Saturday, June 15, 2013
Friday, June 14, 2013
IJUE HISTORIA YA MAREHEMU LANGA KILEO 'LANGA'
Ili kuonyesha anachukizwa, Langa alilieleza jarida moja la burudani kwamba anakusudia kuanzisha Taasisi ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya.
Alisema matumizi ya dawa hizo yaliathiri shughuli zake za muziki na hakuwa na jambo lolote endelevu katika muziki wake.
Kimuziki Langa alianzia kundi la Wakilisha akiwa na Witness Mwaijega na Sarah Kaisi, ambapo walikuwa washiriki wa mashindano ya muziki ya Cocacola Pop stars, yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.
Wakiwa na kundi hilo walifanikiwa kufyatua kibao cha ‘Hoi’, ambacho kiliteka wapenzi wa muziki.
Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness walifyatua kibao cha ‘No Chorus’.
Baada ya hapo Langa alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’ ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha.
Hata hivyo Langa alionyesha yeye ni bora na ana kipaji cha muziki. Amekuwa shujaa kwa kuendesha kampeni kali za kupinga matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana. Serikali inapaswa kusaidia juhudi zake pamoja.Huyu ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha. Mbali ya Langa, wengine ni Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwaijaga `Witness’. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kung’ara kisanii kwa wakali hao, ingawa kwa sasa kundi hilo limesambaratika, kila mmoja akitamba kivyake.
HII NDIO MAKALA YA KWANZA YA LWAKATARE BAADA YA KUTOKA JELA '"MREJESHO KUTOKA MAHABUSU"
Sina budi kumshukuru
sana mwenyenzi Mungu kwa kunitendea mema na zaidi ya yote kunipa uhai na
afya hadi sasa. Wanasema “shukuruni katika yote” na mimi nalazimika
kushukuru kwa yale yote niliyofunuliwa na kuwa sehemu ya ushuhuda wangu
katika maisha niliyobakiza hapa duniani.
Namshukuru Mungu muweza wa yote kwa kunirejesha tena uraiani na kwa kuniunganisha na familia yangu,mke na watoto,wazazi ,ndugu,majirani na marafiki,viongozi wenzangu na wanachama wa chama kikubwa CHADEMA na zaidi ya yote watanzania walio wazalendo wanaoipenda na kuipigania nchi yao.
Ninapojikuta huru nje ya milango ya mninga uliowekewa makufuli makubwa,madirisha yenye nondo,ukuta uliowekewa waya wenye miiba mikali na ulinzi wa maaskari wanaonichunga saa 24,inanikumbusha wimbo mmoja wa mchakamchaka uliokuwa ukiimbwa gerezani kila siku saa 11:00 alfajiri tunapoamshwa uliokuwa na maneno;
“Kama raia!kama raia!kama raia!kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa baba na mama kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa ndugu na rafiki kama raia!
Kama raia…….”
Namshukuru Mungu muweza wa yote kwa kunirejesha tena uraiani na kwa kuniunganisha na familia yangu,mke na watoto,wazazi ,ndugu,majirani na marafiki,viongozi wenzangu na wanachama wa chama kikubwa CHADEMA na zaidi ya yote watanzania walio wazalendo wanaoipenda na kuipigania nchi yao.
Ninapojikuta huru nje ya milango ya mninga uliowekewa makufuli makubwa,madirisha yenye nondo,ukuta uliowekewa waya wenye miiba mikali na ulinzi wa maaskari wanaonichunga saa 24,inanikumbusha wimbo mmoja wa mchakamchaka uliokuwa ukiimbwa gerezani kila siku saa 11:00 alfajiri tunapoamshwa uliokuwa na maneno;
“Kama raia!kama raia!kama raia!kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa baba na mama kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa ndugu na rafiki kama raia!
Kama raia…….”
SIMBA, YANGA NA SUPER FALCONS KAZI KWAO, ZARUHUSIWA KWENDA DARFUL....!!!
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Siku
chache baada ya Serikali ya Tanzania kukataa kuziruhusu timu tatu za
Tanzania, Simba , Yanga na Super Falcons ya visiwani Zanzibar kushiriki
michuano ya kombe la Kagame, leo hii Serikali imeziruhusu klabu hizo
kwenda Sudan kushiriki michuano ya Klabu Buingwa Afrika Mashariki na
Kati, Kombe la Kagame.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiongea na
waandishi wa habari kanda ya kati Dodomo asubuhi ya leo amesema
wameruhusu klabu hizo ziende Sudan baada ya kuhakikishiwa na Serikali ya
nchi hiyo kwamba itatoa ulinzi wa kutosha dhidi ya timu za Tanzania.
