Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru aliyepumzishwa katika chumba cha Dharura katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili leo.Mzee Kingunge alikimbizwa Hospitalini Hapo
Baada ya Kujisikia Vibaya.jopo la Madaktari Bingwa linamfanyia uchunguzi
Mzee Kingunga ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.Aliyesimama Nyuma ya Rais
ni mke wa Mzee Kingunge na kushoto ni Mtoto wa Mzee Kingunge Bwana
Kinjekitile(picha na freddy Maro)
Friday, March 22, 2013
Rais Kikwete awataka vijana wawe wazalendo, wasifurahie nchi inaposemwa vibaya
Rais wa JK amewataka
vijana kuacha kushabikia watu wanaoisema nchi vibaya, amesema enzi zao
watu waliokuwa wakiisema nchi vibaya walikuwa wanawachukia tofauti na
saizi vijana wanashabikia!
Akizidi kuongea,
kuwa endapo nchi itasemwa vibaya basi wao huchukia!
Kauli hiyo ameitoaJana jijini
D'Salaam
WAZIRI SITTA ACHONGEWA KWA LOWASSA
Edward Lowassa
KWA UFUPI
Historia ya kisiasa baina ya vio ngozi hao inakifanya kikao cha
leo kuwa mvuto wa aina yake kwani kitendo cha wabunge kuichongea Wizara
ya Sitta kwa Kamati ya Lowassa kitatoa mwanya wa mpambano kati ya
wanasiasa hao wawili.
Wakati hayo yanatokea, kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake,
Edward Lowassa itakutana na Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Samuel
Sitta kujadili mambo mbalimbali yakiwamo sera ya Tanzania katika jumuiya
hiyo.
Lowassa, alijiuzulu Uwaziri Mkuu 2008 wakati Sitta akiwa Spika
na inasadikiwa kwamba tukio hilo lilijenga ufa kati ya wanasiasa hao
wawili, ambao tayari wanatajwa katika kinyang’anyiro cha Urais 2015.
Wakizungumza mbele ya kamati hiyo, wabunge wa EAC walisema
wizara hiyo haijawapa mwongozo wa kutetea maslahi ya Tanzania ndani ya
jumuiya, jambo ambalo linawafanya washindwe kuchangia hoja zenye uzito.
“Tunatengwa na wizara, jambo ambalo linatufanya tutoe hoja
tunazozijua wenyewe, kutokana na hali hiyo wanapaswa kubadilika,”alisema
Shyrose Bhanji.
Aliongeza kuwa kila wanapojaribu kuwasiliana na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, wamekuwa waki pigwa kalenda, jambo ambalo linawafanya
kupata taarifa nyingine kupitia vyombo vya habari.
“Tulitarajia tungeelezwa msimamo wa nchi, lakini mpaka sasa
hatujaelezwa chochote na kwamba kila mmoja anachangia kutokana na upeo
wake,” aliongeza. Mbunge mwingine, Abdallah Mwinyi alisema mpaka sasa
Tanzania haina sera ya mtangamano ambao utawaweka pamoja wabunge hao
katika kujadili mambo ya jumuiya.
“Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zina sera ya
mtangamano ambazo zinawaweka pamoja wabunge kujadili mambo mbalimbali
yanayohusu maslahi ya nchi zao, lakini sisi hatuna, wakati Rwanda
imejiunga juzi tu tayari wameandaa sera inayowapa mwongozo wabunge wao,”
alisema Mwinyi.
Sitta akana
Alipoulizwa juu ya malalamiko, Sitta, ambaye jana jioni alikuwa
anahudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu, alijibu
kwa ujumbe mfupi wa maandishi;”Si kweli...niko kwenye kikao nitakupigia
baadaye.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Stargomena Tax
amewashangaa wabunge hao kwa kulalamika kukosa ushirikiano na kwamba
madai hayo si ya kweli.
“Hivi wabunge hawa wanataka tuwape ushirikiano wa aina gani?
Mbona tumekuwa tukikutana nao mara kwa mara na kuwapa misimamo ya nchi?
“Tulishakaa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na tuliwapa hadidu
za rejea ili wawape wabunge wa Afrika Mashariki,” alieleza Dk Tax.
Dk Tax pia alisema wamechapisha kijitabu cha kuwapa mwongoza wa
maeneo ya kuzingatia wakati wanapokwenda kwenye vikao vya Bunge la
Afrika Mashariki.
