Tuesday, May 21, 2013
Monday, May 20, 2013
BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZ : MSIGWA APEWA DHAMANA
MBUNGE WA CHADEMA IRINGA MCHUNGAJI MSIGWA HATIMAYE AMEPEWA DHAMANA SASA HIVI NA WENGINE 60 WALIOLETA VURUGU KUBWA SANA JANA MJINI IRINGA NA KUHARIBU MALI NYINGI SANA ZA WANANCHI
LOVENESS DIVA AMKEJELI TENA MH. ZITTO KABWE.....!!!
Baada ya kutangaza kumpiga chini Mh.Zitto Kabwe, Loveness Diva ameamua kumchokonoa tena kwa kumkejeli kuhusu uamuzi wake wa kugombea Urais.....
Huu ni ujumbe wake aliouweka instagram:
".Ivi kwa akili yako unadhani unastahili kweli kuwa Rais mteule wa taifa hili....??
"Usiponijibu nikaridhika, basi ntakuchukulia kama mtu mwenye upeo finyu asiyejua alitendalo.."
MWENYEKITI WA CHADEMA AACHIA NGAZI......!!!
Lushoto. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Lushoto, mkoani Tanga, kimepata pigo baada ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kwekitui, Miraji Kassim kujiuzulu, kufuatia kile alichokielezea kuwa ni kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wenzie ngazi ya kijiji ambao wote ni wa CCM.
Mwenyekiti huyo ambaye alichaguliwa Aprili 27 mwaka huu katika uchaguzi mdogo, aliwashangaza wafuasi wake baada ya Kaimu Mtendaji wa kijiji hicho Athumani Kibiriti, kusoma baraua ya kujiuzulu kwake katika mkutano wa hadhara.
Mkutano huo uliitishwa na Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teklonojia, January Makamba.
YANGA: MRISHO NGASSA ATAMBULISHWA RASMI KUREJEA YANGA HII LEO
Katibu Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, Lawrence Mwalusako amemtambulisha rasmi Mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa kuwa mchezaji mpya kujiunga na timu hiyo msimu ujao wa Ligi na michuano ya kimataifa.
Mrisho Ngassa ambaye anarudi Yanga baada ya kuihama timu hiyo kwa kutimkia kwa Matajiri wa Bongo, Azam FC na baade mwaka jana kuzwa Simba kwa Mkopo baada ya kutokea sintofahamu za kimaadili ndani ya Klabu yake hiyo.
Ngassa alienda kuichezea Simba msimu uliopita baada ya Klabu yake ya Azam kuchukizwa na kitendo chake cha kuibusu jezi ya Yanga wakati timu hizo zikicheza.
Ngassa anakuwa ni mchezaji wa kwanza kuatangazwa na klabu hiyo kumsajili muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu na tayari ameshaanguka saini ya kuichezea klabu yake hiyo ambayo anamapenzi nayo makubwa hapa nchini kwa miaka 2.
MBUNGE MSIGWA AFIKISHWA MAHAKAMANI IRINGA MCHANA
Mbunge Msigwa akishuka katika gari ya polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana huu
Mbunge Msigwa akishuka katika gari hilo la polisi tayari kwa kuelekea chumba cha mahakama
Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani leo
Watuhumiwa wengine wa vurugu za machinga na polisi wakishuka katika karandinga la polisi
BUNGE LAAHIRISHWA BAADA YA KAULI NZITO TOKA UPINZANI
Bunge limeahirishwa baada ya kambi upinzani kudai kwamba serikali inatoa kucha, macho, meno na kuwaua waandishi wa habari. Hayo yalikuwepo ktk hotuba ya kambi ya upinzani iliyosomwa na msemaji wa wizara hiyo mheshimiwa Sugu. Kwa mujibu wa asasi ya kimataifa (jina limenitoka) inafuatilia haki na usalama wa waandishi wa habari, Tanzania iko ktk nchi kumi hatari kwa maisha ya waandishi wa habari ktk ripoti yake ya 2012.
Kama serikali haihusiki, kwa nini serikali isiunde tume ya kimahakama kama ilivyoombwa na chadema ili tujue ukweli? Ama waunde tume ya mahakama au wakubali tu kwamba wao ndo wanaohusika.
JK: MNAOTAKA URAIS 2015 ANZENI KUPITAPITA.
MWENYEKITI WA CCM DK JAKAYA KIKWETE.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amefungua milango kwa kuwataka baadhi ya watu ndani ya chama hicho wanaowania urais mwaka 2015 kuendelea na mchakato huo.
Rais Kikwete amewatahadharisha watu hao kuendesha kampeni zao kwa ustaarabu pasipo kuibua chuki wala kujenga makundi ambayo alisema ni hatari kwa kuwa yanaweza kukipasua chama.
Rais Kikwete aliyasema hayo katika mkutano ndani wa wabunge wa chama hicho uliofanyika jana katika ukumbi wa CCM (white house) mkoani hapa.