Makalla
amesema wameandikiwa barua na Serikali ya Sudan ikiwahakikishia kwamba
timu za Tanzania zitapewa ulinzi mkubwa zisiathirike na machafuko
yanayoedelea Sudan.
BAADA YA KUPATA TUZO MBILI ZA KILI DIAMOND AMSUTA ‘MGANGA WAKE’
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
STAA
anayeng’aa katika Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
amemsuta mganga aliyejitokeza na kudai kwamba mwaka huu staa huyo
hatapata mafanikio yoyote na atapotea katika fani.
Mganga
huyo ambaye alidai utaalamu wake ndiyo uliompandisha chati Diamond
alisema mwaka huu staa huyo hatapata tuzo, atafifia na jina lake
litasahaulika kutokana na kukiuka masharti yake.
Akizungumza
na Ijumaa hivi karibuni, Diamond alisisitiza kutomtambua mganga huyo na
anamshangaa kwa kuwa mwaka huu amepata mafanikio tofauti na alivyosema.
“Hebu
angalieni, mganga alidai mwaka huu nitafutika katika fani, mbona
nimepata tuzo mbili kwenye Kil na nimechaguliwa kuwa balozi wa Cocacola
na shoo zinajaza kinoma?” alihoji Diamond.
Aidha,
alisema shoo zake bado zinajaza watu wengi huku akiitolea mfano ya
mwisho iliyofanyika Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar hivi karibuni
iliyojaza nyomi ya watu.
NA GPL
WANAFUNZI WA CHUO KIMOJA MKOANI MTWARA WAFANYA PARTY YA KIFUSKA
Pombe iko kichwani hapo....Kila kitu kwake ni sawa ..
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wanafunzi wa chuo kimoja maarufu Mkoani Mtwara hivi karibuni walifanya party ya ufuska na kuwaacha watu midomo wazi kwa mambo yaliyokuwa yanatendeka.
KINANA AMBURUZA KORTINI MBUNGE MSIGWA BAADA YA KUMWUITA JANGILI
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdul-rahman Kinana amemfungulia kesi
Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema), kutokana na kumtuhumu
anajihusisha na ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu.
Kinana
amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana
na kitendo cha Mbunge huyo kutoa tuhuma hizo dhidi yake kwa nyakati
tofauti nje na ndani ya Bunge, pia alikataa kuzikanusha na kumuomba
radhi.
Inadaiwa
kuwa Aprili 21 mwaka huu Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na
Utalii alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Shule ya Msingi Mbuguni wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Aidha
alizitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Kambi ya Upinzani katika
Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka
2013/2014. Katika hati ya madai, Kinana anadai kuwa kutokana na tuhuma
hizo ameharibiwa tabia yake, uaminifu, hadhi yake kitaaluma na weledi na
kumfanya achukiwe na kudharauliwa katika jamii.
Anadai
kuwa kabla ya tuhuma hizo alikuwa katika hatua za mwisho za mchakato wa
mazungumzo ya mradi wa ubia wa kilimo cha mboga na mwekezaji kutoka
kampuni ya nje, lakini tuhuma hizo zimesababisha kampuni hiyo kuvunja
majadiliano hayo.
Kinana
anadai kuwa sababu iliyotolewa na kampuni hiyo kuvunja mazungumzo hayo
ni kutajwa kwake na mbunge huyo kuwa ni jangili anayejishughulisha na
biashara hiyo.
TAARIFA KAMILI KUHUSU KIFO CHA LANGA NA RATIBA YA MAZISHI...!!
Wakati ambapo mashabiki wa muziki wa Hip Hop nchini wakianza kusahau majonzi ya kumpoteza Albert Mangweha aka Ngwair mwezi uliopita, leo wametoneshwa tena kwa kifo cha mwana hip hop mwingine, Langa Kileo aka Lyrically And Naturally Gifted African.
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa hospitali ya taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha aliyezungumza na Clouds FM, Langa amefariki leo June 13, saa 11 jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo tangia juzi mida ya jioni. Hata hivyo amesema kutokana na maadili na taratibu za hospitali asingeweza kutoa chanzo cha kifo cha Langa na jukumu hilo ni la ndugu zake.
