Tuesday, April 09, 2013

Uhuru Kenyatta kuapishwa rasmi leo kuwa Rais wa Kenya.

Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta, anaapishwa rasmi leo huku marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakitazamia kuwa miongoni mwa wageni mashuhuri kwenye sherehe hizo.



Uhuru na mgombea mwenza wake, William Ruto, walichaguliwa katika uchaguzi wa Machi 4 mwaka jana kwa zaidi ya kura milioni 6.13 na hivyo kumshinda mpinzani wake Rail Odinga, aliyepata kura milioni 5.3 .


Uchaguzi huo ulifuatiwa ule wa Desemba mwaka wa 2007 uliomalizika kwa ghasia za kikabila na kusababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha na wengine kupoteza makazi.
Kuhusu sherehe, maofisa wa Serikali ya Kenya, walisema zinatazamiwa kuhudhuriwa na viongozi kadhaa barani Afrika na kwamba baadhi yao walianza kuwasili nchini humo tangu jana.
Viongozi hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete ambaye ameambatana na maofisa kadhaa wa Serikali yake.Wengine ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Omar al-Bashir wa Sudan.


Hata hivyo, kumekuwa na sintofahamu kuhusu kuhudhuria kwa kiongozi huyo wa Sudan anayetakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inayomtuhumu kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu katika Jimbo la Darfur.

Ziara ya Jay Z na Beyonce nchini Cuba yazua utata kwa baadhi ya wanasiasa nchini Marekani.


Wanasiasa wawili wa bunge la Kongres la Chama cha Republican nchini Marekani wamehoji iwapo ziara ya wanamuziki maarufu wa nchi hiyo mume na mke Jay Z na Beyonce nchini Cuba ilikuwa na kibali cha serikali.
Mastaa hao wamepigwa picha kadhaa wakiwa mjini Havana wakisalimiana na mashabiki wao, wakitoka kupata msosi na kutembelea sehemu kadhaa za mji huo wakati wakisherehekea miaka mitano ya ndoa yao.

Hata hivyo vikwazo vya kibiashara vya Marekani vinazuia wamerekani kuitembelea Cuba kwa sababu za kiutalii pekee na anayetaka kusafiri lazima aombe kibali maalum.
Wanasiasa hao Ileana Ros-Lehtinen na Mario Diaz-Balart wametuma barua kwa Idara ya hazina ya Marekani wakiulizia ni aina gani ya kibali walichopewa wanamuziki hao kuitembelea nchi hiyo.

Wamesema vikwazo vya kuitembelea nchi hiyo viliwekwa kwa sababu marekani iliiorodhesha serikali ya Cuba kama taifa linalounga mkono ugaidi na kudai kuwa nchi hiyo ni moja kati ya nchi zenye rekodi mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa kawaida sababu za muhimu zinazoweza kumruhusi raia wa Marekani kwenda Cuba ni pamoja na matibabu, kusoma, sababu za kidini, huduma za kijamii na sababi nyingine za kibinadamu.

Mshindi wa Tshs 10,000,000 za DStv apatikana.


Masoud Said (38), mkazi wa Mbeya akifurahia kitita cha Tshs 10,000,000 alizozawadiwa na DStv kwenye campaign ya DStv Rewards. Kila wiki, DStv wamekuwa wakitoa Tshs 5,000,000 kwenye droo maalum kwa wateja wake wanaofanya malipo kabla ya akaunti zao kukatika. Kushoto ni Meneja wa Fedha wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Francis Senguji na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Furaha Samalu.
Mshindi wa Tshs 10,000,000 za DStv  Masoud Said akiwa ameshikilia mabulungutu ya fedha zake.

Mwigulu akiri kuhusika video ya Lwakatare

POLISI WADAIWA KUMFANYIA UNYAMA KADA WA CHADEMA
HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba, amekiri kuhusika na video inayomwonesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.
Nchemba amekuwa akitajwa na viongozi wa CHADEMA kuwa anahusika kutengeneza video hiyo, kwa kuwa aliwahi kutamba wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni kuwa anayo video inayowaonesha viongozi wa chama hicho wakipanga mauaji.
Hata hivyo, tangu Nchemba atoe kauli hiyo Januari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilikaa kimya hadi Machi 12 lilipomkamata na kumhoji Lwakatare, siku moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa You tube na mtu anayejiita ‘Bukoba Boy’.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 09.04.2013

.
.
.

MFANYABIASHARA WA KIHINDI AUAWA NA KUPORWA MIL 100, SALENDER BRIDGE

Majambazi yamempiga risasi mfanyabiashara wa Kihindi na kumuua papo hapo na kumpora shilingi milioni 100 eneo la Salender Bridge, Upanga Dar es Salaam jana jioni .
Kwa mujibu wa walioshuhudia sakata hilo, wanasema mtoto wa kike wa marehemu pia alipigwa risasi ya paja, lakini akafanikiwa kuendesha gari lao huku akiwa na mwili wa marehemu babake hadi Hospitali ya Regency.
Hivi sasa msichana huyo shupavu, anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo...
Habari zaidi tutaendelea kuwaletea kadri tutakavyokuwa tunazipata..

Monday, April 08, 2013

UWOYA, DIAMOND WANASWA HOTELINI!

