Saturday, July 27, 2013

BAADA YA NEY WA MITEGO, KALA JEREMIAH NAYE ATANGAZA NIA YAKE YA KUMPIGIA KAMPENI LOWASSA....!!!




Msanii wa Hip Hop na mshindi wa tuzo 3 za KTMA 2013, Kala Jeremiah amefunguka kwa kuandika waraka mrefu kuelezea jinsi anavyomkubali waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwamba anafaa kuiongoza nchini.

Usome waraka wake huo wote;
Mimi Kala Jeremiah nilikuwa msanii wa kwanza Tanzania kumsema mheshimiwa Edward Lowassa kupitia wimbo wangu uitwao wimbo wa taifa baada ya mheshimiwa kukumbwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond.

Kwa kipindi kile kila mmoja wetu alihamaki sana na kuona kweli mzee wa watu ni fisadi.Kwenye wimbo huo kuna mistari nilisema, ‘mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowassa.

Kwa kuwa mimi ni mzuri sana kwenye kufanya uchunguzi binafsi nilitumia muda mwingi sana kulichunguza swala hili la kashfa hii na baadae niligundua kuwa ni swala la kisiasa, na yalikuwa ni mapito ambayo mwanadamu yoyote hupewa muda wa kupitia magumu ili kupimwa imani yake kwa Mungu.

Baada ya kugundua hayo mwaka jana nilitengeneza wimbo unaoitwa ‘Azimio la Arusha’ ambao upo kwenye album yangu ya Pasaka ambayo iko sokoni tokea mwaka jana.

RAY C ATANGAZA KURUDI KWENYE GAME KWA KISHINDO.... APANIA KUFANYA MAMBO MAKUBWA AGOSTI MWAKA HUU...!!!



Mabibi na mabwana mko tayari kwa ujio mwingine wa Ray- C. Malkia wa kiuno bila mfupa Rehema Chalamila aka Ray-C ametangaza ujio wake rasmi baada ya kuwa chimbo kwa kipindi kirefu toka apate matatizo miezi kadhaa iliyopita.

Ni baada ya siku chache kupita toka Ray-C atamke kuwa anapenda sauti ya ‘dogo lake’ Recho na kuwa atakuja kufanya naye kazi, leo amethibitisha kuwa mwezi Agosti ndio anarudi rasmi kutoka chimboni.
Kupitia akaunti ya Instagram Ray-C aliweka picha ya gazeti moja lililoandika ‘Ray-C kuonekana hadharani mwezi Agosti’, na baada ya followers wake kutaka ufafanuzi ndipo alifunguka kwa kusema “For Sure it’s bout time nw nimewapa muda sana watoto sasa mdada is coming back”.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 27, 2013

DSC 0258 fb197
DSC 0259 4d7d9

AZAM TV YALIPA BILLIONI 6.5 ILI KUONYESHA MECHI ZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA

 
Badhi ya viongozi wa TFF wakisaini mikataba na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam, Said Mohammed (wa kwanza kulia) leo kwenye Ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam.
Televisheni ya Azam inayojulikana kama Azam TV imeingia mkataba wa miaka mitatu wa kuonesha michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambapo mkataba huo umetajwa kuwa na thamani ya Tsh bilioni 6.5
 
Aidha Televisheni hiyo itakuwa na majukumu ya kuonesha mechi za moja kwa moja (LIVE) zisizopungua 60 za Ligi hiyo huku nyingine 180 zikiwa zimerekodiwa.
SOURCE: GLOBAL PUBLISHER

WAZIRI MKUU WA ZAMANI ATAKIWA KURUDISHA MAGARI YA SERIKALI MARA MOJA...!!!



Former Prime Minister Raila Odinga. Through the spokesman Muthui Kariuki, the government also accused the former premier of putting a siren on one of the cars and using it to manoeuvre through traffic in the city.

In Summary


  • The spokesman was, however, dismissed last evening by Cord deputy minority leader Jakoyo Midiwo, who said two former presidents who had the same status as the former PM, had not returned anything to the government.
The government Thursday accused former Prime Minister Raila Odinga of failing to return six government vehicles in his possession almost four months after leaving office.

Through the spokesman Muthui Kariuki, the government also accused the former premier of putting a siren on one of the cars and using it to manoeuvre through traffic in the city.

