Tuesday, April 09, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 09.04.2013

.
.
.

MFANYABIASHARA WA KIHINDI AUAWA NA KUPORWA MIL 100, SALENDER BRIDGE

Majambazi yamempiga risasi mfanyabiashara wa Kihindi na kumuua papo hapo na kumpora shilingi milioni 100 eneo la Salender Bridge, Upanga Dar es Salaam jana jioni .
Kwa mujibu wa walioshuhudia sakata hilo, wanasema mtoto wa kike wa marehemu pia alipigwa risasi ya paja, lakini akafanikiwa kuendesha gari lao huku akiwa na mwili wa marehemu babake hadi Hospitali ya Regency.
Hivi sasa msichana huyo shupavu, anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo...
Habari zaidi tutaendelea kuwaletea kadri tutakavyokuwa tunazipata..

Monday, April 08, 2013

UWOYA, DIAMOND WANASWA HOTELINI!

Diamond na Uwoya, walifanya jitihada za hali ya juu kuuficha ukweli kuhusu uhusiano wao lakini ilipofika Machi 25, mwaka huu, walinaswa na kamera za Global kwenye hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda, linathubutu kwa kuwa lina ushahidi wa kutosha kutamka kwamba Diamond na Uwoya, walilala kwenye hoteli hiyo, chumba namba 208, waliingia saa 8:24 usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.

Tigo yawekeza kuunganisha watu wa vijijini na kuboresha huduma zake.


Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mh. Charles Bishuli akihutubia wananchi wa wilaya ya Kasulu kwenye sherehe za uzinduzi wa minara. Kulia kwake  Meneja wa Kanda ya ziwa Bw Joseph Mutalemwa na  Meneja wa Tigo wa mkoa wa Kigoma Bw Gamu Kimoro.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mh. Charles Bishuli akitaka utepe kuzindua mnara ya TIGO katika kata ya Muyama wilayani Buhigwe. Kulia kwake Meneja wa kanda ya ziwa Bw. Joseph Mutalemwa.

Waziri Mkuu wa Kwanza mwanamke nchini Uingereza Baroness Thatcher afariki dunia.


Waziri mkuu wa zamani nchini Uingereza Bibi Margret Thatcher amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.
Thatcher aliyekuwa mwanake wa kwanza kushika wadhfa huo, alikuwa alitokea chama cha Conservative na kuongoza nchi hiyo tangu mwaka 1979 hadi 1990.
Waziri Mkuu wa sasa nchini humo Bw. David Cameron ameelezea masikitiko yake na kumuita mwana mama huyo kuwa mjasiri wa Uingereza.
Naye Malkia Elizabeth wa II wa nchi hiyo hakusita kueleza kushitushwa na habari za kifo hicho huku akisema kimemhuzunisha lakini heshima ya kiongozi huyo itabaki palepale.
Kwa mujibu wa taarifa kiongozi huyo hatazikwa kwa mazishi ya kitaifa lakini atazikwa kwa hadhi sawa na Princes Diana nay a Mama wa Malkia.
Waziri Mkuu wa Uingereza Bw.  Cameron ambaye yuko ziarani nchini Hispania kwa ajili ya mikutano, amelazimika kukatisha ratiba ya mazungumzo yake na rais wa Ufaransa Francois Hollande na kurejea nyumbani.
Lady Thatcher kama alivyokuwa akijulikana alizaliwa akiitwa Margaret Roberts na kuhudumu kama mbunge wa Finchley –London Kaskazini tangu mwaka 1959 hadi 1992.

ANGALIA TUKIO LA WACHAWI WAWILI WALIODONDOKA NA UNGO HUKO KAHAMA- SHINYANGA...

WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI (70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI (80)

Watu wawili wamenusurika kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Mhongolo wilaya ya kahama mkoani shinyanga, baada ya kukutwa katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya kishirikina. 

Watu hao waliojitambulisha kwa majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na Shija Nkwabi(80) wa Nyashimbi wilayani humo, wameanguka kijijini hapo wakitokea kijiji cha nduku wiyani humo wakielekea Nyihogo Kahama kwa shughuli za kishirikina.

