......................................................................
Na
Esther Macha, Mbeya
LICHA ya
Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya
vyandarua hali hiyo bado imekuwa tatizo kutokana jamii zilizo nyingi
Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuwa na imani potofu kuhusu matumizi
ya vyandarua vyenye dawa kuwa hawapati usingizi na wengine kudai ni
njia ya uzazi wa mpango.
Hayo
yalisemwa jana Bwana afya katika Ofisi ya Wilaya ya Mbarali Bw.Yona
Msyani wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili, kuhusiana na elimu
ya ugonjwa wa maralia katika viwanja vya hospitali ya Chimala Mission
.
Alisema
kuwa suala la utumiaji wa vyandarua imekuwa changamoto kubwa kwa
katuiika utendaji kazi kwa wataalamu wa afya kutokana na wananchi
kuwa na imani potofu juu ya matumizi ya vyandarua vyenye dawa.
“Bado
tuna changamoto kubwa sana hivyo inatupasa kujipanga na kuelimisha
jamii kutambua umuhimu wa matumizi ya vyandarua “alisema.
Hata
hivyo alisema kuwa imani hiyo potofu si kwa Wilaya ya mbarali tu kwani
hali hiyo ilijitokeza wakati wa kampani ya ugawaji wa vyandarua hivyo
mwaka 2010 kwa nchi nzima.
Bw.
Msyani alisema kuwa kama wataalamu wa afya bado wanaendelea kutoa
elimu ya afya kwa wananchi jinsi ya kujizuia na ugonjwa wa maralia
ikiwa ni pamoja na kuondokana na dhana potofu waliyojenga wananchi.
Akizungumzia
kuhusu vifo ambavyo vinatokana na ugonjwa maralia ,Bwana afya huyo
alisema kuwa maralia I ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo hasa kwa
watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
“Tatizo
hili lipo kwa kiasi kikubwa kwa watoto , mwaka 2012 mwezi januari
mpaka desemba waliugua watoto 1,635 chini ya umri wa miaka mitano
ambapo kati ya hao waliofariki ni 100 kwa mwaka jana kutokana na
ugonjwa wa maralia.