“He is forever mourning that the government is not giving him recognition, yet he has refused to return six government vehicles and has gone on and bought an illegal siren and is forever driving all over town using the wrong lanes,” the spokesman said yesterday.

STARS WAKIWA MAZOEZI KUPAMBANA NA CRANE LEO




 Wachezaji mbalimbali wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Satrs' ambao wanasakata kabumbu ndani ya nchi wakijifua katika Uwanja wa Taifa wa Mandela uliopo Nambole nchini Uganda. Stars ipo nchini Uganda na leo inataraji kushuka katika dimba la uwanja huo kumenyana vikalina The Crenes ya Uganda kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani CHAN.

Moja ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya leo (Julai 27 mwaka huu) dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.

POLISI AZUA BALAA MKUTANO WA CHADEMA NUSURA APIGWE

Na Bryceson Mathias, Kikombo
ASKARI Polisi wa Kata ya Kikombo  aliyejulikana kwa jina Moja la Sivanus (pichani), Jana alizua Tafrani kwenye Mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya Kumnyanganya Kipaza Sauti (Mike) Katibu wa Wilaya wa Dodoma Mjini, Jella Mambo.
Silvanus alizua hayo Julai 26, ambapo alinusurika Kipigo cha Wananchi  waliokuwa na hasira kwa kufanya tukio hilo, ambapo walidai hata kungekuwa na makosa ya Matamko au kitu kingine chaochote, hakustahili kuingia jukwani na kumnyang’anya Kipaza sauti Katibu huyo.
Askari Silvanus aliyeonekana kulewa na kuwaacha wenzie kwenye gari, alichukuwa hatua hiyo, Mambo alipomtambulisha aliyekuwa Mgombea wa Chadema Kata hiyo, Yona Kusaja, kwamba, uchaguzi uliopita Kusaja hakushindwa ila Chama Tawala (CCM) kilichakachua kura zake na kutoa vitisho kwa wapiga kura.

Friday, July 26, 2013

HUYU NDO MSANII ALIYETANGAZA KUMPORA MUME WA AUNT EZEKIEL... !!!

KATIKA hali isiyo ya kawaida msanii anayechipukia katika filamu za Kibongo, Isabella Fransis ‘Vai wa Ukweli’ anamtafuta ubaya gwiji katika tasnia hiyo, Aunt Ezekiel kwa kusema anamtamani mumewe.

Vai wa Ukweli bila ya kupindisha maneno amedai kuwa hapati usingizi kutokana na kumzimia Sunday Demonte ambaye ni mume wa Aunt.


Akizungumza na mwandishi wetu, Vai alisema ili kuonesha kuwa anachokisema kinatoka moyoni mwake, amekata vipande vya picha za Dimonte na kuvibandika chumbani kwake.

 “Kusema ukweli nampenda sana Sunday na sijaanza kumpenda leo wala jana kwani namfahamu tangu zamani alipokuwa Kariakoo,” alisema Vai.

Msanii huyo chipukizi alisema anamuonea wivu Aunt kwa kuamini kuwa anafaidi sana kwa kuwa na mwanaume huyo.
 

Kwa upande wake Aunt alishangazwa na taarifa hizo na akaomba atafutwe baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ajue cha kufanya.

FABREGAS AFUNGUKA, ATAMANI KUJIUNGA NA MOYES, VAN PERSIE OLD TRAFFORD


Uncertain future: Cesc Fabregas could leave Barcelona for Manchester United 
Haijulikani hatima yake: Cesc Fabregas  anaweza kujiunga na Manchester United
Lakini ukweli ni kwamba  Fabregas amewaambia maswahiba wake wa England kuwa anataka kuondoka Camp Nou, na hii inawapa moyo zaidi kumnasa.

Inafahamika kuwa Fabregas amevutiwa na ahadi nzuri ya kucheza muda wote katika kikosi cha United na anapenda kujiunga na nyota mwenzake wa zamani wa Asernal, “Hakunaga” Robin Van Persie ambaye kwa sasa ndio roho ya ushambuliaji ya pale Old Trafford.