Katika maelezo yao wazee hao wamedai  kuwa wameanguka baada ya kutokea ajali ya kishirikina huko angani, ambapo waligongana na wenzao ambao hawakuwafahamu walikotoka na walikokuwa wanaelekea.

Chadema kuwasha moto bungeni, ni kuhusu wanachodai 'utendaji usiofaa' wa Bunge.

Wakati Bunge la 11 la Bajeti kwa mwaka huu likianza kesho, Kamati Kuu ya Chadema imesema itatumia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulibana Bunge kuhusu utendaji usiofuata Kanuni za Bunge unaofanywa na Spika na wasaidizi wake.
 
Pia wabunge hao wameitaka Serikali kuweka wazi mikataba iliyoingia hivi karibuni na Serikali ya China ili wananchi waweze kufahamu kilichomo vinginevyo watatumia kambi hiyo kuwabana wahusika.


Katika kikao cha 10 kilichomalizika Februari 8, mwaka huu mjini Dodoma, Mnadhimu wa kambi hiyo, Tundu Lissu alisema kuwa wanaandaa hoja za kumng’oa Spika na Naibu wake, Job Ndugai kwa kile walichodai kukiuka kanuni mbalimbali za Bunge.

Kambi ya upinzani ilikuwa ikilalamika kuondolewa kwa hoja binafsi za baadhi ya wabunge wao ikiwemo ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Maji), James Mbatia (Mitalaa ya Elimu) na Joshua Nassari, ambaye hoja yake ilihusu utendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati akiahirisha kikao cha 10, alisema kuwa hoja binafsi zitakuja tena katika kikao cha 11 na wenye hoja watazifufua.

Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema Kamati Kuu ilibaini kwamba matukio yaliyotokea katika kikao 10 yalitokana na meza ya spika kutofuata kanuni.

MKAPA AWATAKA VIONGOZI WAFUATE MISINGI YA NYERERE

Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.
Akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa
madhehebu yote.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 9 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
 
.
.
.
.

Sunday, April 07, 2013

LULU AONGOZA WASANII NA WENZIE KUTEMBELEA KABURI LA KANUMBA NA KUKUTANA NA MAMA KANUMBA.


Lulu akiwa na mama yake mzazi leo walipo tembelea kaburi la marehemu Steven Kanumba ikiwa ni mwaka mmoja toka amefariki
Wakimuombea Marehemu Steven Kanumba

BARUA YA ZITTO KABWE INAYOMTAKA "LWAKATARE ATIMULIWE CHADEMA" YAZUA BALAA

ANGALIA PICHA ZA BONGO MOVIES WAKIPATA LUNCH NYUMBANI KWA WEMA SEPETU

CEO wa kampuni ya Endless Fame Pro' Wema Sepetu
Leo amewaalika wasanii wenzake wa Bongo Movie
Nyumbani kwake Kijitonyama
kujumuika nae kwa pamoja kwenye Chakula cha mchana.....


Hatman & Irene Uwoya

HII NDIO PARTY YA KUMKARIBISHA MSANII WA BONGO MOVIE KAJALA BAADA YA KUNUSURIKA KWENDA JELA


 wema, kajala n friend wakishow love..
best friends forever inshaallah mwenyez mungu awaweke
hapa wakiingia ukumbini.

ANGALIA PICHA ZA NDOA YA MZEE PHILIP MANGULA NA MWALIMU YOLANDA KABEREGE, JANA





Akifungisha Ndoa Hiyo Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe Isaya Mengele Amekumbusha Maneno ya Mungu na Kuwataka Wanandoa Kuishi Kwa Misingi ya Dini Kama Ilivyoelekezwa Kwenye Vitabu Vya Dini.




 Kulia ni mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akiwa na waziri mkuu Mizengo pinda katikati akifuatiwa na Katibu mkuu wa CCM.




 Kushoto ni msemaji wa familia ya mzee Philip Mangula Dr.Lechion Kimilike ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu huria cha Tanzania Tawi la Njombe[NJOMBE OPEN UNIVERSITY].

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA APRIL 7 TANZANIA.

.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...