Monday, July 01, 2013
WAPENZI WADONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI...!!!
Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.
Wawili
hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la
makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa
wameegemea kufunguka.
Mashuhuda
walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao
walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje.
Kwa
mujibu wa The Sun, chanzo kimoja cha habari kilisema: "Huku wawili hao
wakiwa wameshikamana vilivyo, walianguka nje ya jengo hilo."
Picha za kuogofya zimefichuliwa kwenye tovuti za nchini humo zikionesha wapenzi hao wakiwa wamefunikwa kwa mashuka na polisi.
Damu ilitapakaa kwenye njia ya waenda kwa miguu karibu na wapelelezi wanaonekana wakichunguza eneo la tukio.
Miili
ya wapenzi hao ilipigwa picha karibu na baiskeli ambayo ilikuwa
imelazwa chini, lakini hakukuwa na ripoti zozote kwamba yeyote chini
alikuwa amejeruhiwa katika ajali hiyo.
Ripoti zinasema kwamba madirisha hayo kwenye jengo hilo la makazi yalikuwa hayana ubora unaotakiwa.
Inafikiriwa
kwamba mwanaume huyo na mwanamke wanawezekana walikuwa wakijaribu
kujipooza kando ya dirisha hilo ndipo tukio hilo likatokea.
Haikufahamika ni umbali gani kutoka juu wawili hao walikuwa wakati wakianguka.
Wuhan ni jiji maarufu zaidi lililopo katikati ya China.
Ukiwa na historia ya miaka 3,500 ni moja kati ya miji mikongwe na iliyostaarabika katika China.
HUYU NDIYE MWANAMKE ALIYEMKATA UUME MUMEWE AFUNGWA MAISHA GEREZANI...!!!
Mwanamke mmoja wa California ambaye alituhumiwa kukata uume wa mumewe kabla ya kuutupa kwenye mashine ya kusagia taka amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Catherine
Kieu, mwenye miaka 50, alipatikana na hatia ya mashitaka ya kutesa na
kosa la kuharibu viungo vya mwili katika shambulio la Julai 11, 2011 na
kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, lakini anaweza kufikiriwa kupewa
msamaha baada ya kutumikia miaka saba.
Alitiwa hatiani Aprili kwa kila kosa moja la kutesa na kuharibu viungo vya mwili.
Muathirika, anayefahamika kama Glen wakati wote wa kesi, alikuwa mahakamani kwa ajili ya hukumu ya jana.
"Natumaini
hii itakuwa mara ya mwisho kabisa ninayoweza kumwona," alisema Glen.
"Najihisi nafuu kiasi fulani, na ilikuwa siku ya huzuni kubwa kwangu."
Muathirika huyo alikimbizwa hospitali, lakini upasuaji kurejesha uume wake haukufanikiwa.
Wakati
wa kesi hiyo, muathirika huyo mwenye umri wa miaka 60 alitoa ushahidi
kwamba uume wake hauwezi tena kuunganishwa mahali pake na kwamba anahisi
kama ameuawa.
Kieu
alikuwa na wivu na hasira kuhusu mipango ya mumewe kumpa talaka sababu
alimwona rafiki yake wa zamani wa kike, upande wa mashitaka ulisema.
Sunday, June 30, 2013
LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMIE MAMBO YA USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA AKIWA TANZANIA
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Alisema jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.
Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.
Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.
Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."
JK AMGEUKA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI JOSEPH WARIOBA
RAIS
Jakaya Kikwete amemgeuka Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Jaji Joseph Warioba, kwa kuridhia azimio la Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kutaka uwepo muundo wa serikali mbili.
Rais
Kikwete ambaye juzi aliongoza kikao cha Kamati Kuu (CC), mjini Dodoma,
aliridhia azimio hilo, huku akijua fika kuwa ndiye aliyemruhusu Jaji
Warioba kuingiza kipengele hicho kwenye rasimu wakati alipoifikisha
mbele yake kabla ya kuitoa hadharani.
Kutoka
na hali hiyo, Kamati Kuu imewataka wanachama wao wote kupitia mabaraza
ya CCM kuhakikisha wanakubaliana na msimamo wa chama wa kupinga muundo
wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Zanzibar, waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa Kamati Kuu
imepitisha azimio la kutaka mabaraza ya Katiba ya chama hicho yajadili na kuridhia msimamo wa kuwa na serikali mbili.
