Friday, May 03, 2013
BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZ!!!! : MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 KUSAHISHWA UPYA,
MCHUMBA WA MTU ATUPWA JELA KWA KUJIUZA...........!!!
Na Richard Bukos
MREMBO
Brandina Barthon (24), Jumatatu iliyopita alihukumiwa kwenda jela miezi
6 baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi ya ukahaba iliyokuwa
ikimkabili katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar.
Brandina
alisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William
Mutaki ambaye alisema kutokana na ushahidi uliothibitika, mahakama hiyo
inamhukumu kwenda jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa wengine.
Hukumu
hiyo ilimfanya mrembo huyo kuchanganyikiwa na kuangua kilio lakini
mheshimiwa hakimu aliamua kukazia hukumu yake bila ya kupepesa
macho.
Wakati
mwanamke huyo akiangua kilio, afande wa Jeshi la Magereza alimfikia na
kumchukua kwa ajili ya kumpeleka kwenye Karandinga kuelekea Gereza la
Segerea kuanza maisha ya jela.
Mbali
na Brandina, mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa mtuhumiwa huyo
aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga machozi baada ya kutolewa
hukumu hiyo.
HII NDIO LIST KAMILI YA VIONGOZI WA TANZANIA NA WA KIMATAIFA WALIOJIUNGA FREEMASONS
Siri ya List za Viongozi wa Tanzania Yatajwa (Secret Society), Freemason, imedaiwa kuwa na siri nzito na viongozi wakuu wa nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MWINYI NA ANDY CHANDE
| |
Andy ChandeKikubwa kinachodaiwa ni kuwa Chande anatumiwa na Freemason kuhakikisha kwamba kila kiongozi wa nchi hii anakuwa karibu na jamii hiyo ya siri.
Inazidi kudaiwa kuwa Freemason inafanya njama za hali ya juu kujiweka karibu na Ikulu, ikiwa na mpango wao wa muda mrefu wa kusimika rais ambaye ni memba wa jamii hiyo katika awamu zinazokuja.
Uchunguzi umeonesha kuwa Chande amekuwa karibu na Ikulu tangu Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na amedumu kujiweka karibu na viongozi wa nchi mpaka awamu hii ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
NEEMA YAWASHUKIA WALIOFELI .... MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KUPANGWA UPYA
TUME ya kuchunguza sababu za kufeli kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya mitihani ya kuhitimu mwaka 2012 imekamilisha kazi yake na taarifa za uhakika zilizolifia gazeti hili zinasema , upangaji alama zao utafanyika upya.
Kama ambavyo gazeti hili lilivyobaini katika uchunguzi wake wa kiuandishi kwamba kulifanyika mabadiliko ya utoaji alama kwa ajili ya mitihani waliyofanya wanafunzi mwaka huo (2012) bila maandalizi kwa wadau, tume hiyo imependekeza alama zipitiwe upya (regrading).Katika alama za awali, alama D anapoyopewa mtahiniwa baada ya mtihani wake kusahihishwa ilikuwa ni kuanzia alama 21 kwenda mbele na F ilikuwa 20 kushuka chini lakini katika mabadiliko yaliyoleta ‘maafa’ ya kufeli kwa watahiniwa wa mwaka jana, alama D ilianzia 35 na kuendelea, wakati ile ya kufeli (F) ilianzia alama 34 kushuka chini.
Thursday, May 02, 2013
HUSANA IDD NA NAOMI WA BONGO MOVIE WAGOMBEA PENZI LA JANUARY...!!
Msanii
anayechipukia kwenye soko la filamu na muziki, Naomi Mbaga ameibuka na
kumuonya Husna Idd ‘Sajent’ amuachie bwana wake, January.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Naomi aliweka bayana kuwa January ambaye ni
Mwanamuziki wa Bendi ya Victoria ni mpenzi wake wa muda mrefu hivyo
alishangazwa kuona habari mitandaoni kuwa Sajent amejituliza kwa mpenzi
wake huyo baada ya kumwagana na mzazi mwenzake, Charles Gabriel ‘Chaz
Baba’.
