HUKU
mwili wake ukitarajiwa kuwasili Bongo kesho, kifo chake Albert
Mangweha ‘Ngwea’ kilichotokea katika hali ya utata Mei 28, 2013 nchini
Afrika Kusini, kimeibua mambo mapya, Ijumaa Wikienda lina mzigo wote.
MAMA MANGWEA NAYE AZIDIWA, AKIMBIZWA HOSPITALI YA MKOA
Habari kutoka msibani Moro jana zilisema mama mzazi wa marehemu Mangwea, Denisia Mangwea naye alizidiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa baadhi ya waombolezaji msibani hapo, mama huyo alipata mshtuko wa moyo kufuatia kifo cha mwanaye ambapo taarifa za kifo hicho zilimshtua tangu Jumanne mpaka alipozidiwa jana.

HABARI KUTOKA SAUZI SASA
Habari kutoka kwenye Jiji la Johannesburg ambako Ngwea alifia, mtiririko wa maelezo ya wenyeji wa Mangwea na Mgaza Pembe ‘M 2 The P’ nayo yanaibua mapya ambayo awali yalikuwa hayajulikani.
MAELEZO YA SAUTI ZA WENYEJI
Wakizungumza hewani kupitia redio moja ya jijini Dar, wenyeji wao wawili waliojitambulisha kwa jina moja moja la Godfrey na Godluck ambao walikuwa na Mangwea na M 2 The P, kila mmoja alisema lake huku maelezo yao yakionesha dalili ya kutofautiana au kuzua maswali masikioni mwa watu.