Kamati
Kuu ya CCM imekuja na mapendekezo ya namna ya kurekebisha kasoro kubwa
za Muungano ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikiwa na
Wazanzibari.
BEYONCE ATINGA VAZI LA KANGA, ILIYOTENGENEZWA NA MTANZANIA
Christina (katikati)
Utajiskiaje
kuona Beyonce akiwa amevaa vazi lililotengenezwa kwa kanga yenye
maneno ya Kiswahili? ‘Wawili Ninyi Yawahusu….’ yanasomekana maandishi
kwenye vazi alilolivaa mwanamuziki wa Marekani,
Beyonce Knowles.
Vazi
hili alilolivaa Beyonce kwenye moja ya show zake za tour ya Mrs
Carter, limetengenezwa na mwanamitindo wa Tanzania aishie jijini London
Uingereza, Christine Mhando mwenye brand ya Chichia London.
Chichia London ndio brand iliyo maarufu sana nchini Uingereza kwa
kutengeneza nguo za Kitanzania kwa kutumia Kanga na material mengine
Kiafrika.
Hizi ni baadhi ya nguo alizotengeneza.
LOWASSA AWATEKA WAENDESHA BODABODA ARUSHA...!!!
Wafanyabiashara
maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu na
Diwani wa Mererani, Mathias Manga, ndiyo waliyobuni wazo hilo la
kuwaanzishia mfuko vijana wa bodaboda.
Katika harambee hiyo, sh milioni 84 zilipatikana huku Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia sh milioni 10 na pikipiki 1WAZIRI
Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema usafiri wa pikipiki maarufu
kama bodaboda ni sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusaidia
kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Akizungumza
katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu
mkoani Arusha, Lowassa alisema sera hiyo ni ya kuwakomboa vijana.
Alisema kuwa kitendo cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda ni mfano kwa wafanyabishara wengine nchini.
“CCM
ni chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji
kunyanyuliwa kimaisha, kitendo hiki cha wafanyabisharaa wa Arusha ni cha
kuunga mkono sera ya CCM,” alisema.
Lowassa
alisema tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka na kwamba
wasipowasaidia vijana kuondokana na tatizo hilo amani itatoweka.
“Ndiyo
maana CCM katika ilani yake ya uchaguzi imeliweka hilo na pia
kulisisitiza katika vikao vyake vya juu vya Mkutano Mkuu pamoja na
Halmashauri Kuu,” alisema.
HUU NDIO WOSIA WA MZEE MANDELA NA MAHALI ANAPOPENDA KUZIKWA
Mzee
Nelson Mandela ameandika wosia kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4
ambamo ameagiza azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu
zake huko Qunu, imebainika.
Rais
huyo wa zamani wa Afrika Kusini, mwenye miaka 94, bado yuko mahututi
lakini lakini hali yake inaimarika hospitalini mjini Pretoria ambako
amekuwa huko kwa siku 21 zilizopita akitibiwa maambukizi kwenye mapafu.
Mnamo
Januari 1996, wakati akiwa bado Rais, Mzee Mandela aliripotiwa kuandika
wosia ambao aliagiza kufanyiwa maziko ya kawaida karibu na kijiji
ambako alikulia kwenye rasi ya Mashariki.
Alisema
kwamba wakati akifurahia kumbukumbu ya kulitumikia taifa hilo mjini
Pretoria angetaka kuzikwa katika eneo la familia hiyo na kuwekewa jiwe
la kawaida kama alama ya lilipo kaburi lake.
Gazeti
la South African Mail na Guardian yaliripoti yakimnukuu rafiki wa siku
nyingi wa familia akisema: "Hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la
kufikiriwa, lakini hakuwahi kutaka chochote cha ufahari".
Licha
ya ukweli kwamba mauzo ya kitabu cha Mandela cha Long Walk To Freedom,
na michoro yenye jina lake, kumpatia mamilioni ya pesa kwa hadhi wosia
wake uliripotiwa kutosha kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4.
OBAMA ATOA SABABU YA KUTOFANYA ZIARA KENYA...!!!
Rais Barack Obama. |
Wakati
Rais wa Marekani, Barack Obama amesema asingeweza kufanya ziara Kenya
kutokana na Rais wake, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Rutto
kukabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa
Kivita (ICC), pia amehadharisha Afrika kuhakikisha kuwa kampuni za
kigeni zinaajiri wafanyakazi wazalendo ili wawekeze nchini mwao.
