Kishindo
cha kuondoka kwako kwenye uso wa dunia tunayoishi kinaweza kuwa kikubwa
ama kidogo au hakuna kabisa kutokana na mazingira au heshima
uliyojijengea katika jamii.

Fatma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi Kidude aliaga dunia wiki iliyopita akiwa na zaidi ya miaka 100. Bado jina lake linatamkwa kwenye vinywa vya wengi na linaweza kuendelea kutamkwa kwa miaka mingi zaidi.
Bi
Kidude, mwanamke shujaa mzaliwa wa Visiwani Zanzibar alileta mapinduzi
katika muziki asilia wa mwambao. Aliitangaza Zanzibar, Tanzania na Bara
la Afrika sehemu mbalimbali duniani alipokwenda kwa ziara za kimuziki.
Inaaminika alifanya kazi hiyo ya muziki, mafunzo ya unyago na biashara
ya hina na wanja kwa zaidi ya miaka 90.
Katika
kipindi chote, Bi Kidude hakushuka kimuziki hadi pale mdomo ulipoanza
kuwa mzito kutokana na uzee miaka 10 kabla ya kifo chake Aprili 17,
mwaka huu baada ya kuugua maradhi ya kisukari na kongosho kwa muda
mrefu.
Pia inaaminika kuwa ndiye msanii mkongwe zaidi aliyekuwa akipanda jukwaani na umri mkubwa ukilinganisha na wengine unaowajua.