Mapumziko: Giggs, juu, na Wilfried Zaha chini wakipumzika ufukweni
Mabingwa
soka nchini England, klabu ya Manchester United leo hii imefanya
mazoezi mazoezi ufukweni mwa bahari ambapo walisafiri kutoka bandari ya
Sydney kwenda Ufukwe wa Bondi kwa njia ya boti.
Mazoezi
hayo yamefanyika katika bichi ya Bondi kabla ya kukwea pipa kuelekea
nchini Japan kuendelea na ziara ya ya kujianda na msimu mpya wa ligi kuu
soka nchini England.
Vijana
hao wa David moyes watakuwa na mechi tano za kirafiki nchini Japan na
jumanne ya kesho kutwa watashuka dimbani kucheza na Yokohama F-Marinos
mjini Yokohama.
Kufuatia
ushindi wa mabao 5-1 walioupata jana dhidi ya A-League All Stars ,
kikosi hicho leo asubuhi kimefanya mazoezi fukwe za Bond.
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
No comments:
Post a Comment