“Aniachie bwana wangu, kama ameachika kwa huyo Chaz Baba atafute bwana mwingine na siyo wa kwangu. Ole wake nimkute naye siku, atanitambua,” alisema Naomi.
“Aniachie bwana wangu, kama ameachika kwa huyo Chaz Baba atafute bwana mwingine na siyo wa kwangu. Ole wake nimkute naye siku, atanitambua,” alisema Naomi.
Sendeka, Shelukindo wamtetea Kinana
Tuhuma
dhidi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana,
(pichani) kuhusika katika usafirishaji wa pembe za ndovu,
zimewalazimisha wabunge kadhaa wa CCM kumsafisha.
Hali hiyo ilijitokeza juzi jioni wakati wakichangia hotuba hiyo ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Tuhuma hizo zilitolewa na Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Mchungaji Peter Msingwa (Chadema), kuituhumu kampuni ya Sharaf Shipping Agency inayomilikiwa na Kinana kukamatwa na pembe za ndovu nchini China.
Mbunge wa Simanjaro , Christopher Ole Sendeka (CCM), alimtetea Kinana kuwa kampuni yake haihusiki katika sakata la pembe za ndovu.
Hali hiyo ilijitokeza juzi jioni wakati wakichangia hotuba hiyo ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Tuhuma hizo zilitolewa na Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Mchungaji Peter Msingwa (Chadema), kuituhumu kampuni ya Sharaf Shipping Agency inayomilikiwa na Kinana kukamatwa na pembe za ndovu nchini China.
Mbunge wa Simanjaro , Christopher Ole Sendeka (CCM), alimtetea Kinana kuwa kampuni yake haihusiki katika sakata la pembe za ndovu.
Chadema yachelea kujitoa mchakato wa Katiba
Sina
mpango wa kujitoa kwenye Tume kwa kuwa nimekula kiapo kwa ajili ya
Watanzania, hadi sasa sijaona sababu ya kutaka kujitoa, alisema Profesa
Baregu.
Dar es Salaam. Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshindwa kutoa kauli kuhusu
kujitoa kwake kwenye mchakato wa Katiba Mpya baada ya muda kilioutoa kwa
Serikali kutaka kurekebishwa kwa baadhi ya mambo katika mchakato huo
kumalizika juzi.
Mwenyekiti
wa Chadema na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe
alisema bungeni Aprili 11, mwaka huu kuwa chama chake kitajitoa katika
mchakato huo endapo mambo muhimu mawili hayatapatiwa ufumbuzi hadi
kufikia Aprili 30, mwaka huu.
Mambo
hayo ni kufutwa kwa uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya wilaya ya katiba
uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata (WDC), badala yake
wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa kata husika bila kuchujwa na
kamati hizo.
YULE MHINDI ALIYEDAIWA KUMUUA MWALIMU WA SHULE YA MSINGI NAYE AJIUA.......!!!
MHINDI
mwenye uraia wa India, Srinivasa Rao Talluri, 36 anayedaiwa kumuua
Mwalimu Elizabeth Mmbaga wa Shule ya Msingi Atlas, jijini Dar es Salaam
amejiua Aprili 17 mwaka huu katika Hoteli ya Transit iliyopo Karakata.
Talluri
ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya vinywaji vikali
ijulikanayo kwa jina la Moan’s Drinks Ltd iliyopo Oysterbay, Dar maiti
yake ilikutwa chumbani saa mbili asubuhi na inadaiwa alijiua kwa kunywa
sumu ambayo mabaki yake yamepelekwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali
kwa uchunguzi.
Habari za kipolisi zimesema kuwa baada ya wafanyakazi wa Hoteli ya Transit jijini Dar kugundua kuwa Mhindi huyo amekufa, walitoa taarifa polisi ambao walifika na walipochunguza chumbani, walikuta kuna pombe aina ya Pushkin chupa tatu, chupa yenye sumu ya kuulia wadudu, chips na maziwa glasi moja.
Habari za kipolisi zimesema kuwa baada ya wafanyakazi wa Hoteli ya Transit jijini Dar kugundua kuwa Mhindi huyo amekufa, walitoa taarifa polisi ambao walifika na walipochunguza chumbani, walikuta kuna pombe aina ya Pushkin chupa tatu, chupa yenye sumu ya kuulia wadudu, chips na maziwa glasi moja.
