Linah akiwa katika pozi kali.
Mrembo na mwanamuziki wa kike nchini,
Linah Sanga amezikanusha ripoti zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na
rapper Kimbunga na kudai kuwa ameshangazwa mno na taarifa hizo.
Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo
mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina
yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika:
“Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela
mavi mambo ya kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa
kosa la kumbaka msanii lina.”
Bongo5 imezungumza na Linah ambaye
amesema amepigiwa simu na watu wengi wa karibu kumuuliza suala hilo
wakiwemo, Barnaba, Ditto, Amini na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown.
Amesema Soudy alimwambia kuwa ameziona taarifa hizo kwenye Facebook kwenye akaunti ya Kalapina.