Wabunge watano wa Chadema
jana walitimuliwa bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa siku tano
kutokana na vurugu zilizotokea jana usiku.Wabunge hao ni Lissu,
Hezekiah Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi
(Mbeya Mjini) Godbless Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa
(Iringa Mjini).
Chanzo za kufukuzwa kwao ni
kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa
kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya
Mbunge wa Iramba Mashariki,
Mwigulu Nchemba.
Kutokana na tafrani hiyo,
Nchemba hakuweza kuhitimisha hotuba yake hivyo Ndugai alilazimika
kukatisha mkutano wa Bunge.Hata hivyo wakati akiahirisha mkutano huo,
tayari wabunge hao walikuwa wameshatolewa nje baada ya askari
kuongezwa.
Mapema Mbunge wa Kigoma
Mjini (CCM), Peter Serukamba alitoa tusi zito la nguoni wakati wa
hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, licha ya Spika wa Bunge, Anne Makinda
kupiga mkwara wa kuwashughulikia wabunge watakaorusha matusi.