Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtuhumu Waziri wa Uchukuzi,
Dk Harrison Mwakyembe kwamba alitoa zabuni ya ujenzi wa bandari ya
nchikavu kwa kampuni inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinyume
cha sheria za ununuzi. Chadema
walisema jana kwamba, kampuni hiyo ni Jitegemee Trading Company ambayo
ilipewa zabuni ya ujenzi wa bandari katika Viwanja vya Sukita pasipokuwa
na mchakato wa kushindanisha kampuni nyingine.
Mkurugenzi
wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema:
“Mwakyembe aseme alitoa zabuni hiyo kwa Jitegemee kwa kuzingatia vigezo
gani? Kampuni ngapi zilishindanishwa katika mchakato huo na asipofanya
hivyo hastahili kukaa wizarani hapo bali alipelekwa Segerea gerezani
kwani ni kosa kubwa kutoa zabuni kinyemela.”
Hata
hivyo, Dk Mwakyembe, ambaye yuko jimboni kwake Kyela mkoani Mbeya
alipoulizwa kuhusu madai hayo alijibu na kukata simu; “Mimi nina kazi ya
kuongoza wizara na wao Chadema wana kazi ya kuchonga mdomo, hivyo
waache mimi niongoze Serikali.