Marehemu Elizabeth Mmbaga enzi za uhai wake.
Inadaiwa
kwamba Mhindi huyo aliachishwa kazi katika kampuni hiyo Aprili 2,
mwaka huu baada ya kugundulika kuwa alitumia vibaya zaidi ya shilingi
400,000 ambapo Aprili 3, mwaka huu alifikishwa polisi Kituo cha
Oysterbay, jijini Dar.
Mwandishi wetu alifika katika ofisi za Moan’s Drinks Ltd alikokuwa akifanyia kazi Mhindi huyo na kuonana na mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Raju na akakiri kutokea kwa kifo cha Talluri.
Habari zinasema mwili wake ulifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jumatatu iliyopita na ukasafirishwa kupelekwa India Jumatano ya wiki iliyopita kwa ajili ya mazishi.
Mwandishi wetu alifika katika ofisi za Moan’s Drinks Ltd alikokuwa akifanyia kazi Mhindi huyo na kuonana na mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Raju na akakiri kutokea kwa kifo cha Talluri.
Habari zinasema mwili wake ulifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jumatatu iliyopita na ukasafirishwa kupelekwa India Jumatano ya wiki iliyopita kwa ajili ya mazishi.
Kitanda walichokuwa wakilala wapenzi hao.
Mhindi
huyo anadaiwa kuwa alikuwa mpenzi wa Mwalimu Elizabeth ambaye siku
moja kabla ya kifo chake imeelezwa kuwa alikuwa naye kwenye baa moja
karibu na nyumba ya Eliza, hata hivyo, alikutwa amekufa katika chumba
chake Kimara Baruti, Dar Aprili 15 mwaka huu huku shingoni kukiwa na
michubuko iliyoashiria kuwa alinyongwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Marietha Minangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho katika hoteli hiyo.
“Ni kweli alikutwa amekufa katika Hoteli ya Transit na chumbani tulikuta sumu ambayo tumepeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Marietha Minangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho katika hoteli hiyo.
“Ni kweli alikutwa amekufa katika Hoteli ya Transit na chumbani tulikuta sumu ambayo tumepeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi,” alisema.
CCM WAMVAA MKUU WA MKOA WA ARUSHA.....WANADAI AMEMUONGEZEA UMAARUFU GODBLESS LEMA...!!
VIGOGO
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo wabunge, wamemjia juu Mkuu wa
Mkoa (RC) wa Arusha, Magessa Mulongo kwa jinsi alivyoshughulikia kesi ya
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Wabunge
hao waliliambia gazeti hili mjini Dodoma kuwa kesi ya uchochezi
iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Lema kwa shinikizo la mkuu huyo,
itaiathiri kwa kiasi kikubwa CCM.
Mbunge
wa Mwibara, Kangi Lugola alisema kuwa amefuatilia kwa makini chanzo
cha kesi ya Lema na hatimaye kukamatwa na polisi mithili ya gaidi, na
kubaini kuwa hulka
za utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa serikali zinawapa sifa na umaarufu zaidi CHADEMA.
“Mimi
sitaki kuingilia kesi, lakini ukiangalia kuanzia ile inayoitwa video
ya vurugu za Chuo cha Uhasibu Arusha na jinsi Mkuu wa Mkoa alivyofika
eneo la tukio na kuondoka, utabaini udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo
ambao leo unamfanya Lema aonekane shujaa.
“Leo
tunaingia kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani pale Arusha, tunaweza
tukashinda, lakini tutafanya kazi ya ziada kwa sababu tu ya udhaifu wa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,” alisema Lugola.
LIL WAYNE AZIDIWA TENA, AKIMBIZWA HOSPITALI.
According
to TMZ, rapper Lil Wayne was rushed to Cedars-Sinai Hospital in L.A on
Tuesday night after suffering another seizure. He was treated and
released yesterday morning.
Wayne
then did a radio interview yesterday afternoon and explained he's an
epileptic, and has been suffering from seizures since he was a kid.
MWAKA MMOJA KABURINI... KANUMBA THE GREAT FILM INAPUMULIA MASHINE
Mojawapo ya ofisi za Kampuni ya Kanumba The Great Films illiyopo Sinza Mori.