Hata hivyo taarifa za awali zilidai kuwa Langa alikuwa anaumwa Malaria kali iliyopelekea kukimbizwa Muhimbili jana jioni.
Baba wa marehemu Mzee Kileo amesema taarifa kamili na mipango ya mazishi zitatolewa pale vikao vya familia vitakapofanywa.Pia baba yake alisema msiba huu umetokea wakati mama yake Langa hayupo Tanzania,alisema kwa sasa mama yake Langa yupo Marekani lakini baada ya kupewa taarifa hizo tayari ameshakata tiketi ya kurudi Tanzania na ataanza safari kesho.Msiba uko nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni(Anna Peter).
MAJINA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA 2013 NA KAMBI ZA JESHI WALIKOPANGIWA...TAREHE YA KURIPOTI NI 24 MWEZI HUU
TANGAZO
MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-
1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.
2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.
3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.
5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.
6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.
Zifuatazo ni selection za kambi walikopangiwa
Attached Files1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.
2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.
3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.
5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.
6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.
Zifuatazo ni selection za kambi walikopangiwa
- bulombora.pdf (806.9 KB )
- kanembwa.pdf (659.1 KB)
- maramba.pdf (334.6 KB)
- mgambo.pdf (791.9 KB)
- mlale.pdf (712.2 KB)
- msange.pdf (1.20 MB)
- ruvu.pdf (882.0 KB)
- rwamkoma.pdf (556.2 KB)
Thursday, June 13, 2013
KAULI YA BALOZI WA TANZANIA KUHUSU MSICHANA ANAYEDAIWA KUTAKA KUNYONGWA BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA EGYPT
Baada ya watu wengi kuzipata habari na bila kujua imekuaje kwa Mtanzania anaedaiwa kukamatwa na dawa za kulevya nchini Egypt na kwamba alikua anakaribia kunyongwa, balozi Mohamed Haji wa Tanzania nchini Egypt ameongea Exclusive na millardayo.com na kueleza yote anayoyafahamu kuhusu hii ishu. Namkariri akizungumza 1. Ni kweli kuna raia wawili Watanzania wamekamatwa na dawa za kulevya ambao ni Mbarak Abdallah Salim (28) na Sharifa Mahmud (27) wakazi wa Magomeni Kagera Dar es salaam, wanaundugu wa mtoto wa shangazi na mjomba. 2. Walikamatwa tarehe 16 May 2013 wakati wakiingia Misri, kwa mujibu wa maelezo safari yao ilianzia Dar es salaam kwenda Mombasa, Nairobi mpaka Misri. |
.
PICHA ZA KALA JEREMIAH AKIAMKABIDHI MAMA MZAZI WA MANGWAIR TUZO YAKE
MH: ZITO KESHO KUWA MGENI RASMI SHOW YA MWANA FA, HUKU SUGU AKIWA KWA JIDE
Ile the Big Square 1, show za magwiji wa
muziki Tanzania mwana FA ‘The Finest’ na Lady Jay Dee ‘Miaka 13 ya Lady
Jay Dee’ zitapigwa kesho June 14, huku presha ikiwa inaongezeka hasa kwa
fans wanaotamani kuhudhuria show walioichagua na kuona ukubwa wa show
kama walivyotarajia.
Show hizi kubwa zina nguvu sana kutokana
na ukubwa wa majina ya wasanii husika. Kwa mujibu wa lady Jay Dee timu
anaconda kesho itaungwa mkono na mheshimiwa Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
Jide ambae hivi karibuni ameachia wimbo
mpya unaopatikana kwenye album yake ‘Nothing but the truth’ inayoitwa
Yahaya, amepost kupitia kupitia ukurasa wake wa facebook na pia katika
akaunti yake ya Twitter kuonesha list ya wasanii watakaopanda jukwaani,
na pia uwepo wa Sugu.
” Miaka 13 ya Lady JayDee, Ijumaa ya kesho shughuli inaanza rasmi saa 3:00 usiku...Ukiskia paaaa ujue show imeisha
1. Prof Jay 2. Juma Nature 3. Grace Matata 4. Hamza Kalala 5. Wakazi na ugeni wa Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU
Nyimbo zote unazozipenda zitalia tar 14 June, pale Nyumbani Lounge sababu yaaaaa sababu yaaaaaa ?????????”
Kwa upande wa Mwana FA ambae atapiga show
yake na Live band akiwa na kundi kubwa na maarufu kwa upigaji wa Live
Band ‘Wananjenje’, yeye amepewa full sapoti na mbunge wa Kigoma
Kaskazini Zitto kabwe.
