JOSEPHINE Mushumbusi, mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA,
Dk. Wilbroad Slaa, jana alisababisha vicheko
mahakamani baada ya kushindwa kumtambua mshtakiwa anayedaiwa kumpora maeneo ya
SUMA JKT.
Josephine alimuacha mshtakiwa katika kesi yake na kumtambulisha mshitakiwa wa kesi nyingine kuwa ni miongoni wa watuhumiwa waliomvamia.
Hayo yalitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa alipokuwa akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Leonard Chalo.
Washitakiwa katika kesi hiyo ambao wanakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha ni Getisi Mturi, Gake Mwita, Salum Mpanda na Charles Chasens.
Mturi na wenzake wanadaiwa Julai 13, 2011, eneo la Suma JKT makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, walimvamia Josephine na kumpora vitu mbalimbali na kabla ya kufanya uhalifu huo walimtishia kwa silaha.
Josephine alidai Julai 13 mwaka 2011, aliingia ofisini kwake katika jengo la Mawasiliano Tower saa 2.00 asubuhi na kutoka saa 11.00 jioni kwenda nyumbani kwake eneo la Boko akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.