MIPANGO
endelevu inapaswa kufuatwa na kila mwanadamu, katika familia zetu za
Kiafrika mara nyingi tunaanguka katika suala la mipango mikakati ya muda
mrefu. Mwanadamu akifariki, mara nyingi wanaoachwa kuendeleza kazi za
marehemu wanaishia kusuasua na kutofikia malengo.
Yapata
mwaka mmoja tangu, aliyekuwa legend wa simema za Kibongo, Steven
Kanumba ‘The Great’ afariki dunia na kuiacha Kampuni yake ya Kanumba The
Great Film ikiendeleza shughuli zake za kuzalisha filamu kama kawaida.
Kampuni
aliyoiacha pale Sinza-Mori, jijini Dar ilibaki chini ya mikono ya
wafanyakazi wake wakiongozwa na mdogo wa marehemu, Seth Bosco, mpiga
picha za video, Zakayo Magulu pamoja na Mayasa Mrisho ‘Maya’ ambaye
alikuwa akifanya kazi kama msimamizi wa ‘location’ (location manager) na
masuala ya makeup.
Kadiri
siku zilivyozidi kusonga, umoja kati yao ulianza kupungua. Kila mmoja
anaonekana kuhangaika kivyake licha ya kwamba kampuni bado ipo. Mikakati
ya jumla ikawa haijadiliwi, kila mmoja akawa anaangalia namna ya
kujikwamua kivyake.
Mara
kadhaa nimekuwa nikizungumza na baadhi ya wasanii waliokuwa tegemezi
katika kampuni hiyo, wamekuwa wakiniambia wapo bize kufanya kazi zao
binafsi nje ya Kanumba The Great Film. Hiyo inaonesha dalili kwamba kazi
za umoja zimeanza kulegalega.
Marehemu Steven Kanumba akiwa na tuzo za filamu enzi za uhai wake.
Mh. Rais Ang'atwa na Chui............!!!
Rais wa Botswana, Ian Khama ameshonwa baada ya kung'atwa na Duma, kwa mujibu wa maafisa wakuu nchini humo.
Mnyama huyo alikuwa analishwa alikokuwa anahifadhiwa katika kambi ya kijeshi wakati alipomrukia rais Khama na kumgwara
Tukio
hilo ilikuwa ajali tu wala sio shambulio kali, kwa mujibu wa msemaji wa
serikali Jeff Ramsay aliyezungumza na waandishi wa habari.
Majeraha ya Bwana Khama, yalikuwa madogo wala haikujitokeza kama ajali kubwa.
Inaarifiwa ajali ilitokea ghafla na kumgutukia Rais Khama na walinzi wake.
"Duma alimgwara tu lakini sio kumshambulia, kama wanavyodahani watu wengi,'' alisema bwana Ramsay.
Bwana Khama alionekana akiwa amevalia plaster kwenye mkutano ulioandaliwa baada ya tukio hilo.
Duma, ambao ndio wanyama wenye kasi kubwa zaidi ardhini, ni moja ya wanyama wanaokabiliwa na tisho kubwa la kuangamia.
Ni wanyama 12,400 pekee wanaosemekana kusalia mbugani katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Botswana.
WASTARA AKATAA KUWA MKE WA PILI
MSANII
wa filamu za Kibongo, Wastara Juma hivi karibuni alikataa kuolewa na
kuwa mke wa pili baada ya kupigiwa simu na mwanamke mmoja jijini Dar
akimtaka awe mke mwenzake.
Wastara
ambaye hivi sasa yuko Uarabuni kwa ajili ya mapumziko baada ya kufiwa
na mumewe, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Januari mwaka huu, alikataa
ofa hiyo na kusema kwamba kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini, mwanamke huyo aliamua kufanya hivyo
baada ya kushauriana na mumewe kuhusu Wastara kuingia katika familia
yao.
“Mwenyewe
alisema alishauriana na mumewe na haoni tatizo Wastara kuwa mke
mwenzake kwa sababu imani ya dini yao inaruhusu,” kilieleza chanzo
hicho.
Subscribe to:
Posts (Atom)