MZEE SMALL ANAENDELEA VIZURI KIASI,LAKINI BADO ANAHITAJI MSAADA WETU WADAU


Taarifa ya Mrejesho : Hali ya Msanii nguli wa maigizo hapa nchini Tanzania, Ndg
Said Bin Wangamba almaarufu kama Mzee Small inaendelea vizuri, na
ANASHUKURU sana kwa wale wote wanaomkumbuka katika kipindi hiki kigumu
cha maradhi. Kwa sasa anaweza kujikongoja taratibu mwenyewe.,

Anaendelea na mazoezi ya kila siku, na kubwa ni dozi ya dawa kwa ajili  ya kumsaidia kuondoa uvimbe uliogundulika miezi kadhaa iliyopita,  kichwani mwake ambapo dozi moja tu inagharimu takribani 30,000TZS pamoja
na mahitaji mengine ya lazima ya kila siku,
 Kwa yeyote atakaeguswa  tafadhali unaweza kuwasiliana na Mzee wetu kupitia, M-PESA kwa kutumia  namba ya Said Ngamba (Mzee Small) 0754647265 na TIGO PESA kwa kutumia  namba ya mkewe 0658111311,

Changamoto: Ni Wakati MUAFAKA Sanaa kuwa Ajira Rasmi na yenye MAPATO STAHIKI, Alituchekesha na kutuondolea uchovu kwa kipaji chake, nasi tumkumbuke na kumuenzi,
 
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma

MAJANGA MADANGURO YA MAKAHABA YAZIDI KUFUMULIWA....!!!


 
 Hili ni sakata la  kikongwe mmoja anayedaiwa kumiliki idadi kubwa ya madanguro katika uwanja wake na kuwapangisha makahaba katika eneo maarufu kwa jina la Kijiji cha Makahaba.
Mwandishi wetu alipokea ujumbe mfupi ulioelezea ufuska unaofanywa na mabinti ambao hupewa eneo na kujenga vibanda kisha kujiuza kwa bei chee katika kijiji hicho maeneo ya Kigamboni jijini Dar.


Bada ya simu hiyo, uchunguzi wetu  ulibaini kwamba, eneo hilo linalofanyiwa ufuska huo linamilikiwa na kikongwe aliyejitambulisha kwa jina la mzee Matutu akidaiwa kuendesha maisha kwa biashara hiyo ya madanguro.
 
Baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuwa ni kweli jambo hilo linafanyika eneo hilo,waandishi walivamia eneo la tukio wakiwa na mjumbe wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina la Abbas na kujionea madanguro yaliyojengwa kwa mstari ambapo milango yake iliachwa wazi huku ndani wakionekana mabinti wakiwa wamejilaza kihasarahasara wakiwatega wateja wanaopita katika mtaa huo.

MAAJABU: BINTI ALIYEZALIWA BILA MACHO WALA PUA ATAKIWA KUTOA UBAVU WAKE ILI AFANYIWE UPASUAJI...!!!

Msichana Brave Cassidy Hooper (17) kutoka Charlotte, Kaskazini mwa Carolina Marekani aliyezaliwa bila pua wala macho anategemea kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kurekebisha uso wake.

u-4
Brave anategemewa kufanyiwa upasuaji huo (July 31) mwaka huu ambapo inategemewa sehemu ya mfupa utaondolewa katika ubavu wake kwaajili ya kutumika kutengeneza paji la uso wake, mfupa huo utasaidia kama kiunganishi cha pua mpya atakayowekewa.

IRENE UWOYA AREJEA NCHINI KUTOKA KWA MSWATI - AMEAIDIWA MAMBO MAKUBWA

 
Mwigizaji Irene Uwoya amerejea nchini toka nchini Swaziland alipokuwa kwa takribani wiki tatu.
Irene Uwoya aliyerejea nchini leo hii amerejea na salamu toka nchini Swaziland alizoziandika kupitia ukrasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii alisema…
 
“Mswat anawasalinmu sana! Nahiv karibun atatinga hapa nakanipa kibali chakufanyya move na ful suport...I wl prove u wrong...try me”
 
Akimaanisha, amerejea nchini na Mswati amnawasalimia sana na amesema atakuja nchini hivi karibuni na amenipa kibali cha kufanya Filamu na atanisaidia kwa kila kitu. Nijaribu nitakuthibitishia kuwa umekosea (Kwa Kiswahili fasaha).
 
Bado tunamtafuta Irene amabye namba yake ya simu haipatikani kujua kama kauli hii ni ya kweli au anawatania tuu mashabiki wake.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 26, 2013


DSC 0095 1cb01
DSC 0096 51ada

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...