Miss Utalii Tanzania 2012/13 watembelea Ukumbi wa Kimataifa na kisasa wa Makumbusho ya Taifa.
Washiriki
wa Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13,jana
wametembelea Ukumbi wa kwanza na wa Kisasa na wa aina yake Tanzania
ambao unamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kurugenzi ya
mambo ya kale na makumbusho ya Taifa uliopo ndani ya Makumbusho ya Taifa
jirani na Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) karibu na maeneo ya Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Wakiwa
katika Ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 470 kwa wakati mmoja,
walishuhudia Viti,Mitambo na vifaa vingine vya kisasa vyenye uwezo wa
kuendesha Matamasha na mashindano ya Urembo kwa kiwango cha hadhi ya
nyota tano.
Wengi
wa washiriki hao walionyesha hamasa na kujaribu kuwashawishi viongozi
na wakuu wa msafara wao ili kufanya Fainali hizo katika Ukumbi huo ambao
umekuwa ni kivutio kikubwa, jambo ambalo Viongozi na kamati iliokuwa na
jopo la msafara huo lilionekana kukubaliana na mawazo ya nia ya warembo
hao ya kuomba Fainali hizo zifanyike ndani ya Ukumbi huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo
nchini na Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo,kuhusu uwezekano wa
kuandaa Fainali hizo katika Ukumbi huo wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM
THEATRE, alisema kuwa kila jambo ni mipango, hivyo na kwa kuwa lengo na
nia ya Mashindano ya Miss Utalii ni kutangaza Vivutio vya Taifa kuna
uwezekano pia Fainali hizo zikafanyika hapo ikiwa pia ni kuwapa heshima
Wizara ya Maliasili na Utalii ambao ndiyo walezi wakuu wa mashindano ya
Miss Utalii Tanzania kwa kuwa wao ndiyo wamiliki wa Ukumbi huo ambao kwa
sasa unaonekana kuwa ni kati ya kumbi pekee zilizojengwa kisasa na
hadhi ya kimataifa hapa nchini Tanzania.
ziara
hiyo ya kutembelea Ukumbi huo kwa washiriki wa Miss Utalii Tanzania
2012/2013 iliandaliwa na Washiriki wenyewe baada ya kuusikia sifa zake
kutoka kwa watu mbalimbali na Mitandao ya Kijamii.
Aidha
Chipungahelo amesema kwamba warembo hao wanatarajia kupanda katika
jukwaani baada ya kutoka kwenye ziara ya kutembelea hifadhi za Taifa
ambazo ni pamoja na Saadan, Mikumi, Udzungwa, Mkomanzi, Arusha na Mlima
Kilimanjaro watakaokuwa wameambatana na waandishi wa habari.
Akizungumzia
hali ya Ukumbi huo Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo
amesema kwamba ni heshima kubwa kwa Taifa na sekta nzima ya Utalii kuona
Warembo ambao wanatangaza Utalii wa Nchi yetu wakivutiwa na ukumbi huo
hata kufikia kupeleka maombi ya kutaka wao kuwa Warembo wa kwanza
kupanda katika jukwaa hilo la Ukumbi wa kisasa na wa kimataifa wa
NATIONAL MUSIUM THEATRE ulipo ndani ya Makumbusho ya Taifa ambao ni
kivutio kikubwa kwa sasa katika anga za Burudani na sanaa.
“Ukumbi
ni mzuri kama ambavyo wenyewe wandishi mlivyoona na kutazama, hakika ni
jambo la kujivunia na kusifiwa kwa Wizara yetu, maana unaonekana ni
jambo la kujipanga hadi kuweza kutengeneza kwa ubora huo unaoonekana
sasa, bila shaka nyie wenyewe mtaona ni kwa kiasi gani Umeandaliwa,
lakini hata hivyo ni changamoto kwa Wizara zingine katika kubuni na
kuweka rasilimali kama hizi kwa manufaa ya Taifa, kama ambavyo mnaona
wenyewe, kwani hata Washiriki wamefurahi na hata kusifia sana hivyo pia
nachukua fulsa hii kuishukuru Wizara kwa kuwekeza Ukumbi wa Kisasa ambao
ni faida kwa Taifa” alisema Chipungahelo.
Pia
aliendelea kusisitiza na kuomba wadau na wapenzi mbalimbali wa
mashindano haya kujitokeza kuunga mkono kudhamini na kununua tiketi siku
ya shindano..
