
SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili, kilichomfanya Diamond kufikia hatua ya kumtongoza na kutoka naye kimapenzi, ni kitendo cha Uwoya kutoa maneno ya kumponda huku akionesha waziwazi hali ya kumchukia kila walipokutana.
UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND
“Unajua Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na mara nyingi alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa zikimfikia mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo ndiyo zilichochea.