Saturday, August 03, 2013

SIMBA YAMSAINI RASMI BEKI WA KATI NAHODHA WA TIMU YA TAIFA YA BURUNDI GILBERT KAZE

Klabu ya Simba imekamilisha rasmi usajili wa beki wa kati Gilbert Kaze kutoka Vital O ya Burundi. Gilbert aka Demunga ni mmoja wa mabeki bora walionyesha kiwango kizuri hasa kwenye michuano ya Cecafa iliyopita. Amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba. Gilbert Kaze pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Burundi - na alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa timu hiyo walioiwezesha Burundi kufuzu kucheza CHAN mwakani nchini South Africa.

KESI YA JENGO LA GHOROFA JIRANI NA IKULU LAZIDI KUWANASA WATU WENGI


UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya jengo refu la ghorofa 18 lililojengwa jirani na Ikulu bila kufuata utaratibu unatarajia kuita mashahidi 13 na vielelezo 20 kuthibitisha mashtaka dhidi ya vigogo walioruhusu ujenzi huo.

Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai.

Alikuwa akisoma maelezo ya awali ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi fimbo.

Swai alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Agosti 7 mwaka kwa ajili ya mashahidi wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu wake Richard Maliyaga.

RAIS KIKWETE AMVAA KAGAME, MSHANGAA KWA LUGHA ZA MATUSI NA KEJELI.


RAIS KIKWETE.Rwanda's President Paul KagameRAIS KAGAME.

DAR ES SALAAM. KWA mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete amemtolea uvivu Rais wa Rwanda, Paul Kagame kutokana na kitendo chake cha kumtolea lugha za matusi baada ya kumshauri kukaa meza moja na vikundi vya waasi wa nchi yake (FDLR), huku akimtaka kuacha kukuza mgogoro usiokuwepo.
 

Rais Kikwete alitoa ushauri huo kwa Rwanda takribani miezi miwili iliyopita wakati akizungumza katika kikao cha Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika mapema mwaka huu, mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambao ulikuwa ukij adili suala la amani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Ukanda wa Maziwa Makuu.
 

Ushauri huo pia uliwagusa Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Joseph Kabila (DRC), ambao aliwataka kufanya mazungumzo na waasi wanaopingana na Serikali zao.

HIVI NDIVYO RAIS JAKAYA KIKWETE ALIVYOFUTURU NA WASANII NA WATU WA MEDIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii Mkongwe wa Bongofleva,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy G K.
  Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa bongofleva na muigizaji wa Filamu hapa nchini,atambulikae kwa jina la kisanii Zuwena Mohamed a.k.a. Shilole.

MZEE MAJUTO AFUNGA NDOA YA SIRI NA MSICHANA "MBICHI"....!!!


Kuna taarifa kwamba gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani 'King Majuto' almaarufu mzee Majuto amefunga ndoa ya siri ndani ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani. Tukio hilo limetokea Julai 8, mwaka huu pande za Mbagala Zakhem jijini Dar ambapo mzee Majuto alifunga ndoa na msichana mbichi aitwaye Rehema Omary.

Mzee Majuto aliambatana na wasanii wenzake Suleiman Barafu aliyekuwa mpambe wake na mwingine aliyefahamika kwa jina la utani kama mama Sharon.
Baada ya waandishi wetu kupata taarifa kuhusu tukio hilo, waliwahi kutia timu Mbagala, nyumbani kwa binti huyo.


Baada ya kufika, waandishi wetu walibaini kuwa ni kweli kulikuwa na shamrashamra za ndoa ambayo ilikuwa ikifanyika kwa siri huku watu wakizuiliwa kupiga picha.
Muda mfupi baadaye, gari aina ya Toyota Noah (namba za usajili tunazo) lililowabeba mzee Majuto na wapambe wake liliwasili.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 3, 2013

DSC 6292 d7d2a
DSC 6293 82b43

hakuna makato yoyote kwenye huduma ya Airtel money – “Hakatwi Mtu Hapa”

Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini. Kushoto Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa (kulia) Meneja masoko Airtel money Rwebu Mutahaba.
Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa akiongea na wahandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure itakayo wawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure, pichani Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na Meneja masoko Airtel money Rwebu Mutahaba kwa pamoja wakionyesha Bango la hakatwi mtu wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma za mawasilino leo imezindua ofa kabambe kwa watumiaji wa huduma ya kifedha ijulikanayo kama ‘Hakatwi mtu hapa’ inayowawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa kupitia huduma ya Airtel money bila makato yoyote.

