Friday, April 05, 2013
KAJALA APEWA SHAVU JINGINE NA WEMA...........!!!!
Muigizaji
na Miss Tanzania wa zamani Wema Sepetu amesema licha ya kumsainisha
Kajala Masanja kwenye kampuni yake, hategemei kumfanyisha kazi kurudisha
shilingi milioni 13 alizomtolea kwenye hukumu yake.
Akiongea
kwenye kipindi cha XXL, Wema amesema Kajala atakuwa akifanya kazi zake
lakini atakuwa akimlipa kama kawaida. Kwa kuanza Kajala ataigiza kama
mhusika mkuu kwenye filamu iitwayo Princess Sasha.
“Tutaenda
kuishoot nje ya Dar, ninataka kuishoot mandhari fulani hivi kama ya
kijijini. Ni mtoto wa mfalme, Kajala ndo atakuwa Princess Sasha, she is
going to be the main character, “ alisema Wema.
DAWA MPYA ZA KIENYEJI ZA KUKUZA MAKALIO ZAWATEKA WAREMBO WENGI
BAADA
ya zile dawa za Kichina za kuongeza makalio, ‘hips’ na matiti
zilizotikisa Bongo na kubainika kubeba madhara makubwa kama vile ‘kalio’
moja kuwa kubwa kuliko lingine, kujazia zaidi chini kuliko juu na mwili
kufa ganzi, zilikosa soko, lakini sasa zimeibuka nyingine za kienyeji
Uchunguzi
uliofanywa na audifacejackson blog kupitia kwa wataalam mbalimbali wa
tiba za asili TANZANIA , ulibaini kuwa dawa hizo zimejaa tele kwa
waganga wa kienyeji.
JOKATE KUKITANGAZA KIMATAIFA KIKUNDI CHA WANAHABARI
Aliyewahi
kuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006 Jokate Mwegelo alijitolea
kuwafungulia website kikundi hicho ili kiweze kujitangaza na kutambulika
ndani na nje ya nchi.
Jokate
alisema kuwa ili kikundi hicho kifanikiwe ni lazima wajitambue na kuwe
na timu imara ambayo itakuwa makini na nia thabiti ya kujiinua kimaisha
na kukuza uchumi wa Taifa.
"Mafanikio
niliyokuwa nayo si kwasababu mimi ni bilionea bali ni kutokana na
ushirikiano tuliokuwa nao mimi na wenzangu hadi tukafanikiwa kuwa na
kampuni inayojulikana kama kidoti". Alisema Jokate.
Aliongeza
kuwa japo kuwa wanakabiliana na changamoto mbalimbali lakini
wanaendelea vizuri na biashara ambapo mbali na kuuza nywele tunatarajia
kuuza vipodozi pamoja na nguo
Mbali
na hilo alisema kuwa ili wafanikiwe ni lazima wawe na upendo ili kila
mtu aweze kuwa huru na kueleza kile anachokiona kina manufaa katika
kikundi.
Tigo yadhamini Ngorongoro Marathoni
Kampuni
ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo imedhamini Mbio za Sita za
Ngorongoro Marathon zenye lengo la kupambana na ugonjwa wa malaria
zinazotarajiwa ‘kutimua vumbi’jumamosi ya Aprili 6, mwaka huu katika
mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha. Ufunguzi wa mbio hizo utafanywa na
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.
Meneja
Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga alisema kuwa, kwa mwaka huu kampuni
hiyo imetoa fedha taslimu, simu za kisasa kabisa za mkonaoni pamoja na
muda wa hewani kwa mshindi wa kwanza wa kundi la wanaume na mshindi wa
kwanza kwa kundi la wanawake.
“Tigo
kwa kuwajali Watanzania, tumeona umuhimu mkubwa sana wa kuunga mkono
juhudi zinazofanywa na serikali katika mapambapo dhidi ya malaria ambayo
imekuwa ikipoteza maisha ya watu wengi wa rika mbalimbali kupitia mbio
hizi…” alifafnua Mpinga. Kwa
upande wake Mratibu wa ZARA Charity ambao ndio waandaji wa mbio hizo
Bw, Datus Joseph alifafanua kuwa, pamoja na kusaidia mapambano dhidi ya
malaria, mbio za Ngorongoro Marathon pia zinasaidia kukuza utalii wa
ndani na nje ya nchi.
“Mbio
hizi ni za Sita tangu kuanzishwa kwake na Tigo wameendeea kutupa
‘support’ na tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa wadhamini wetu…”
alifafanua Joseph. Aliendelea kufafanua kuwa, ZARA Charity inawashukuru wadhamini mbalimbali wa mbio hizo ambazo zimekuwa za mafaniko makubwa.
