Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani
mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne
na wengine kujeruhiwa.Bomu hilo
lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama
hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika
katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya
wananchi.Hilo ni tukio la pili la
bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu
lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,
Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine
kujeruhiwa.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.
Mama akikimbizwa hospitali kupata matibabu.