Alitoa
kauli hizo mbili kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari na baadaye alipozungumza na viongozi vijana wa
Afrika akiwa katika ziara yake nchini Afrika Kusini.
Akizungumza jioni jana na vijana katika eneo la Soweto jijini Johannesburg, Obama alisema ataangalia uwezekano wa kwenda Kenya akiwa bado madarakani kwani bado ana miaka mitatu na miezi saba ya uongozi wake.
Akizungumza jioni jana na vijana katika eneo la Soweto jijini Johannesburg, Obama alisema ataangalia uwezekano wa kwenda Kenya akiwa bado madarakani kwani bado ana miaka mitatu na miezi saba ya uongozi wake.
Saturday, June 29, 2013
MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU "BRIAN DEACON" AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.
Brian Deacon akiigiza kama Yesu ndani ya filamu ya JESUS.
Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS'' |
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.
HII NDIO SABABU YA KAJALA KUNYOA BONGE LA UPARA...!!!
Mwigizaji
aliyerudi uraiani hivi karibuni Kajala Masanja amefanya mabadiliko
makubwa ya mtindo wake wa nywele baada ya kunyoa kipara “kikavu”
kichwani mwake.
Katika
picha alizozitoa mwigizaji huyo kupitia kwenye mtandao jana, mwigizaji
huyo ameonekana akiwa na kipara tofauti na alivyozoeleka na nywele
nyingi siku za nyuma.
Bongomovies.com
tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili kujua “kunani”?? na staili hiyo
na tulimpigia simu na maongezi yalikuwa kama ifuatavyo:
Bongomovies.com: Mambo kajala, mzima?
Kajala: Mzima, kwema?
Bongomovies.com: Kwema kabisa, vipi tena na kipara kichwani?
Kajala:
Aha,..Siunajua tena mishe mishe, nipo na shoot movie yangu mpya ndo
mana imenibidi ninyo kipara maana inanilazimu kuonekana hivyo ndani na
Filamu hiyo.
Bongomovies.com: Okay, na itaitwaje?
Kajala: Itaitwa Heart attack
Bongomovies.com: Umewashirikisha nani na nani humo ndani?
Kajala: Atakuwepo Hemedi na mastaa wengine Kibao, kifupi ni bonge la movie yani.
Bongomovies.com: Basi tunaisubiri kwa hamu sana
Kajala: Pamoja sana.
MKE AMFUMANIA MUMEWE AKIWA NA KIMADA GESTI HUKO SINZA, MUME AMKIMBIA MKEWE AKIWA UCHI WA MNYAMA
Tukio
hilo lililowashangaza wengi lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita
katika gesti moja iliyopo Sinza jijini Dar. Awali Flaviana na bwana wake
huyo walichukua chumba baada ya kushindwa kurudi nyumbani kutokana na
kuzidiwa na kilevi.
Ilikuwaje fumanizi likatokea?
Ilielezwa
kuwa wakati wawili hao wakiingia kwenye chumba cha gesti hiyo, Flaviana
alikuwa bwii hivyo ‘kuzima’ kwenye kochi na kushindwa kufanya chochote.
“Wakati
Aron akiwa chumbani pale, alifika shosti wa Flaviana aitwaye Dina na
kwa kuwa Flaviana alikuwa hajitambui, wawili hao walianza kupeana
malavidavi.
“Flaviana
akiwa amelala alikuwa kama vile anasikia watu wakishughulika lakini
alishindwa kufanya chochote kutokana na kuzidiwa na pombe.
“Wale
wakaendelea kubanjuka. Ilipofika saa 12 asubuhi Flaviana akapata nguvu
na kuamka kwenda kujisaidia, aliporudi akabaini shosti wake amemsaliti
na ndipo alipoanzisha timbwili,” alidai mtoa habari wetu.
Flaviana apigia simu mapaparazi
Wakati
timbwili hilo likiendelea chumbani hapo, Flaviana alipata mwanya wa
kuwapigia simu mapaparazi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na
kumshuhudia Dina akiwa ndani ya Bajaj huku akivaa nguo kabla ya
kumuamuru dereva kuondoka kwa spidi.
Naye
mwanaume ambaye alikuwa ndani ya chumba cha gesti hiyo, aliposikia
waandishi wamefika, alitokea mlango wa nyuma akiwa amevaa ‘boksa’ na
tisheti, akaacha suruali yake chumbani hapo.