Promosheni ya Airtel money Bure itatoa unafuu wa kiuchumi kwa wateja wengi wanaotumia huduma ya Airtel money.

akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema “Airtel inaongoza kwa huduma bora zenye gharama nafuu nchini, na tunaendelea kutoa huduma zenye ubunifu kwa kuzindua promosheni mbalimbali kwa mwaka mzima.’Hakatwi mtu hapa’ promosheni tunayozindua leo ni mfano na mwendelezo wa dhamira yetu ya kufanya huduma ya Airtel money kuwa suluhisho na huduma bora ya kifedha nchi nzima”.

Kwa upande wake Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa aliongeza kwa kusema “ promosheni hii itawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma na kutoa pesa kwenye mtandao wowote bila makato.

“Tunayofuraha kuweza kutoa unafuu kwa wateja kufanya miamala ya pesa bila makato yoyote na kuwaondolea gharama za kutuma na kutoa fedha zillizokuwepo hapo awali. Tumeamua kufanya hivyo ili kuwawezesha wateja wetu kupata kiasi chote cha pesa zao bila makato yoyote” aliongeza Singano.

Airtel kwa sasa inaendesha promosheni maalumu kwa wateja wake ya Airtel yatosha. promosheni ya ‘Hakatwi mtu hapa’ ni msisitizo unaoonyesha Airtel yatosha ambapo huduma zote ikiwa ni pamoja na kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi, huduma za internet na sasa kwenye huduma ya Airtel money ambayo inakuwa promosheni kabambe , nafuu kuliko zote nchini. Huduma ya Airtel money sasa bila shaka Yatosha

MKOJO NA MAAJABU KWA BINADAMU DUNIANI...!!!

MKOJO UKIWA UMEKINGWA.
Mkojo kama huo ambao mwanaume huyu anajisaidia kwa kificho, kinyume cha sheria hadharani ni bidhaa ambayo inaweza kusaidia jamii kwa sasa. Na mpigapicha wetu 

JOHANNESBURG, AFRIKA YA KUSINI. 


JIULIZE , je, umeenda haja ndogo leo asubuhi au la?

Kama jibu ni ndiyo, basi ujue umemwaga kiasi kikubwa cha nishati ambacho pengine kingeweza kuok oa kiasi cha  fedha za kulipia bili ya umeme nyumbani kwako. Pia, mkojo una manufaa zaidi kwako ambayo huenda hukuyajua.
 

Wanayansi na watafiti nchini Uingereza wamevumbua nguvu za mkojo katika kuzalisha nishati ambayo inaweza kuchaji simu kwa muda wa dakika 25 na pia kumwezesha mteja kutuma ujumbe na kuperuzi intaneti.

Friday, August 02, 2013

MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 2, 2013

DSC 6258 c620d
DSC 6259 f6735
DSC 6260 3cfb2
DSC 6261 a45de
DSC 6262 3c931

DSC 6263 967a5

MKE WA DR. SLAA ATOA KALI MAHAKAMANI....!!!

 
 JOSEPHINE Mushumbusi, mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, jana alisababisha vicheko mahakamani baada ya kushindwa kumtambua mshtakiwa anayedaiwa kumpora maeneo ya SUMA JKT.

Josephine alimuacha mshtakiwa katika kesi yake na kumtambulisha mshitakiwa wa kesi nyingine kuwa ni miongoni wa watuhumiwa waliomvamia.

Hayo yalitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa alipokuwa akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Leonard Chalo.

Washitakiwa katika kesi hiyo ambao wanakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha ni Getisi Mturi, Gake Mwita, Salum Mpanda na Charles Chasens.

Mturi na wenzake wanadaiwa Julai 13, 2011, eneo la Suma JKT makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, walimvamia Josephine na kumpora vitu mbalimbali na kabla ya kufanya uhalifu huo walimtishia kwa silaha.

Josephine alidai Julai 13 mwaka 2011, aliingia ofisini kwake katika jengo la Mawasiliano Tower saa 2.00 asubuhi na kutoka saa 11.00 jioni kwenda nyumbani kwake eneo la Boko akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.

