Wednesday, August 14, 2013

SHEIKH PONDA ASOMEWA MASHITAKA AKIWA HOSPITALI


 
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda amesomewa mashitaka ya uchochezi na Mwanasheria wa serikali, akiwa wodini MOI anapoendelea kupata matibabu. Sheikh Ponda arijeruhiwa Jumamosi iliyopita akiwa katika mhadhara wa Kiislamu huko mkoani Morogoro. Baada ya kujeruhiwa Ponda alilazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kuhamishiwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) aliposomewa mashitaka. Kesi yake itaendelea pindi atakapopata nafuu.

ANGALIA VIDEO YA HOTUBA YA RAIS KIKWETE YA MAJUMUISHO YA ZIARA YA MKOA WA KAGERA MWISHONI MWA JULAI 2013

KAMATI KUU YA CCM KUAMUA HATMA YA MADIWANI BUKOBA

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na CCM.


Kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho. Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.



Hivyo basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.

AFANDE FEKI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI ABAMBWA LEO HUKO TABATA KINYEREZI

 Askari Bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyekamatwa leo mchana maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake mara baara ya kukamatwa. Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake.
Afande huyo akiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa mchana wa leo akila vichwa maeneo ya Kinyelezi Mnara,Tabata jijini Dar es Salaam.Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake.

MBOWE AANIKA HADHARANI JINSI ANAVYOKOSWA KOSWA KUUAWA ...!!!


Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema amenusurika kuuawa katika matukio matatu yanayotokana na harakati zake za kisiasa.

Akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mji wa Meatu mkoani Simiu jana, Mbowe alisema hata kama atauawa hatasikitika na kwamba Watanzania wasimlilie.

Mbele ya umati huo akiwemo mbunge wa Maswa, John Shibuda, Mbowe alisema kuna watu ndani na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakifanya kila mbinu kuwaangamiza viongozi na makada wa chama hicho.

Mbowe alisema viongozi wa CHADEMA akiwemo yeye mwenyewe wamekumbana na misukosuko mingi, ikiwemo yenye kuhatarisha maisha yao kutoka kwa wanasiasa wasioipenda nchi, lakini kwa neema ya Mungu wamenusurika.


“Leo hii hata kama nikiuawa, naomba Watanzania msinililie. Mbele ya jeneza langu, nizikeni huku mkisema Bwana Alitoa na Bwana Ametwaaa, Jina Lake Lihimidiwe.

MWANAFUNZI ATEKWA NA KUFANYISHWA NGONO KWA SIKU NNE....!!!

 
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Marangu inayomilikiwa na kanisa Katoliki jimbo la Moshi, (jina limehifadhiwa) alitekwa na kukufungiwa kwenye hoteli moja ya kitalii mjini hapa na kufanyiwa vitendo vya ngono kwa muda wa siku nne mfululizo.

Mwanafunzi huyo anadaiwa kutekwa Agosti 6 mwaka huu na kijana mmoja (jina linahifadhiwa) mfanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi (Airtel) mjini Dodoma.

Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumatano, kaka wa mwanafunzi huyo, Joseph Temba, alidai mdogo wake alitekwa na mtu huyo na tayari mtuhumiwa ameshakamatwa.

Alisema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Agosti 10, mwaka huu, katika baa moja akiwa na mdogo wake baada ya raia wema kutoa taarifa za kuonekana kwake.

JAY Z NOMA-AWAPA WAFANYAKAZI WAKE BONAS YA MILION 70 KILA MMOJA-MPAKA MFANYAKAZI WA NDANI

Hip hop mogul na mfanyabiashara mwenye ‘kisu’ cha maana (pesa) Shawn Carter a.k.a Jay Z licha ya kuwa baba mzuri kwa Blue Ivy, mume mzuri wa mkewe Beyonce lakini pia ni boss mzuri (tena sana) kwa wafanyakazi wake baada ya kuamua kuwapa ‘bonus’ ya kutisha (kwa ukubwa) ya mshahara.

Hivi karibuni Jay Z na Beyonce waliamua kurudisha fadhila kwa wafanyakazi hao wapatao 80 kwa kuamua kuwapa bonus ya zaidi ya $46,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 70 kila mmoja kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.

Wafanyakazi waliodondokewa na zali hilo ambalo hawakulitegemea ni wale wa kampuni zake zote, club yake ya 40/40 hadi wale wafanyakazi wao wa nyumba zao 3 za Marekani.

CHELSEA YADUWAZWA, DAVID LUIZ AMCHANA MOURINHO KUWA ANATAKA KUONDOKA KUJIUNGA NA BARCELONA

Hairy moment: David Luiz has told Chelsea he wants to quit for Barcelona, according to Mundo Deportivo
Hairy moment: David Luiz has told Chelsea he wants to quit for Barcelona, according to Mundo Deportivo
Raha kwa Barca: David Luiz amewaambia Chelsea kuwa anataka kutimkia Barcelona
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo
Hairy moment: David Luiz has told Chelsea he wants to quit for Barcelona, according to Mundo DeportivoLuiz amekuwa katika harakati za kujiunga na Barcelona baada ya dili la  Thiago Silva, aliyekuwa akitajwa kujiunga Camp Nou kubuma. Kocha Jose Mourinho hakufurahishwa na kiwango cha Luiz mechi za nyuma, lakini alisema nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 hatauzwa majira haya ya kiangazi.

