana ya kufyeka.

POLISI WAMKAMATA ALIYEMUUA BILIONEA ERASTO MSUYA.....!!!


Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa akihojiwa na makachero.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.

“Tumewakamata watu wametupa mwanga mzuri na huyo mfanyabiashara ndiye aliyetoa fedha za kununua pikipiki na siku moja kabla ya tukio zilihifadhiwa nyumbani kwake,” alidokeza polisi mmoja.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 15, 2013.


.

.

HAYA NDIO MAPOKEZI YA FEZA KESSY UWANJA WA NDEGE DAR



Mwakilishi wa Tanzania katika jumba la Big Brother 'The Chase' aliyetolewa Jumapili Agosti 11 Feza Kessy amewasili leo jioni Tanzania katika uwanja wa kimataifa wa Mwl J.K Nyerere jijini Dar es Salaam.

Katika mapokezi watu mbalimbali walijitokeza kumpokea Feza Kessy akiwemo Vanessa Mdee,Mama mzazi wa Feza kessy,ndugu jamaa na marafiki pamoja na Meneja wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania 'Barbara'.




MAJANGAAAAAAA... MTU NA MDOGO WAKE WAOANA HUKO BAGAMOYO....POLISI WAINGILIA KATI....!!!

MWANAFUNZI wa kidato cha pili jina kapuni (16), amejikuta akiozeshwa na wazazi wake kwa mwanaume aliyetambulika kwa jina la Kaizilege Jabiri (31) ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa...
Kaka mtu akitiwa mbaroni
Tukio hilo lilitokea Juni 14, mwaka huu jijini Dar nyumbani kwao Mlandizi, Bagamoyo, Pwani ambako mwanaume huyo alifunga ndoa na binti huyo na kurejea naye nyumbani kwake, Ubungo Kisiwani, Dar huku baadhi ya watu wakihofia uhai wa ndoa hiyo.

Baada ya kuanza maisha ya ndoa kama mke na mume, Agosti 6, mwaka huu taarifa zikafika kwenye Kituo cha Polisi cha Ubungo ambapo maafande walisema hiyo haiwezekani.
“Polisi walipopata habari walisema hakuna ndoa hapo, wakajipanga kwenda kuvamia nyumbani kwa wanandoa hao,” kilisema chanzo.
Dada  mtu akiwa ameshika tama.

Wednesday, August 14, 2013

SHEIKH PONDA ASOMEWA MASHITAKA AKIWA HOSPITALI


 
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda amesomewa mashitaka ya uchochezi na Mwanasheria wa serikali, akiwa wodini MOI anapoendelea kupata matibabu. Sheikh Ponda arijeruhiwa Jumamosi iliyopita akiwa katika mhadhara wa Kiislamu huko mkoani Morogoro. Baada ya kujeruhiwa Ponda alilazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kuhamishiwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) aliposomewa mashitaka. Kesi yake itaendelea pindi atakapopata nafuu.

ANGALIA VIDEO YA HOTUBA YA RAIS KIKWETE YA MAJUMUISHO YA ZIARA YA MKOA WA KAGERA MWISHONI MWA JULAI 2013

KAMATI KUU YA CCM KUAMUA HATMA YA MADIWANI BUKOBA

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na CCM.


Kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho. Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.



Hivyo basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.

AFANDE FEKI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI ABAMBWA LEO HUKO TABATA KINYEREZI

 Askari Bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyekamatwa leo mchana maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake mara baara ya kukamatwa. Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake.
Afande huyo akiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa mchana wa leo akila vichwa maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam.Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake.

MBOWE AANIKA HADHARANI JINSI ANAVYOKOSWA KOSWA KUUAWA ...!!!


Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema amenusurika kuuawa katika matukio matatu yanayotokana na harakati zake za kisiasa.

Akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mji wa Meatu mkoani Simiu jana, Mbowe alisema hata kama atauawa hatasikitika na kwamba Watanzania wasimlilie.

Mbele ya umati huo akiwemo mbunge wa Maswa, John Shibuda, Mbowe alisema kuna watu ndani na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakifanya kila mbinu kuwaangamiza viongozi na makada wa chama hicho.

Mbowe alisema viongozi wa CHADEMA akiwemo yeye mwenyewe wamekumbana na misukosuko mingi, ikiwemo yenye kuhatarisha maisha yao kutoka kwa wanasiasa wasioipenda nchi, lakini kwa neema ya Mungu wamenusurika.


“Leo hii hata kama nikiuawa, naomba Watanzania msinililie. Mbele ya jeneza langu, nizikeni huku mkisema Bwana Alitoa na Bwana Ametwaaa, Jina Lake Lihimidiwe.

MWANAFUNZI ATEKWA NA KUFANYISHWA NGONO KWA SIKU NNE....!!!

 
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Marangu inayomilikiwa na kanisa Katoliki jimbo la Moshi, (jina limehifadhiwa) alitekwa na kukufungiwa kwenye hoteli moja ya kitalii mjini hapa na kufanyiwa vitendo vya ngono kwa muda wa siku nne mfululizo.

Mwanafunzi huyo anadaiwa kutekwa Agosti 6 mwaka huu na kijana mmoja (jina linahifadhiwa) mfanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi (Airtel) mjini Dodoma.

Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumatano, kaka wa mwanafunzi huyo, Joseph Temba, alidai mdogo wake alitekwa na mtu huyo na tayari mtuhumiwa ameshakamatwa.

Alisema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Agosti 10, mwaka huu, katika baa moja akiwa na mdogo wake baada ya raia wema kutoa taarifa za kuonekana kwake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...