Washiriki
wa Miss Utalii Tanzania wakiwa wanatembelea Ukumbi wa Kimataifa wa
Makumbusho ya Taifa(NATIONAL MUSEUM THEATRE).
Mahakama ya Zimbabwe yaweka ngumu kumuachia mwanasheria Mtetwa kwa dhamana.
Mahakama nchini Zimbabwe imekataa kumuachia
kwa dhamana mwanasheria anayetetea haki za binadamu Beatrice Mtetwa na
wasaidizi wanne wa Waziri Mkuu Bw. Morgan Tsvangirai.
Mwanasheria huyo Mtetwa alikamatwa Jumapili
iliyopita akishutumiwa kuzuia mkondo wa sheria kufanya kazi yake na
atabakia kizuizini hadi tarehe 3 mwezi Aprili mwaka huu.
Wasaidizi wane wa Bw. Morgan Tsvangirai
wanashikiliwa kwa kutuhumiwa kujifanya maaafisa wa polisi, lakini
wamekana tuhuma hizo.-DW.
Thursday, March 21, 2013
WOLPER, HARTMANN WAPATA AJALI
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amenusurika kufa ajalini baada ya gari lake kugongana na gari lingine.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, jirani na nyumba ya staa mwenzake, Wema Sepetu ambapo Wolper aliyekuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota-Brevis Saloon alivaana uso kwa uso na gari lingine aina ya Toyota-Nadia.
Kwenye ajali hiyo, gari la Wolper lilibondeka mbele na kuvunjika kioo cha pembeni (side mirror).
Wolper.
Akizungumza na mwandishi wetu, Wolper alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kumshukuru Mungu kwa kumnusuru kwani hakuumia popote.
“Nilikuwa na mdogo wangu tunaelekea gereji kufuata gari langu, hili nililopata nalo ajali, siyo la kwangu hata sijui itakuwaje!” alisema Wolper.
Hartman Mbilinyi.
Wakati huohuo, Hartman Mbilinyi ambaye ni prodyuza wa filamu, Jumatatu usiku alipata ajali baada ya gari lake kugongana na pikipiki wakati akirudi nyumbani kwake, Tegeta.
MAMA LINEX AMKATAA MCHUMBA WA KIZUNGU WA LINEX
Sunday
Mangu ‘Linex’ akiwa na mchumba wake Suvi Rikka.
SIKU chache baada ya Mbongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’
kumvisha pete ya uchumba demu wake mtasha, Suvi Rikka, mama wa staa
huyo, Imelda Barnabas ameibuka na kumchana mwanaye kuwa haitambui pete
wala mchumba huyo kwa kuwa kitendo hicho hakina baraka zake wala za
familia.
Shemeji yetu katika pose
Linex alipoulizwa juu ya sakata hilo,
alifunguka:
“Yah! Bi mkubwa amenijia juu ile
mbaya, ila najitahidi kumuomba msamaha, hope atanielewa.”
JACK WOLPER NA RADO WAJIPANGA KUTOKA NA "MAHABA NIUE"
Muigizaji
wa filamu mwenye mvuto nchini, Jacquiline Wolper hivi karibuni
ataonekana kwenye filamu mpya aliyoigiza na Simon Mwapagata maarufu kama
Rado iitwayo Mahaba Niue.
Akiongea na mtandao wa bongomovies, Rado amesema katika kuwapa raha zaidi mashabiki wao, filamu hiyo itatoka na zawadi ya bure ya kalenda.
Filamu hiyo imetayarishwa na Step Entertainment.
Akiongea na mtandao wa bongomovies, Rado amesema katika kuwapa raha zaidi mashabiki wao, filamu hiyo itatoka na zawadi ya bure ya kalenda.
Filamu hiyo imetayarishwa na Step Entertainment.
