CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefanikiwa kunasa siri za mipango ya hujuma zilizokuwa zimeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne za Jiji la Arusha, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika, zimebainisha kuwa CHADEMA katika uchaguzi huo kilifanikiwa kushinda kata hizo baada ya kuvunja ngome ya CCM iliyok
uwa ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba.
Kwa mujibu wa habari hizo, mipango karibu yote iliyokuwa ikifanywa na CCM, ikiwemo halali na haramu, ilivuja na kufika mikononi mwa wapinzani wao ndani ya muda mfupi hata kabla ya utekelezaji.
Imedaiwa kwamba baadhi ya watu waliokuwa katika kambi ya CCM, waliamua kwa siri kufichua mipango hiyo na kuifikisha kwa mahasimu wao kutokana na kile kilichodaiwa kuchoshwa kushiriki katika mambo ya kidhalimu.
Habari zinasema maofisa kadhaa wa CCM ambao wamekuwa wakiratibu na kusimamia mipango karibu yote miovu dhidi ya wapinzani, waliamua kwenda kinyume na makubaliano hayo, na kwa njia ya siri wakafanikiwa kutoa mpango mzima hadharani.