WAKATI Serikali ya Tanzania ikiendelea na maandalizi ya kupokea msafara wa watu 700 waliotarajia kuingia nchini kwa ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama, Rais huyo amesitisha safari yake.
Ikulu ya Marekani imetangaza kwamba msafara wa Rais Obama kuja kutembelea Bara la Afrika haitakuwepo tena,baada ya serikali ya nchi hiyo kukosa fedha itakayoweza kugaramia safari ya Rais huyo.
Taarifa
iliyonaswa na kutoka katika mitandao mbalimnali nchini Uingereza na
Marekani zinaeleza kwamba mbali na suala la bajeti ya Rais huyo kuja
nchini Tanzania kuwa kubwa pia kamati ya sheria ,ulinzi na usalama wa
Marekani imeshindwa kuthibitisha juu ya suala la ulinzi na Usalama wa
Rais Obama katika kipindi chote atakachokuwa nchini Tanzania pamoja na
baadhi ya nchi Barani Afrika.
Taarifa
hiyo pia ilieleza kwamba msafara wa Rais Obama unahitaji maandalizi ya
kutosha kwa sababu ni msafara unaohusisha watu wengi pamoja na vyombo
mbalimbali vya ulinzi ikiwemo wanyama.
Msemaji
wa Ikulu ya Marekani alisema kwamba serikali ilijaribu kuangalia
uwezekano wa Rais Obama kuja Tanzania na baadaye kutembelea Senegel
pamoja na Afrika Kusini ambapo alitakiwa kukaa Tanzania kwa saa mbili
tu lakini gharama za ulinzi imekuwa kubwa sana.
Katika
msafara wa Obama inatakiwa kuwe na ndege mbili za mwendo kasi, kwa
ajili ya kulinda ndege ya Rais,iwepo ndege za askari wa majini
zinazotembea kwenye meli habarini, iwepo pea maalum za magari zitakazo
sushwa katika nchi zote tatu mapema kwa kutumia ndege za jeshi kwa ajili
kuimarisha ulinzi kabla ya Rais kutua katika nchi hizo" alisema Mseaji
wa Ikulu ya marekani Josh Earnest.
Nakala
ya taarifa hiyo pia ilimkariri msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani
akisema kwamba pia katika msafari huo ni lazima iwe na vifaa maalum vya
kutolea matibabu katika kipindi chote cha ziara ya Rais, lazima pia
iwe na chombo maalum kwa ajili ya waandishi mbalimbali wa habari pamoja
na vyombo vingine vya usalama kwa ajili ya kutoa taarifa ya safari ya
Rais ,pamoja ndege zitakazokuwa zikizunguka kuangalia hali ya usalama
katika hoteli zote atakapo kuwa ana alala Rais Obama na msafara wake.
Taarifa
hiyo ilifafanua kwamba safari hiyo ndiyo safari kubwa kuliko aliyowahi
kuifanya Barani Afrika ambapo alifika nchini Ghana, tangu
alipochaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2009 ambapo inakadiriwa kuwa
itachukua kati ya dola za marekani 60 million sawa na tsh bilioni
96,000,000,000 na dola 100 milion sawa tsh bilioni 160,000,000,000.