PENZI LA MWANAFUNZI LAZUA BALAA LASABABISHA VIZEE KUPIGANA HADHARANI
Kwa kawaida tumezoea kusikia kuwa vijana wakipigana kuhusu wanawake huku tukidhani kuwa wivu wa mapenzi unawatesa vijana peke yao kumbe si kweli mpaka wazee nao wanateswa sana na wivu, Hiki ndicho kilicho tokea katikati ya jiji ambapo wazee wawili walinasa na kamera yetu wakitaka kupigana kisa denti wa shule aliyekuwa akiwachanganya wote wawili bila wao kujijua utata ulikuja pale wazee hao marafiki mmoja wao alipopigiwa simu na msichana huyo baada ya kumaliza kuongea ndipo mzee wa jirani alipouliza huyo nani mwenzake akajibu huyu mpenzi wangu zai hapo ndipo ugomvi ulipoanza na wazee hao kutaka kupigana kisa mwaafunzi wa kidato cha tatu. |
Wanafunzi washinda danguroni Dar
Dar
es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata
ya Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es Salaam, wametajwa
kujiingiza katika kashfa ya ngono, kuvuta na kuuza bangi katika moja ya
nyumba zinazozunguka shule hiyo.
Hilo ni tukio lingine jipya, kwani mwishoni mwa mwaka jana, kuliibuka matukio ya ajabu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi, Ruaruke, Rufiji mkoani Pwani ambao walielezwa kujihusisha na uvutaji bangi hata kukonyeza na kubaka walimu wao.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Yasinta Assey akionyesha baadhi ya nguo na viatu vya wanafunzi vilivyokutwa katika eneo linalodaiwa kuwa danguro linalotumiwa na wanafunzi wa shule hiyo, jana. Picha na Pamela Chilongola
Mkuu wa Sekondari hiyo, Jasinta Assey alikiri na kusema kwamba vitendo vya uvutaji bangi na biashara ya ukahaba kwa wanafunzi wake, vinachangiwa na askari wa Kituo kidogo cha Stakishari ambao alidai wanachukua rushwa kwa wauzaji wa bangi na nyumba bubu za wageni. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Shule hiyo, Jasinta Assey alisema ni kawaida ya polisi hao kwenda kwenye nyumba hizo kunakofanyika biashara hizo na kuchukua rushwa badala ya kutatua tatizo.
Alisema ongezeko la utoro katika shule hiyo ni tatizo kubwa na wanafunzi wa kidato cha nne wanaosoma masomo ya sanaa ndiyo wanaoongoza kwa kuvuta bangi na kwenda kufanya ngono katika nyumba zilizo jirani na eneo la shule hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ilala, Marietha Minangi alisema hajapata taarifa za hali hiyo.
“Ngoja nimtume Mkuu wa Kituo cha Polisi Stakishari afuatilie kwa karibu,” alisema Minangi na kuongeza: “Lakini ngoja nikwambie, hili suala nakumbuka liliwahi kuripotiwa 2011 wakati nikiwa mkuu wa kituo hicho; nililishughulikia na tulibaini kuwa hakuna mwanafunzi ambaye alikuwa anaenda kwenye nyumba hizo kuvuta bangi wala kufanya ngono.
“Ngoja nimtume Mkuu wa Kituo cha Polisi Stakishari afuatilie kwa karibu,” alisema Minangi na kuongeza: “Lakini ngoja nikwambie, hili suala nakumbuka liliwahi kuripotiwa 2011 wakati nikiwa mkuu wa kituo hicho; nililishughulikia na tulibaini kuwa hakuna mwanafunzi ambaye alikuwa anaenda kwenye nyumba hizo kuvuta bangi wala kufanya ngono.
“Kilichotokea
kwa wakati huo ni kwamba, tuliwachukua baadhi ya wanafunzi ili
watupeleke mahali walipokuwa wakifanyia vitendo hivyo kutokana na
maelezo na vielelezo vyao, lakini hatukubaini hizo sehemu.
“Inawezekana basi haya mambo yameibuka upya baada ya kuona kuna mkuu wa kituo mwingine mpya,” alisema Kamanda Minangi.
Kutokana na matendo hayo, wanafunzi wengi walifanya vibaya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka jana.
“Walifeli sana mwaka jana hawa, walimu wapo, tunawapa nyenzo lakini hawataki, ninaiomba Serikali kuingilia kati suala hili kwani ni la muda mrefu na ni faida ya vijana hawa,” alisema.
Shule ya Majani ya Chai ilishika nafasi ya 61 kimkoa kati ya shule 226 wakati ngazi ya taifa, ilishika nafasi ya 543 kati ya shule 3,392.
Wanafunzi 274 walijisajili kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana na kati yao 130 walipata sifuri, wakati waliopata daraja la nne ni 85, waliopata Daraja la Tatu ni 18 wakati waliopata daraja la pili ni watano. Hakukuwa na daraja la kwanza na wanafunzi 36 hawakufanya mtihani.
