Wednesday, May 01, 2013
Taarifa mbalimbali za michezo kutoka TFF ikiwemo ligi kuu ya Vodacom kuingia raundi ya 25 hapo kesho.
Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura.
LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA 25
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea
katika raundi yake ya 25 kesho (Mei Mosi) kwa mechi tano zitakazochezwa
katika miji ya Dar es Salaam, Turiani, Morogoro na Mlandizi.
Licha ya kuwa tayari Yanga imetawazwa
kuwa mabingwa wa VPL msimu huu (2012/2013), mechi dhidi ya Coastal Union
itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni moja kati ya
zitakazovuta macho na masikio ya washabiki wa mpira wa miguu nchini.
Mechi hiyo namba 172 itachezeshwa na
mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na Said Mnonga na Charles
Chambea wote wa Mtwara wakati mwamuzi wa mezani atakiwa Hashim Abdallah
wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni David Lugenge kutoka Iringa.
Viingilio katik mechi hiyo itakayoanza
saa 10.15 jioni ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh.
8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati
VIP A itakuwa sh. 20,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mchezo.
Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa African
Lyon katika mechi namba 170 itakayochezeshwa na mwamuzi Dominic
Nyamisana wa Dodoma kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani
Morogoro. Nayo Kagera Sugar iliyo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo
wa ligi hiyo itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro.
Kambi ya Upinzani Bungeni imetoa tuhuma nzito kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Kambi
ya Upinzani Bungeni imetoa tuhuma nzito kwa Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana ikidai kuwa anajihusisha na mtandao wa ujangili
nchini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi amejibu tuhuma hiyo akisema ni za uongo huku akiituhumu kambi hiyo kuwa imedanganya wakati inajua ukweli kuhusu tuhuma dhidi ya Kinana.
Akiwasilisha maoni ya upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/14, Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Maliasili, Mchungaji Peter Msigwa alisema vitendo vya ujangili vimekuwa vikilitia doa taifa kwenye jumuiya za kimataifa.
“Kwa bahati mbaya ni kwamba wahusika wengi ambao wanatajwa kwa ushahidi ni makada maarufu na wengine ni viongozi waandamizi wa CCM,” alisema Mchungaji Msigwa.
“Tumeshuhudia watuhumiwa wengine wa ujangili ambao Ikulu imediriki kuwapatia nafasi kubwa za uongozi wa taifa hili, licha ya kutajwa kwenye ripoti ya uchunguzi kuhusiana na ujangili.”
Alisema mwaka 2009, meli ya Kampuni ya Wakala wa Meli ya Sharaf Shipping inayomilikiwa na Kinana ilikamatwa China ikiwa na makontena yenye nyara za Serikali ikiyasafirisha kwenda Hong Kong.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi amejibu tuhuma hiyo akisema ni za uongo huku akiituhumu kambi hiyo kuwa imedanganya wakati inajua ukweli kuhusu tuhuma dhidi ya Kinana.
Akiwasilisha maoni ya upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/14, Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Maliasili, Mchungaji Peter Msigwa alisema vitendo vya ujangili vimekuwa vikilitia doa taifa kwenye jumuiya za kimataifa.
“Kwa bahati mbaya ni kwamba wahusika wengi ambao wanatajwa kwa ushahidi ni makada maarufu na wengine ni viongozi waandamizi wa CCM,” alisema Mchungaji Msigwa.
“Tumeshuhudia watuhumiwa wengine wa ujangili ambao Ikulu imediriki kuwapatia nafasi kubwa za uongozi wa taifa hili, licha ya kutajwa kwenye ripoti ya uchunguzi kuhusiana na ujangili.”
Alisema mwaka 2009, meli ya Kampuni ya Wakala wa Meli ya Sharaf Shipping inayomilikiwa na Kinana ilikamatwa China ikiwa na makontena yenye nyara za Serikali ikiyasafirisha kwenda Hong Kong.
RAIS KIKWETE AUNGA MKONO HOJA YA MBATIA KUHUSU MITAA YA ELIMU.
Rais Kikwete.
Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia.
RAIS
Jakaya Kikwete amekubaliana na hoja ya Mbunge wa Kuteuliwa, James
Mbatia kuhusu kufanyiwa marekebisho kwa mitalaa ya elimu nchini ili
iendane na viwango vya elimu inayohitajika.
Rais
Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wenyeviti na
wamiliki wa shule na vyuo vya binafsi kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa,
Mbeya.
Katika
kikao cha Tano cha Bunge, Januari mwaka huu, Mbatia aliwasilisha hoja
binafsi kuhusu ubovu wa elimu na mitalaa, hoja aliyodai kufinyangwa na
Bunge kabla ya kupatiwa majibu stahiki na hata kuzua mjadala mkali
miongoni mwa wadau wa sekta hiyo.
RAIS OBAMA AMPONGEZA MWANAUME SHOGA ALIYEJITANGAZA HADHARANI

Mchezaji
wa mpira wa kikapu nchini Marekani mwenye asili ya Afrika Jason Collins
amejitangaza kuwa yeye ni shoga hatua ambayo imewashitua watu wengi
hususani wapenzi wa mchezo huo.
Jason
Collins anakua mchezaji wa kwanza wa kimataifa mwanaume ambaye bado
anacheza mpira wa kikapu kutangaza kuwa ni shoga huku akisema kuwa yeye
ni mwanamme mweusi na ni shoga.
Rais
wa Marekani Barack Obama amempongeza mwanababa huyo shoga mwenye umri
wa miaka 34 anayecheza katika ligi ya NBA kwa kujitangaza hadharani.
Rais
Obama ambaye mwaka jana alitangaza kuunga mkono ndoa za mashoga
alimpigia simu Collins na kumpongeza kwa ujasiri alioonyesha na amesema
atamuunga mkono.
Mchezaji
wa zamani wa NBA John Amaechi mwaka 2007 alijitokeza hadharani na
kutangaza kuwa ni shoga lakini yeye alifanya hivyo akiwa tayari
amestaafu kucheza kikapu.
Naye
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton alimpigia simu Collins na
kusema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa wanamichezo wa kimataifa na ni
historia kwa jumuiya ya mashoga na wasagaji.
Binti
wa Bill Clinton, Chelseea ambaye amesema kuwa alimfahamu Collins wakati
wakiwa wanachuo katika chu kikuu cha Stanford na meandika katika
ukurasa wake wa tweeter kwamba anaona fahari kubwa kwa rafiki yake
Collins kwa kuwa na ujasiri wa kuwa mchezaji pekee wa NBA shoga na
kuweka hadharani hali yake.
Tuesday, April 30, 2013
YALIOJILI KWENYE BIRTHDAY KICK YA MTU MZIMA CHIDY BENZ@NEW MAISHA CLUB
Chidy akimlisha keki joketi
Hapa akimlisha keki moja kati ya mafuns wake katika siku yake zakuzaliwa
Totozzilikuwa zaukweli na zakumwaga
Makiss na ma hug yalihusika sana siku hiyooooo
Hii hapa keki ya king kong chidy beeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeenz
BABA MZAZI WA CHRIS BROWN, AMEZUNGUMZA KUHUSU MAPENZI YA CHRIS NA RIHANNA
Gazeti la New York Daily News limefanya Exclusive
interview na baba mzazi wa mwimbaji staa Chris Brown na kutoa maoni
yake kuhusu mahusiano ya kimapenzi ya mwanae na Rihanna RiRi. Clinton Brown amesema “sioni maisha marefu kwa Chris Brown kuwa na Rihanna, sijawahi kupendezwa na kurudiana kwao, unajua ni lazima kwenye uhusiano wa kimapenzi uwe na mtu sahihi ambae ni hitaji la kweli na linaloweza kuwa lako kwenye maisha, lakini sio kama hivi” Clinton amesema hapendi kutumia mifano lakini anadhani watu wameona mahusiano ya mastaa kama Whitney Houston, Michael Jackson, Amy Winehouse na wengine” Kuhusu mrembo ambae angependa kuona anaolewa na mwanae, Clinton amemtaja Jordin Sparks kwa kusema “nimempenda Jordin, ni msichana mdogo lakini mwenye upeo mkubwa… ana akili na heshima” |
DOTNATA AFUNGUKA BAADA YA KUGUNDUA KAWEKEWA SUMU KWENYE JUICE

Amesema alianza kuhisi kupandwa na pressure ambapo alilazwa
kwenye hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufikia 284 huku
wakimweleza huenda ni kwakuwa amenenepa sana.Baadaye alifanyiwa
uchunguzi wa moyo kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa
vipimo zaidi.
Anasema
tatizo hilo lilimsabisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi
alikuwa akitapika.
“Nimezidiwa usiku wa kuamkia
Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa ikabidi wanichunguze kwa makini
kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua nimelishwa sumu takriban mwezi wa
nane sasa huyo mtu aliyenipa sumu aliipitisha kwa njia ya juice,”
amesema Dotnata ambaye kwa sasa ameokoka.
Akizungumzia
sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:
“Kila
mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda
hakupendezewa na mimi niendelea kuishi hivi, labda alifikiria akiniua
mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili
niyasimulie mema ya Mungu. Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako
kumbe ndio mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu.”
Msikilize
zaidi hapa.
NA BONGO CLAN BLOG
NA BONGO CLAN BLOG
Wabunge waliosimamishwa warejea kwa ari Bungeni
Dodoma. Baada ya kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya
Bunge, wabunge watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
jana waliingia bungeni wakionekana kuwa na ari mpya.
Wabunge waliosimamishwa Aprili 17 ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya
Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Wengine ni Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje (Nyamagana),
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini) na Godbless Lema (Arusha Mjini).
Jana
asubuhi Mchungaji Msigwa alikuwa miongoni mwa wabunge waliowahi kuingia
mapema ndani ya Ukumbi wa Bunge na kufuatiwa na Lissu muda mfupi baada
ya kikao kuanza.
Ndani ya Ukumbi wa Bunge, Msigwa
alipata nafasi ya kuuliza swali namba 115 lililokuwa liulizwe na Joyce
Mukya kuhusu Kampuni ya Kamwene Woodworks . Kwa upande wake, Lissu
aliomba mwongozo wa Spika kuhusu kukwama kwa Bajeti ya Wizara ya Maji.
Wabunge wengine haikujulikana sababu za kutofika jana licha ya
kuwa adhabu yao ilikwisha tangu April 25 huku taarifa zikieleza kuwa
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alikuwa apelekwe mahakamani kujibu
staka la uchochezi.
Mwananchi
Mitambo ya analojia Mbeya kuzimwa leo saa 6:00 usiku.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema mitambo ya Analojia mkoani
Mbeya itazimwa rasmi leo saa 6:00 usiku.
Innocent Mungi, alisema Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza na waandishi habari jana, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, alisema Mkoa wa Mbeya umekuwa wa mwisho katika hatua za kuzima mitambo hiyo, katika awamu ya kwanza.
Akizungumza na waandishi habari jana, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, alisema Mkoa wa Mbeya umekuwa wa mwisho katika hatua za kuzima mitambo hiyo, katika awamu ya kwanza.
Mungi alisema uzimaji wa mitambo ya analojia na kuhamia katika mitambo ya Digitali katika awamu ya kwanza, ulihusisha Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Tanga, Mwanza, Moshi na Arusha.
Alisema wakazi wa Mbeya walikwishafahamishwa kuhusu kuzimwa kwa mitambo hiyo kwa kufanya maandalizi yaliayohitajika ili kuepuka usumbufu ambao ungejitokeza.
Aliwataka Watanzania kuacha kunung’unika wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali na hasa yanayohusu matatizo ya ving’amuzi na badala yake, wachukue za kutafuta ufumbuzi
Alisema baadhi ya Watanzania wamekuwa wakitumia muda mrefu kunung’unika na kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Shambulio lafanyika mjini Rome wakati serikali mpya ikiapishwa.
Serikali
mpya nchini Italia imeapishwa na kumaliza hali ya iliyodumu kwa miezi
kadhaa ya wasiwasi wa kisiasa, kufuatia uchaguzi mkuu wa mwezi Februari
mwaka huu, ambao ulishindwa kutoa mshindi wa moja kwa moja.
Hata
hivyo hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao ilifunikwa na tukio la
ufyatuaji risasi nje ya ofisi ya waziri mkuu ambapo maafisa wawili wa
polisi walishambuliwa.
Watu
walioshuhudia tukio hilo wamesema walimuona mwanaume mwenye silaha
akifyatua risasi nje ya ofisi ya waziri mkuu katikati ya mji wa Rome,
wakati baraza jipya la mawaziri likiendelea kuapishwa, umbali wa
kilomita moja kutoka hapo, katika ikulu ya rais.
HAWA NDIO WATUMIAJI 11 WA MADAWA YA KULEVYA WENYE AKILI ZAID DUNIANI NA OBAMA YUMO.........!!!
STEVE JOBS
Imeripotiwa
kwamba mwanzilishi wa Apple alitumia madawa kweny muhula wa kwanza kule
Reed College in Portland, Oregon mwaka 1972. Tangu aach shule, Jobs
amekuwa moja ya watu wenye mafanikio zaidi nchini America na dunia nzima
kwa ujumla. Mwaka 1984,medali ya Taifa ya Technology nchini Marekani
kutoka kwa rais wa kipindi hicho Ronald Reagan. Mwaka 2007, Fortune
Magazine walimtaja kama mtu mwenye nguvu zaidi kwenye biashara na kisha
mwaka 2011 gavana wa California Arnold Schwarzeneggerallimuweka kwenye
California Hall of Fame.pia walimtaja kama CEO wa muongo (CEO of the
decade) mwaka 2009 huku Forbeswakimuweka #57 kwenye list ya “World’s
Most Powerful People” mwaka huo huo.
Sir Richard Branson
Huku ile
‘Sir’ikimuweka kwenye list ya watu wanaoheshimiwa zaidi, hiyo sio sababu
ya yeye kuwa kwenye hii list. Kinachomfanywa awekwe ni kwa sababu yeye
anashika namba 236 kwenye watu matajiri zaidi duniani, mwanzilishi wa
Virgin empire, ambayo inashughulika na vitu vingi kuanzia ndege mpaka
maduka ya rekodi tofauti, simu,na ametengeneza utajiri wake from
scratch.Sio tu kwamba a, he gets high with his 21-year-old son.
alishasema mbele ya umati kwamba haoni tatizo kuhusu kutumia
marijuana,na amefanya mchakato kuhalalisha utumiaji wake,na pia amesema
kama ikiruhusiwa, atauza.
DADA WA NDIKUMANA APALILIA NDOA YA KAKA YAKE
Uwoya akiwa na mumewe Ndikumana enzi hizo.
Dada wa mchezaji
wa Timu ya Rayon Sport, Ndikumana Katauti, Fatuma amefunguka kuwa licha
ya migongano ya ndoa ya kaka yake lakini bado wanapendana.
Akizungumza
na gazeti moja la nchini Rwanda, Fatuma alisema kwamba hata ilivyotoka
habari kuwa wifi yake Irene Uwoya amenaswa na Diamond alishtuka sana
kwani yeye bado anaamini ndoa ya kaka yake ina uhai wa asilimia mia
moja.
“Nilishangaa sana kuona
gazeti limeandika kuwa wifi yangu amenaswa na Diamond, mimi naamini
ndoa ya kaka yangu bado ipo hai,” alisema Fatuma.
Subscribe to:
Posts (Atom)