Siku
mbili kabla ya bunge la Ufaransa kuidhinisha sheria inayohalalisha ndoa
za jinsia moja kumetokea maandamano ya dakika za mwisho mwisho mjini
Paris.
Watu
wanaopinga sheria hiyo wamekusanyika katika eneo la Montparnasse la mji
mkuu katika juhudi za mwisho za kuizuia sheria hiyo, huku maandamano
mengine ya kundi hasimu pia yaliandaliwa kuiunga mkono sheria hiyo.
Zaidi ya watu 100 wamekamatwa katika kipindi cha wiki moja iliyopita katika maandamano mengine ya kupinga ndoa za jinsia moja.
Makundi
ya kutetea haki za binadamu pia yameripoti ongezeko la matusi na
mashambulizi ya kimwili dhidi ya jamii ya mashoga na wasagaji nchini
Ufaransa.
Ufaransa
inatarajiwa kuwa nchi ya 14 kuhalalisha ndoa za jinsia moja, kufuatia
kuidhinishwa sheria hiyo nchini New Zealand wiki iliyopita.