“Baada ya kuona utoro umekithiri shuleni hapo, nilikwenda kutoa taarifa kituo kidogo cha Polisi Stakishari, lakini hawakuonyesha ushirikiano matokeo yake wanakwenda kwa wenyeji hao na kuchukua rushwa.
“Hili inaonekana kama ni dili la hawa askari, kwani wapo walionifuata na kunieleza niache kufuatilia, lakini mimi niliwaambia nitafuatilia tu na ilifikia hatua nikatishiwa maisha.
“Baada ya kuona nazidi kutishiwa maisha, niliogopa, nikaacha...na hivi ninavyoongea na wewe, najua tu watanifuata kwani nimeshaambiwa nikipita peke yangu eneo wanakofanyia biashara zao watanifanyia kitu kibaya,” alisema Assey.Mwalimu huyo alisema kwamba, wanafunzi wa kidato cha nne wanaosoma masomo ya sanaa wapo 54, lakini wakati mwingine utakuta wanafunzi watano tu darasani na waliobakia wanakwenda kuvuta bangi na kufanya vitendo vya ngono.
Assey alisema kuwa iliwahi kutokea wasamaria wema waliwapelekea baadhi ya nguo na viatu vya wanafunzi wa shule hiyo vilivyokutwa eneo wanakofanya biashara hiyo ya haramu.
“Hili darasa linaongoza kwa utovu wa nidhamu na limeshindikana...Nilikuwa nawategemea sana polisi, lakini hawaonyeshi ushirikiano wowote ule...Unaona hizi nguo za wanafunzi zililetwa na mama mmoja baada ya kuzikuta kwenye danguro ‘bubu’,” alisema Assey huku akionyesha sare hizo za shule.
SHILOLE, BABY MADAHA WAFUATA NYAYO ZA WEMA
WAREMBO wawili wanaotesa katika soko la muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wameamua kufuata nyayo za Wema Sepetu kwa kunyoa nywele na kuonekana katika muonekano mpya.
Akizungumza na paparazi wetu, Shilole ambaye amenyoa nywele staili ya kiduku alisema ameamua kufanya bhiv yo ili kuwa na muonekano wa tofauti kwani watu wameshamzoea kila siku kumuona na mawigi na rasta.
Kwa upande wa Baby Madaha alisema ameamua kubadilisha mfumo wa maisha kuanzia nywele hadi mavazi kwani huu ni mwaka mpya hivyo kutoka na staili mpya.
Hivi karibuni Wema alikuwa wa kwanza kutangaza kuwa na muonekano tofauti kwa kutupia picha zake mtandaoni zilizomuonesha akiwa amenyoa.
CCM, Chadema Dar wamgeuzia kibao JK
Ni
nadra kutokea lakini wafuasi wa vyama vya siasa vya CCM na Chadema,
wameungana kumweleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu kero ya maji eneo la
Kimara-Golani, Dar es Salaam.
Rais Kikwete alikutana na hali hiyo wakati akifungua Daraja
la Kimara jana, tukio hilo liliwakusanya watu wengi hasa wanachama wa
CCM na Chadema waliokuwa wamevalia sare za vyama vyao.
Wafuasi wa Chadema waliongozwa na Mbunge wa Ubungo, John
Mnyika ambao walikuwa wakipeperusha bendera za chama chao na kuimba
nyimbo mbalimbali huku wakidai maji. Hata hivyo, kutokana na hali hiyo,
wafuasi wa CCM waliungana na wenzao wa Chadema, kupiga kelele juu ya
suala hilo kiasi cha kugusa hisia za Rais Kikwete.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa daraja hilo, Rais Kikwete
aliahidi kuitisha kikao Jumatatu ijayo kitakachomhusisha Profesa
Maghembe na maofisa wa wizara yake, wabunge wa Dar es Salaam, Mkuu wa
Mkoa, wakuu wa wilaya ili kuweka mikatati ya pamoja kutafuta ufumbuzi wa
suala hilo.
“Ninaomba Machi 25... tukutane ili tuweke mikakati ya pamoja
kutafuta ufumbuzi wa suala hili,” alisema Rais Kikwete.
Akiwa Hospitali ya Mwananyamala, Rais Kikwete alizindua
maabara ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi na akazungumzia suala la dawa
za kulevya kwa kusema atahakikisha mapambano yanaendelea kwani dawa hizo
zinaua nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.