MASAA 48 WALIYOPEWA WAASI WA M23 YAMEISHA ... MAPIGANO KUANZA MUDA WOWOTE ULE



Muda wa saa 48 wa kusalimisha silaha kwa waasi wa March 23(M23), Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umemalizika na wakati wowote mapigano yanaweza kuanza.

Misheni ya Kutuliza Amani ya Umoja wa Mataifa(Monusco) , ilitoa saa hizo zinazomalizika leo na Jeshi la UN litaanza kutumia nguvu kunyang’anya silaha waasi hao.

Taarifa ya Monusco iliyotolewa na Msimamizi wa Misheni hiyo, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz na kusambazwa na Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa jana, inaeleza kwamba, watu binafsi katika eneo la Kivu ya Magharibi ambalo linajumisha Goma na Sake na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama wamepewa saa 48 kuanzia saa kumi jana (juzi) kwa saa za Goma (Jumanne) kuzisalimisha silaha zao.


Taarifa ilisema, “Baada ya saa 10 jioni ya Alhamisi, Agosti Mosi, wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio kwa usalama wa wananchi na Monusco itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kama ilivyoainishwa katika mamlaka na sheria za ushiriki za Monusco.”

"SIONI UHALALI WA KUMSHITAKI WAZIRI MKUU" DPP


MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, amesema haoni mantiki yoyote au uhalali wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), kumshitaki Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Alisema hayo janai wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari, baada ya kufungwa kwa mkutano wa siku tatu wa mawakili wa Serikali wafawidhi, wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi vingine vya Polisi Alisema kauli aliyotoa Pinda bungeni, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu kuhusu Polisi kutumia nguvu kwa wananchi, ililenga wanaokaidi kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria na si kupiga na kuua kama ilivyotafsiriwa na wengi. 

“Sijapata taarifa kwa maandishi juu ya azma ya kumshitaki Waziri Mkuu, lakini Pinda hajavunja sheria kwa kauli yake aliyotoa,” alisema. Alisema kwa jinsi alivyosikia maelezo ya Waziri Mkuu bungeni, kama LHRC wanamshitaki kwa jinai Waziri Mkuu, haoni uhalali wa mashitaka hayo. 

Usahihi wa Pinda Alisema Waziri Mkuu alieleza hatua zinazochukuliwa dhidi ya mvunja sheria, na kufafanua kuwa Mtanzania yeyote ana haki kwa mujibu wa sheria, lakini pia ana wajibu, ndiyo maana vipo vyombo na kila chombo kimepewa mamlaka na wajibu wa kutekeleza. Alifafanua, kwamba kilichoongelewa ni dhana ya mkusanyiko ambayo ni haki kwa mujibu wa Katiba, ikiwemo uhuru wa kukutana, kutoa mawazo na kufanya mawasiliano.

TCHANGIRAI: UCHAGUZI "KICHEKESHO KIKUBWA"

051 68151 
UCHAGUZI wa Rais nchini Zimbabwe ulikuwa ‘kichekesho kikubwa,’ Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amesema, akituhumu udanganyifu wa kura uliofanywa na kambi ya mpinzani wake Rais Robert Mugabe.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Tsvangirai alisema uupigaji kura wa Jumatano ulikuwa ‘upuuzi na si halali’.

Kundi kubwa la waangalizi mapema lilisema kufikia hadi watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.
Chama cha Bw Mugabe ambacho kinadai kushinda, kimekanusha tuhuma hizo kikisema upigaji kura ulikuwa shwari. (HM)


Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Afrika, Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, alisemsa kwenye tathimini yao ya awali kuwa upigaji kura ulikuwa huru na haki.
Makundi mengine ya waangalizi yalisifia hali ya amani katika uchaguzi huo.

Kuhesabu kura ulianza kulianza usiku na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) ina siku tano za kutangaza nani mshindi katika uchaguzi huo.

YANGA KUKIPIGA NA MTIBWA JUMAPILI HII



Afisa Habari wa timu ya Yanga SC, Baraka Kizuguto akiongea na wanahabari leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es Salaam.

Mweka Hazina kutoka DRFA, Ally Hassan, akifafanua jambo juu ya maandalizi ya mechi hiyo.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua matukio kwenye kikao hicho.

URUGUAY KURUHUSU BANGI....!!!


Uruguay

1
Na BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...