CHIDI BENZ "SIWEZI KUMALIZA DK 2O BILA KUVUTA"

Rapper Chidi Benz leo kwa mdomo wake mwenyewe amekiri kuwa alikuwa akitumia madawa ya kulevya kwa miaka mingi. Chidi amefunguka leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.Alisema japo hakwenda Nairobi kwaajili ya rehab, mazingira yalimlazimu kutafuta tiba ili aondokane na madhara ya madawa hayo. Alieleza kuwa alipofika jijini Nairobi alikuwa akitakiwa kufanya show nyingi na mwandaaji alimuuliza kama kuna kitu atahitaji ili awezE kufanya show vizuri.
“Nikamwambia Yeah kuna vitu ntavihitaji,” alisema Chidi. “Nikamwambia ‘mimi bana kuna vitu ninavyovitumia nikikaa 20 minutes bila hivyo vitu ni noma nachanganyikiwa na akili tena sina, kwahiyo sijui tutafanyaje’. 
 Akaniambia ‘mimi ntapataje hivyo vitu Chidi na Nairobi ni gharama sana. Nikamwambia ‘mimi pia nina wazo jingine kuna mtu alinitonya kwamba kuna kitu kinaweza kikafanyika na pesa Fulani, pesa nyingi kama milioni 15, 16 hivi za kibongo. 

Akaniambia kikifanyika hicho maanake vinavyofolewa kabisa hivyo vitu vilivyokuwa vinanifanya niwe hivyo. Akaniambia ‘hiyo naijua lakini ni process, ndio maana dunia nzima haifanyi’. Nikamwambia ‘mimi nafanya kwasababu nilishakutwa na vitu vingi mimi ntafanya.”

MAJINA 250 YA WAUZA UNGA NA BANGI NCHINI TANZANIA.



Majina ya watanzania 255 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya   yamejulikana  na  JAMHURI  imeamua kuyachapisha...


 

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa kwenye orodha hiyo wapo watu maarufu na baadhi wamekuwa wakitoa misaada ,huku wengine wakijifanya ni wazee  wa kanisa na kushiriki  shughuli mbalimbali za kijamii....



 Uchunguzi wetu usio na chembe ya shaka  unaonesha kuwa orodha hii ya watu watakaoandikwa hapo chini kwa sasa wapo chini ya uangalizi wa mahakama na polisi..



"Ni kweli kuna watu tumewapeleka mahakamani, huko wamewekwa chini ya uangalizi na wanatakiwa kuripoti  kwa  muda wanaopangiwa.Tunafanya hivyo baada ya uchunguzi wetu kubaini kwa ni kweli  wanahusika na biashara hii haramu."Alisema  Nzowa

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AUGUST 14, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.



.
.

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KWENYE MAZISHI YA BILIONEA ERASTO MSUYA

IMG-20130812-WA0011
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu ERASTO MSUYA





Familia ya marehemu katika ibada ya kumwaga marehemu Erasto Msuya iliyofanyika Jumatatu huko Sakina Arusha





PONDA: RISASI ILINICHANGANYA....!!!


Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema alichanganyikiwa kiasi cha kushindwa kujielewa kwa muda baada ya kupigwa risasi.
 
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi kwenye wodi binafsi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi) alikolazwa jana, Sheikh Ponda alisema kutokana na hali hiyo hakumbuki matukio yaliyofuata baada ya hapo.
“Sikumbuki hata nilipata huduma ya kwanza hospitali gani kwa sababu sikuwa katika hali ya kawaida. Mambo mengine yaliyotendeka kabla ya kujeruhiwa ninayakumbuka vizuri,” alisema Ponda ambaye inasadikiwa kwamba alipigwa risasi ya begani, Ijumaa iliyopita mjini Morogoro.
Alisema alihutubia katika Kongamano la Waislamu kwa muda mfupi akizingatia muda uliokuwa umetolewa kumaliza mkutano huo na baada ya hapo alishuka na kupanda kwenye gari binafsi ambalo lilizingirwa na polisi ndipo akaamua kushuka na kuanza kutembea kabla ya kujeruhiwa.

Tuesday, August 13, 2013

NDAUKA AANZA KUNG'AA ANGA ZA MUZIKI.....!!!

MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka kwa mara ya kwanza amefanya shoo ya aina yake ya nyimbo ya bongo fleva aliyoshirikiswa na kundi la TNG, katika tamasha la sikukuu ya Iddi lililofanyika Dar Live jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo sasa ameamua kufanya muziki ambapo ameweza kushirikishwa single inayoenda kwa jina la  'Crazy Love ' na kundi hilo ambapo siku hiyo ilikuwa maalumu kwake kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hiyo.


 
 Akizungumza na mwaandishi wa habari hii baada ya kumaliza kufanya shoo hiyo, Rose aliweka wazi kuwa kuimba 'live' jukwaani kunatofauti na kazi ya filamu ambayo ameizoea.

Alisema upande wa filamu ni rahisi kurekebisha makosa endapo ukihisi kukosea tofauti na kuimba live jukwaani kwani ukikosea hauwezi kupata nafasi ya kurekebisha hivyo umakini unahitajika katika kazi hiyo.

"Mimi ni msanii na kuimba ni kipaji changu kingine, lakini kwenye uimbaji inahitajika umakini zaidi tofauti na nilikokuzoea" alisema Ndauka.

TCRA YAJIPANGA KUZIFUNGA SIMU ZOTE ZA KICHINA ( SIMU FEKI )


Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.

 
Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.

Zoezi litaanza kwa   kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya  zoezi la kuzima simu kuanza  ili  kuhakikisha kuwa   wananchi  hawaathiriwi  na  zoezi  hilo.

 
Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EPOCA) pamoja na kanuni zake za mwaka 2011.
 

-Bongo5

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...