KISA KINENE KESI YA LWAKATARE
MBOWE ASEMA HUO NI
MTIRIRIKO WA MABAVU YA DOLA
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana ilimfutia kesi ya makosa ya
ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph, kisha
kuwakamata tena na kuwafungulia kesi mpya yenye mashitaka yaleyale.
Awali
ilielezwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP), Dk. Eliezer Feleshi,
aliwasilisha hati ya kuwafutia kesi washitakiwa kwa sababu hana haja ya
kuendelea nayo.
Hata hivyo
baada ya kuachiwa, Lwakatare na mwenzake walikamatwa tena na kufikishwa
mahakamani hapo kisha kufunguliwa kesi mpya namba 6/2013 ambayo
imepangiwa kwa Hakimu mpya, Aloyce Katemana.
Katika kesi
ya awali namba 37/2013 iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Lwakatare na
wenzake Machi 18, mwaka huu, jana ilikuwa imekuja kwa ajili ya Hakimu
Mkazi, Emilius Mchauru, kuitolea uamuzi wa ama kuwapatia dhamana
washitakiwa hao au la.
Lakini
Hakimu Mchauru alijikuta akishindwa kutoa uamuzi wake kwa
sababu mawakili viongozi wa serikali, Ponsian Lukosi, Prudence
Rweyongeza na Peter Mahugo, waliwasilisha hati hiyo ya DPP chini ya
kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka
2002.
“Kwa kuwa kesi hii Na. 37/2013 ilifunguliwa na
upande wa Jamhuri Machi 18, mwaka huu, na leo kesi hii ilikuja kwa ajili
ya mahakama kutolea uamuzi wa maombi ya washitakiwa kupatiwa dhamana au
la, pamoja na maombi mengine…mahakama hii inasema haitaweza kutoa
uamuzi wake kwa sababu DPP amewasilisha hati ya kutotaka kuendelea
kuwashitaki, hivyo mahakama hii inawafutia kesi washitakiwa wote,”
alisema Hakimu Mchauru.
Baada ya
Hakimu Mchauru kuwafutia kesi, askari kanzu waliwakamata tena
washitakiwa hao na kuwaweka chini ya ulinzi na ilipofika saa 4:20
asubuhi, waliingizwa tena katika ukumbi namba mbili wa mahakama hiyo
mbele ya Hakimu Mkazi mwingine, Aloyce Katemana.
SERIKALI YAAPA KUFA NA MATANGAZO YA DIGITAL
Mkurugenzi
wa Idara Habari MAELEZO, Asah Mwambene.
Serikali
imesema haiwezi kusitisha matangazo ya Digiatl na kurudi kwenye
analojia, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
Mkurugenzi wa Idara HABARI MAELEZO, Asah Mwambene alisema seriakli
haitaraji kurudi kwenye analojia kama baadhi ya watu wanavyotaka .
aliongeza
kwa kusema mpaka kufikia hapa mchakato ulipita na maandalizi yalifanyika
ya kutosha kabla ya kuingia kwenye matangazo ya Digital.
Waziri Mkuu Pinda alipohuduria sherehe za kusimikwa rasmi Papa Francis 1 mjini Roma.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakifanya mahojiano na mtangazaji wa
Radio Vatican, Padri Richard Mjigwa (katikati) kweye moja kati ya
studio za Raido hiyo Mjini Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis 1 Machi 20, 2013.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Picha
juu na chini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakiongozwa na
Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa
Benedikti, Roma kutoka kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma
walikohudhuria sherehe za kumsimikwa kiongozi wa Kanisa Katoliki
Duniani, Papa Francis 1 kwenye viwanja vya Kanisa hiloMachi 19,2013.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakipata maelezo
kuhusu historia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma kutoka kwa
Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa wa
Benedikti, Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa Kiongozi wa Kanisa
Katoliki Duniani, Papa Francis, Machi 202013. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Chakula (FAO), Jose Graziano da Silva wakati
alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo Mjini Roma, Machi 20, 2013.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Chakula , FAO, Bw. Jose Graziano da Silva kutia saini katika kitabu cha
wageni mshuhuri wakati alipotembelea Ofisi za FAO mjini Rome Machi 20,
2013.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO Bw. Jose Graziano da Silva baada ya
mazungumzo yao wakati alipotembelea makao makuu ya FAO mjini Roma,
Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Subscribe to:
Posts (Atom)