WABUNGE wa CCM, jana walizua tafrani nje ya Ukumbi wa Bungebaada ya kukasirishwa na kitendo cha mwenzao wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy kupinga Bajeti ya Wizara ya Ujenzi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.
Katika mchango wake, Keisy alisema haungi mkono hoja kwa sababu Barabara ya Sumbawanga hadi Kanazi-Mpanda mpaka Kibaoni haijajengwa kwa kiwango cha lami.
Alisema zilitengwa Sh27 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo lakini mpaka sasa Wachina waliopewa zabuni ya ujenzi huo wamekosa fedha na wameamua kuuza kokoto.
Alisema zilitengwa Sh27 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo lakini mpaka sasa Wachina waliopewa zabuni ya ujenzi huo wamekosa fedha na wameamua kuuza kokoto.
Mara baada ya Bunge kuahirishwa, Keisy akiwa nje ya ukumbi huo alifuatwa na Mbunge wa Urambo Mashariki, Profesa Juma Kapuya, Omary Nundu (Tanga Mjini), Mendrady Kigola (Mufindi Kusini) na Rita Kabati (Viti Maalumu) na kumzonga.
Baada ya wabunge hao kumzonga, Profesa Kapuya ambaye amewahi kuwa waziri serikalini alihoji kitendo cha mbunge huyo kupinga bajeti... “Kwa nini umekataa kuunga mkono hoja? Ulikuwa unalidanganya Bunge wakati unachangia si kweli huko Rukwa hakuna barabara, barabara mnazo.”