Thursday, April 04, 2013
PICHA ZA RAMANI YA UJENZI WA UWANJA WA YANGA, HIVI NDIVYO UTAVYOKUA
Ramani ya uwanja mpya wa klabu ya Yanga - Kaunda Stadium unavyoekana kwa ndani
Kampuni ya Beinjing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi akinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani.
Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG Zhang Chengwei David amesema upembuzi akinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja wa mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga.
MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE YATOA UFAFANUZI KUHUSU UWANJA WA SONGWE KUITWA JAKAYA KIKWETE
MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI BW. SULEIMAN SULEIMAN AKIZUNGUMZIA UGUMU WA KUBADILISHA JINA LA SONGWE KUITWA JAKAYA KIKWETE |
CHEK PICHA ZA NDOA YA COMEDIAN KUPA ILIYOFANYIKA WEEKEND ILIYOPITA
Weekend iliyopita comedian maarufu “Kupa” alifunga ndoa na mke wake
ambapo sherehe yao ilihudhuriwa na wasanii wenzake kibao kutoka
bongomovie unit. Cheki mpango mzima ulivyokuwa siku ya siku na wasanii
walivyopendeza kwenye party hiyo. Short list ya wasanii waliofika kwenye
party hiyo ambayo MC alikuwa Dr Cheni ni Ray,JB,Nisha,Irene
Uwoya,Wolper na wengine wengi.
WEMA SEPETU AMSUPRISE MARTIN KADINDA KWA BOOOOOOONGE LA KEKI NA MSHIKO WA MAANA
ahahahhha a this woman is something Else.. baada ya kukurukakala zangu Wema sepetu aliniita nyumbani kwake.... as soon as i got there nitwishwa boooooonge la keki... You i was like whaaat? |
hakuishia hapo.... mkononi kashika nini hapo?? usisonye sasa... hahha |
SHILOLE, Q-CHILLAH WAFUMWA LAIVU WAKIWA KATIKA MAHABA
Aibu
hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo
wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya
shoo siku ya Pasaka. Akilisimulia gazeti hili, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo (jina tunalo) alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘malovee’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa. |
Airtel, Samsung wakubaliana kukuza soka la vijana: Airtel Rising Stars Awamu ya tatu kuanza mwishoni mwa mwezi huu
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel inayofanya kazi pamoja na kampuni ya
Samsung zimesaini makubaliano ya kushirikiana kudhamini mashindano
makubwa Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
Katika
mkataba huo wa mamilioni ya dola, Samsung pia itakuwa mtoaji rasmi wa
vifaa vya mawasiliano kwenye mpango huo wa mashindano maarufu kama
Airtel Raising Star (ARS) unaoendeshwa na Airtel.
Airtel
inatoa huduma za mawasiliano kwa simu za mkononi kwenye nchi 20 barani
Asia na Africa huku Samsung ikiwa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya
vifaa vya kisasa vya elektoniki.
Chadema wamtuhumu Mwakyembe kutoa zabuni kinyume cha sheria
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtuhumu Waziri wa Uchukuzi,
Dk Harrison Mwakyembe kwamba alitoa zabuni ya ujenzi wa bandari ya
nchikavu kwa kampuni inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinyume
cha sheria za ununuzi. Chadema
walisema jana kwamba, kampuni hiyo ni Jitegemee Trading Company ambayo
ilipewa zabuni ya ujenzi wa bandari katika Viwanja vya Sukita pasipokuwa
na mchakato wa kushindanisha kampuni nyingine.
Mkurugenzi
wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema:
“Mwakyembe aseme alitoa zabuni hiyo kwa Jitegemee kwa kuzingatia vigezo
gani? Kampuni ngapi zilishindanishwa katika mchakato huo na asipofanya
hivyo hastahili kukaa wizarani hapo bali alipelekwa Segerea gerezani
kwani ni kosa kubwa kutoa zabuni kinyemela.”
Hata
hivyo, Dk Mwakyembe, ambaye yuko jimboni kwake Kyela mkoani Mbeya
alipoulizwa kuhusu madai hayo alijibu na kukata simu; “Mimi nina kazi ya
kuongoza wizara na wao Chadema wana kazi ya kuchonga mdomo, hivyo
waache mimi niongoze Serikali.
MAUNO YA WOLPER YAWACHENGUA WATU UKUMBINI
Baada ya kuonesha vitu adimu ambavyo havikuoneshwa na staa yeyote kati ya waliomtangulia, wageni waalikwa walishangilia na kupiga makofi hadi aliporejea sehemu aliyokaa awali.
RAY ASALIMU AMRI JUU YA FILAMU YAKE INAYO SHUTUMIWA KUUDHALILISHA UKATOLIKI
Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
HATIMA
ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa
imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji
huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.Kanisa Katoliki nchini
linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo
kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna
ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.
Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.
Akipiga
stori na paparazi wetu, Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe
vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani
hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati mwingine. “Asilimia
85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina
ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije
kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.
Subscribe to:
Posts (Atom)