Akizungumza
na Risasi Jumamosi huku akiwaonesha mapaparazi kitanda kilichokuwa
vululuvululu, kilichotumika katika usaliti huo pamoja kondom, Flaviana
alisema: “Nimeumia sana, yaani nimesalitiwa nikiwa humuhumu chumbani,
Aron kanidhalilisha sana na huyo Dina naye kumbe siyo mtu, nitahakikisha
namsaka nimshikishe adabu.”
MAMIA NCHINI AFRIKA KUSINI WAJITOKEZA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI YA KUPINGA KUJA KWA RAIS OBAMA WAKATI ALIPOTUA JANA JIONI KATIKA JIJI LA PRETORIA
Waandamaji
Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Rais Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa
Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika jana Jioni wakati Raisi
Obama alipotua Katika Jiji Hilo jana Jioni Juni 28
Waandamaji
Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Rais
Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini
Jioni ya Juni 28
Waandamaji
wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani
wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Rais Obama Nchini Humo Mapema jana wakati Rais Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ametokea
Nchini Senegali na Kutua Nchini Afrika Kusini huku Akihitisha Ziara
Yake Nchini Tanzania wiki ijayo.
Mmoja
wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza
kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Rais
OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na
kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo. Mwandamaji huyu
amebeba bango jana Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya
Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini
Mwao. Picha Zote na REUTERS/AFP
Friday, June 28, 2013
BIBI YAKE OBAMA MAMA SARAH OBAMA KUJA TANZANIA KUMSALIMIA MJUKUU WAKE ATAKAPOWASILI DARESALAM.
SIKU CHACHE KABLA YA ZIARA YA RAIS WA
MAREKANI KUJA NCHINI TANZANIA IMEFAHAMIKA KUWA BIBI YAKE NA RAIS OBAMA
MAMA SARAH OBAMA ANATARAJIA KUJA NCHINI TANZANIA KUJA KUMSALIMIA MJUKUU
WAKE HUYO.
AKIZUNGUMZA JUZI KIJIJINI KWAKE ENEO LA
KWEGERO HUKO KISUM BIBI HUYO ALIEZALIWA MWAKA 1922 AMESEMA KUWA HAJISKII
VIBAYA OBAMA KUTOITEMGELEA KENYA KWANI ANAJUA KUWA OBAMA NI RAIS WA
TAIFA KUBWA DUNIANI, HIVYO ANAKUWA NA RATIBA AMBAYO INAZINGATIA MAMBO
MENGI NA NI VIGUMU SANA KUIVUNJA.
BIBI HUYO AMEENDELEA KUSEMA KUWA ANAJISIKIA
FURAHA KUONA MJUKUU WAKE HUYO KUJA TANZANIA KWANI HISTORIA INAONYESHA
KUWA KABILA LA KIJALUO LINAMUINGILIANO MKUBWA KATI YA NCHI HIZI MBILI ZA
TANZANIA NA KENYA HIVYO WAO WANAAMINI KUWA OBAMA AMEITEMBELEA NCHI YA
NYUMBANI KWAO.
NAY WA MITEGO NA DIAMOND KUJA NA NGOMA MPYA..."SALAMU ZAO"
Baada
ya kutamba na Muziki Gani, Diamond na Nay Wa Mitego wako mbioni
kuachia ngoma nyingine hivi karibuni baada ya kupembua ipi ianze kati
ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’.
Nay
ameiambia mpekuzi kuwa kuna nyimbo tatu ambazo zipo tayari, Salamu
Zao, Kwa Masela na Utakula Jeuri Yako, hawajajua ipi itaanza kutoka
kwasababu kila mmoja yupo katika tour zinazoendelea.
Wamesema wakikaa wakashauriana na wadau mbalimbali ndipo watakapoamua mzigo upi uingie mtaani kwanza.
“Kuna
kazi ambazo zinakuja hivi karibuni ambazo nimefanya na Diamond lakini
mpaka sasa hivi sijajua ni ipi ambayo itaanza kutoka lakini tutawaita
wadau wachague ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’ ambazo zipo
tayari na ‘Utakula Jeuri Yako’ nimefanya mwenyewe...
"Ilibidi
tutoe nyimbo ambayo tumefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi hakuna
maamuzi ya moja kwa moja tuitoe au kila mtu atoe ya kwake au
tutaendelea na project yetu iliyoendelea, kwahiyo wadau wakae mkao wa
kula,” amesema Nay.
Subscribe to:
Posts (Atom)