Stori
ya kwanza ni ya Mbunge wa Nkasi Ally Keissy June 18 2013 bwana
alivunja rekodi ya kuwa mbunge aliechekesha watu wengi wakiwemo wabunge
bungeni, sio tu kwa sababu ya kutoa vichekesho lakini pia ni kwa namna
alivyokua akieleza mambo pamoja na kuikosoa Serikali.
Mbunge wa Nkasi Ally Mohamed Keissy.
Anakwambia
‘Twende Kigoma, Mwanza, Tabora, Mpanda, Shinyanga tuwaulize watu
mnataka reli au viwanja vya ndege… mtashangaa wenyewe, vipaumbele gani
mnapeleka viwanja vya ndege? mtu gani wa Tabora anapanda ndege kama sio
Mbunge, DC na Mkuu wa mkoa… ? ni Treni…… hawataki viwanja vya ndege,
viwanja vya ndege baadae….
kwanza ndege zenyewe zikwapi? mna ndege nyie???? mabilioni ya hela mnajenga viwanja vya ndege… ndege hatuna, wapanda ndege ni nyie wenyewe Wabunge na Mawaziri… jamani tutulie tuweke vipaumbele ambavyo vinaweza kusaidia Wananchi na uchumi wa nchi, mtapakia mizigo, madebe mawese kwenye ndege? migebuka kwenye ndege? acheni mambo ya kurukiakurukia ndege zenyewe hamna”