Zitto ameweka wazi kupitia akaunti yake ya twitter kuwa anamsapoti sana msanii huyo.
“You have my full support “@MwanaFA”
"BABY MADAHA ASITAKE KUPATA UMAARUFU KUPITIA JINA LANGU TENA ANIKOME" ...... JACK WOLPER
MWANADADA anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Jaqueline Massawe
‘Wolper Gambe’ amesema anamshangaa sana msanii wa muziki ambaye pia ni
mwigizaji Baby Madaha kutumia vyombo vya habari kutengeneza ugomvi
wakati hana mawasiliano naye yoyote na wala si rafiki yake au mtu
aliyekaribu naye na hana mazoea naye.
“Nimelizika na umaarufu nilio nao sihitaji
kujipeleka katika magazeti na kuongelea vitu ambavyo havina faida katika
jamii, mimi sina urafiki na Baby Madaha, namshanga anavyotapatapa
kuniandika vibaya kwa jambo lisilo nihusu, mambo hayo niliyafanya nikiwa
Chipukizi”
“Nakumbuka mimi nilipigiwa simu na rafiki yake
akiniomba namba mwenye nyumba lakini ghafla nikapiwa simu na mwandishi
wa habari mara Polisi nikashangaa huyo mtu hata namba ya mwenye nyumba
sijamtumia nasumbuliwa na watu utafikiri mimi ndio mtuhumiwa, lakini
jambo ninalomshangaa mimi ni dalali?,” alihoji Wolper.
Hivi karibuni yalizuka maneno yakiwahusisha wasanii hawa wawili
ikisemekana walikuwa wakigombea nyumba ya kupanga, huku Baby Madaha
kuigizwa mjini na mwenye nyumba kwa kupangishwa nyumba hewa, Wolper
amedai kuwa kwa sasa yeye amekuwa makini halipii nyumba kienyeji bali
ulipia kwa mwanasheria wake tena kwa kufuata taratibu kwa kukwepa
utapeli.
MUME WA MTU ANASWA GEST AKIWA NA SHOGA WAKIFANYA UCHAFU WAO
Tukio
hilo lililoshuhudiwa na watu kibao, lilijiri Juni 10, mwaka huu katika
nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Kunaswa
kwa wanaume hao ambao ilidaiwa walikuwa kwenye harakati za kufanya
Usodoma na Ugomora, kulifuatia mke wa mmoja wao kunasa meseji za
kimapenzi walizokuwa wakitumiana wawili hao.
Mama
huyo alipobaini meseji hizo chafu, wawili hao wakisisitiziana kukutana
kwenye gesti hiyo usiku wa siku hiyo, alimpigia simu mmoja wa waandishi
na kumpa mkasa mzima ambapo walikubaliana saa moja zoezi la
kuwanasa litaanza..
Ilipofika saa 1:30 usiku, timu yetu, mama huyo, wapambe wake na polisi walikuwa wanafanya doria nje ya gesti hiyo.
Saa
5:30 usiku, mume wa mwanamke huyo akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa
shoga walifika gesti hiyo bila kujua kama waliwekewa mtego wa kunaswa na
kwenda kuchukua chumba namba 2.
Wakiwa
ndani, mke alimpigia simu mumewe na kuhoji alipokuwa akajibiwa alikuwa
mitaa ya nyumbani kwao Manseze, Dar akipiga stori na rafiki zake.
Wawili
hao wakiwa wanajiandaa na mchezo wao usiofaa, polisi aligonga mlango
akijifanya mhudumu aliyetaka kumpatia taulo, jamaa bila kujua alifungua
ndipo walipofumaniwa na kuibua varangati zito.
Kufuatia
timbwili hilo, waliwekwa chini ya ulinzi na kutolewa pale gesti tayari
kupelekwa kituoni ndipo mwanaume anayedaiwa kuwa shoga akatimua mbio
mithili ya mwanariadha wa kimataifa, Usain Bolt wa Jamaika na wanandoa
hao waliendelea kuzozana huku mke akimlalamikia mumewe na kumwambia
wakifika nyumbani ampe talaka yake.
Hata
hivyo, mwanamke huyo aliomba sakata hilo lisipelekwe polisi kwa madai
alichotaka ni kumfumania mumewe na kwamba alikuwa na ushahidi wote.
GPL
Subscribe to:
Posts (Atom)