Mkutano huo ambao ulianza saa 3.00 asubuhi ulilenga kujadili masuala mbalimbali ya taifa ikiwamo utekelezaki wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho katika majimbo na ahadi mbalimbali za viongozi wa taifa.
Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya ukumbi huo kilieleza kuwa Rais Kikwete aliwataka wanachama wenye nia ya kugombea urais kuwa na tahadhari na watu aliowaita vishoka wa siasa.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Rais Kikwete alisema watu wa aina hiyo wana tabia ya kula huku na huku kwa kujiingiza katika kambi zaidi ya moja.
Polisi Wakamatwa na Bangi Gunia 18 Wakisafirisha na Gari ya Mkuu wa Polisi
Askari hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu saa nne usiku eneo la Kilemapofu, Wilaya ya Moshi Vijijini wakiwa na magunia 18 ya bangi ambayo walikuwa wameyapakia kwenye gari la Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2025.
Akithibitisha kukamatwa kwa askari hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema askari hao walikuwa wakipeleka bangi hiyo Wilaya ya Rombo kwa mfanyabiashra mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake.
Kamanda Boaz aliwataja askari waliokamatwa na wanashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi katika mji mdogo wa Himo kuwa ni F.1734 Koplo Edward (dereva) wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Arusha na G.2434 Konstebo George wa kituo cha polisi Ngarenanyuki Wilaya ya Arumeru.
Alibainisha kuwa kukamatwa kwa askari hao kunatokana na operesheni ya kukabiliana na dawa za kulevya inayofanywa na polisi katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
ANGALIA PICHA ZA DIAMOND, NAY WA MITEGO WAFANYA KUFURU DAR LIVE......!!!
Diamond Platnumz akiwapa hi mashabiki. |
MAWAZIRI WATATU WA JK KUNG'OLEWA.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dk Shukuru Kawambwa.
Dk. Mathayo David Mathayo, Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi.
Dk. Fenella Mukangara, Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
UPEPO mbaya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unazidi kuvuma, safari hii wabunge wake wakimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri watatu.
Mawaziri wanaotakiwa kung’olewa ni Dk. Shukuru Kawambwa (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Dk. Mathayo David Mathayo (Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Dk. Fenella Mukangara (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).
Kama Rais Kikwete atakubali kuwaondoa madarakani mawaziri hao, hii itakuwa mara ya pili kwake kufanya hivyo. Mara ya kwanza ilikuwa Mei mwaka jana.
Mwaka jana Rais Kikwete aliamua kuwaengua madarakani baadhi ya mawaziri waliokuwa wakiandamwa kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo uwajibikaji mbovu.
Miongoni mwa walioenguliwa mwaka jana ni Dk. Haji Mponda aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mustafa Mkulo (Waziri wa Fedha), William Ngel
eja (Nishati na Madini na Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii).
HUYU NDIE BINTI ALIYETOROKEA UINGEREZA AKIKWEPA KUTOMASWA NA MFALME MSWATI
Msichana mdogo ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza baada ya kukataa kwa dharau harakati za ndoa za wake wengi za Mfalme Mswati III wa Swaziland na kugoma kujiunga kwenye nyumba harimu ya wake 13.
Tintswalo Ngobeni, mwenye umri wa miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa hilo la kusini mwa Afrika akiwa na umri wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta hisia za mfalme huyo milionea, mtawala maarufu mkandamizaji kwa maisha yake ya anasa.
Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme Mswati III, mwenye umri wa miaka 45, anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila mwaka.
Tintswalo, ambaye sasa anaishi mjini Birmingham, alikuwa na umri wa miaka 15 tu wakati Mfalme huyo alipofanya harakati zake baada kumuona kwenye jumba la kifalme la mke wake wa nne, LaNgangaza. Binti huyo alisema 'alitishika' pale alipogundua dhamira zake za ndoa.
"Wake zake wamewekwa kwenye majumba yao, wakizingirwa na walinzi, na hakika hawawezi kwenda kokote isipokuwa tu mfalme akisema hivyo. Kitu pekee wanachofanya ni kwenda Marekani mara moja kwa mwaka, wakati mfalme huyo anapowapatia posho kwa ajili ya manunuzi."
Tintswalo alikuwa amelazimishwa kuachana na maisha ya starehe kwenye shule moja ya bweni huku shangazi yake, ambaye alikuwa mlezi wake mkuu, akisuka mipango ya kutorokea Uingereza kuungana na mama yake, ambaye alihamia mjini Birmingham miaka mitano kabla, akimtoroka mume wake mnyanyasaji.
"Sikuwa na jinsi," alisema. "Hakuna aliyewahi kumwangusha mfalme huyo au kuthubutu kumdharau, hivyo nikatoweka tu."
Sunday, May 19, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)