Mhe. Abubakar Khamis Bakar, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu jinsia moja.
Waziri
wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Bwana Abubakar Khamis Bakar,
aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati
akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka
Chama cha Wananchi (CUF).
Katika
swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya
Zanzibar itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali
kwa watu ambao watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu.
Waziri
Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na utamaduni
Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha miaka saba
kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.
Pia
alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi yakiwemo
ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu ya
kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa
kunukuu.