Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the
Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini kesho kutwa Ijumaa kwa ndege ya
Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania
(Taifa Stars) itakayochezwa Jumapil9 na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya
Kilimanjaro Hyatt Regency.
Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya
mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karumei katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo
maofisa
na Jumamosi itafanya
mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo
itakayochezwa saa 9 kamili alasiri.
Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho chini
ya Kocha Rachid Taoussi ni Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou,
Younnes Bellakhadar, Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir
Feddal, Younnes Hammal, Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.
Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine
Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal,
Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah
Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef
El Arabi.
Wakati huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi
hiyo zitaanza kuuzwa keshokutwa katika vituo vya Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa
Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa
na Dar Live Mbagala.
Milango siku ya mechi kwa ajili ya
watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili mchana