HIVI karibuni mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa akifuturu na hawara yake, Penniel Mungilwa ‘Penny’, kitendo ambacho kimewashangaza wengi na baadhi kufikia hatua ya kumponda kuwa anakwenda kinyume na Uislam.
Tukio hilo lilijiri nyumbani kwa Diamond maeneo ya Sinza- Mori jijini Dar ambapo mbali na mastaa hao, pia walikuwepo waumini wengine wa dini hiyo walioalikwa katika chakula hicho kitakatifu.
Waumini wamponda
Wakizungumza na gazeti hili mara baada ya kumuona Penny ambaye ni demu wa Diamond akiwa eneo hilo, baadhi ya waumini walisema walishangazwa na uwepo wake kwani sheria ya dini ya Kiislam hairuhusu kuwa karibu na kimada hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Walisema, Diamond hatakiwi kuwa karibu na Penny si kwa kipindi hiki tu bali hata baada, mpaka pale ambapo atatoa mahari na kuozeshwa kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislam.