Serikali
mpya nchini Italia imeapishwa na kumaliza hali ya iliyodumu kwa miezi
kadhaa ya wasiwasi wa kisiasa, kufuatia uchaguzi mkuu wa mwezi Februari
mwaka huu, ambao ulishindwa kutoa mshindi wa moja kwa moja.
Hata
hivyo hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao ilifunikwa na tukio la
ufyatuaji risasi nje ya ofisi ya waziri mkuu ambapo maafisa wawili wa
polisi walishambuliwa.
Watu
walioshuhudia tukio hilo wamesema walimuona mwanaume mwenye silaha
akifyatua risasi nje ya ofisi ya waziri mkuu katikati ya mji wa Rome,
wakati baraza jipya la mawaziri likiendelea kuapishwa, umbali wa
kilomita moja kutoka hapo, katika ikulu ya rais.