Rais Barack Obama. |
Wakati
Rais wa Marekani, Barack Obama amesema asingeweza kufanya ziara Kenya
kutokana na Rais wake, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Rutto
kukabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa
Kivita (ICC), pia amehadharisha Afrika kuhakikisha kuwa kampuni za
kigeni zinaajiri wafanyakazi wazalendo ili wawekeze nchini mwao.
Alitoa
kauli hizo mbili kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari na baadaye alipozungumza na viongozi vijana wa
Afrika akiwa katika ziara yake nchini Afrika Kusini.
Akizungumza jioni jana na vijana katika eneo la Soweto jijini Johannesburg, Obama alisema ataangalia uwezekano wa kwenda Kenya akiwa bado madarakani kwani bado ana miaka mitatu na miezi saba ya uongozi wake.