Edward Lowassa
KWA UFUPI
Historia ya kisiasa baina ya vio ngozi hao inakifanya kikao cha
leo kuwa mvuto wa aina yake kwani kitendo cha wabunge kuichongea Wizara
ya Sitta kwa Kamati ya Lowassa kitatoa mwanya wa mpambano kati ya
wanasiasa hao wawili.
Wakati hayo yanatokea, kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake,
Edward Lowassa itakutana na Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Samuel
Sitta kujadili mambo mbalimbali yakiwamo sera ya Tanzania katika jumuiya
hiyo.
Lowassa, alijiuzulu Uwaziri Mkuu 2008 wakati Sitta akiwa Spika
na inasadikiwa kwamba tukio hilo lilijenga ufa kati ya wanasiasa hao
wawili, ambao tayari wanatajwa katika kinyang’anyiro cha Urais 2015.
Wakizungumza mbele ya kamati hiyo, wabunge wa EAC walisema
wizara hiyo haijawapa mwongozo wa kutetea maslahi ya Tanzania ndani ya
jumuiya, jambo ambalo linawafanya washindwe kuchangia hoja zenye uzito.
“Tunatengwa na wizara, jambo ambalo linatufanya tutoe hoja
tunazozijua wenyewe, kutokana na hali hiyo wanapaswa kubadilika,”alisema
Shyrose Bhanji.
Aliongeza kuwa kila wanapojaribu kuwasiliana na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, wamekuwa waki pigwa kalenda, jambo ambalo linawafanya
kupata taarifa nyingine kupitia vyombo vya habari.
“Tulitarajia tungeelezwa msimamo wa nchi, lakini mpaka sasa
hatujaelezwa chochote na kwamba kila mmoja anachangia kutokana na upeo
wake,” aliongeza. Mbunge mwingine, Abdallah Mwinyi alisema mpaka sasa
Tanzania haina sera ya mtangamano ambao utawaweka pamoja wabunge hao
katika kujadili mambo ya jumuiya.
“Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zina sera ya
mtangamano ambazo zinawaweka pamoja wabunge kujadili mambo mbalimbali
yanayohusu maslahi ya nchi zao, lakini sisi hatuna, wakati Rwanda
imejiunga juzi tu tayari wameandaa sera inayowapa mwongozo wabunge wao,”
alisema Mwinyi.
Sitta akana
Alipoulizwa juu ya malalamiko, Sitta, ambaye jana jioni alikuwa
anahudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu, alijibu
kwa ujumbe mfupi wa maandishi;”Si kweli...niko kwenye kikao nitakupigia
baadaye.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Stargomena Tax
amewashangaa wabunge hao kwa kulalamika kukosa ushirikiano na kwamba
madai hayo si ya kweli.
“Hivi wabunge hawa wanataka tuwape ushirikiano wa aina gani?
Mbona tumekuwa tukikutana nao mara kwa mara na kuwapa misimamo ya nchi?
“Tulishakaa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na tuliwapa hadidu
za rejea ili wawape wabunge wa Afrika Mashariki,” alieleza Dk Tax.
Dk Tax pia alisema wamechapisha kijitabu cha kuwapa mwongoza wa
maeneo ya kuzingatia wakati wanapokwenda kwenye vikao vya Bunge la
Afrika Mashariki.