Mabeki wa Toto African, Evarist Maganga (kushoto) na Peter
Mutabuzi wakimkaba mshambuliaji wa Azam Brian Umony. Beki Mutabuzi
amejiunga na Kagera Sugar kwa ajili ya msimu ujao wa ligi. Picha na
Michael Matemanga.
*********
Mosses
Oloya wa Uganda anayecheza soka la kulipwa nchini Vietnam anaweza akawa
ndiye mchezaji anayetikisa zaidi kwenye usajili wa soka la Bongo kwa
timu 14 zinazojiandaa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Oloya
anamudu vyema kucheza nafasi ya winga wa kushoto pamoja na kulia kama
ilivyokuwa kwa mfungaji hatari wa Simba, Emmanuel Okwi aliyetua klabu ya
Etoile du Sahel ya Tunisia Januari mwaka huu, baada ya kupata mafanikio
makubwa akiwa na Simba.