Diamond na Uwoya, walifanya jitihada za hali ya juu kuuficha ukweli kuhusu uhusiano wao lakini ilipofika Machi 25, mwaka huu, walinaswa na kamera za Global kwenye hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda, linathubutu kwa kuwa lina ushahidi wa kutosha kutamka kwamba Diamond na Uwoya, walilala kwenye hoteli hiyo, chumba namba 208, waliingia saa 8:24 usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.

Tigo yawekeza kuunganisha watu wa vijijini na kuboresha huduma zake.


Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mh. Charles Bishuli akihutubia wananchi wa wilaya ya Kasulu kwenye sherehe za uzinduzi wa minara. Kulia kwake  Meneja wa Kanda ya ziwa Bw Joseph Mutalemwa na  Meneja wa Tigo wa mkoa wa Kigoma Bw Gamu Kimoro.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mh. Charles Bishuli akitaka utepe kuzindua mnara ya TIGO katika kata ya Muyama wilayani Buhigwe. Kulia kwake Meneja wa kanda ya ziwa Bw. Joseph Mutalemwa.

Waziri Mkuu wa Kwanza mwanamke nchini Uingereza Baroness Thatcher afariki dunia.


Waziri mkuu wa zamani nchini Uingereza Bibi Margret Thatcher amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.
Thatcher aliyekuwa mwanake wa kwanza kushika wadhfa huo, alikuwa alitokea chama cha Conservative na kuongoza nchi hiyo tangu mwaka 1979 hadi 1990.
Waziri Mkuu wa sasa nchini humo Bw. David Cameron ameelezea masikitiko yake na kumuita mwana mama huyo kuwa mjasiri wa Uingereza.
Naye Malkia Elizabeth wa II wa nchi hiyo hakusita kueleza kushitushwa na habari za kifo hicho huku akisema kimemhuzunisha lakini heshima ya kiongozi huyo itabaki palepale.
Kwa mujibu wa taarifa kiongozi huyo hatazikwa kwa mazishi ya kitaifa lakini atazikwa kwa hadhi sawa na Princes Diana nay a Mama wa Malkia.
Waziri Mkuu wa Uingereza Bw.  Cameron ambaye yuko ziarani nchini Hispania kwa ajili ya mikutano, amelazimika kukatisha ratiba ya mazungumzo yake na rais wa Ufaransa Francois Hollande na kurejea nyumbani.
Lady Thatcher kama alivyokuwa akijulikana alizaliwa akiitwa Margaret Roberts na kuhudumu kama mbunge wa Finchley –London Kaskazini tangu mwaka 1959 hadi 1992.

ANGALIA TUKIO LA WACHAWI WAWILI WALIODONDOKA NA UNGO HUKO KAHAMA- SHINYANGA...

WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI (70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI (80)

Watu wawili wamenusurika kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Mhongolo wilaya ya kahama mkoani shinyanga, baada ya kukutwa katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya kishirikina. 

Watu hao waliojitambulisha kwa majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na Shija Nkwabi(80) wa Nyashimbi wilayani humo, wameanguka kijijini hapo wakitokea kijiji cha nduku wiyani humo wakielekea Nyihogo Kahama kwa shughuli za kishirikina.

Katika maelezo yao wazee hao wamedai  kuwa wameanguka baada ya kutokea ajali ya kishirikina huko angani, ambapo waligongana na wenzao ambao hawakuwafahamu walikotoka na walikokuwa wanaelekea.

Chadema kuwasha moto bungeni, ni kuhusu wanachodai 'utendaji usiofaa' wa Bunge.

Wakati Bunge la 11 la Bajeti kwa mwaka huu likianza kesho, Kamati Kuu ya Chadema imesema itatumia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulibana Bunge kuhusu utendaji usiofuata Kanuni za Bunge unaofanywa na Spika na wasaidizi wake.
 
Pia wabunge hao wameitaka Serikali kuweka wazi mikataba iliyoingia hivi karibuni na Serikali ya China ili wananchi waweze kufahamu kilichomo vinginevyo watatumia kambi hiyo kuwabana wahusika.


Katika kikao cha 10 kilichomalizika Februari 8, mwaka huu mjini Dodoma, Mnadhimu wa kambi hiyo, Tundu Lissu alisema kuwa wanaandaa hoja za kumng’oa Spika na Naibu wake, Job Ndugai kwa kile walichodai kukiuka kanuni mbalimbali za Bunge.

Kambi ya upinzani ilikuwa ikilalamika kuondolewa kwa hoja binafsi za baadhi ya wabunge wao ikiwemo ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Maji), James Mbatia (Mitalaa ya Elimu) na Joshua Nassari, ambaye hoja yake ilihusu utendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati akiahirisha kikao cha 10, alisema kuwa hoja binafsi zitakuja tena katika kikao cha 11 na wenye hoja watazifufua.

Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema Kamati Kuu ilibaini kwamba matukio yaliyotokea katika kikao 10 yalitokana na meza ya spika kutofuata kanuni.

MKAPA AWATAKA VIONGOZI WAFUATE MISINGI YA NYERERE

Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.
Akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa
madhehebu yote.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 9 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
 
.
.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...