Saturday, March 02, 2013
Mshindi wa Tigo Smartcard Promotion Julius Kanza awasili nchini Hispania.
Mshindi
wa Tigo Smartcard Promotion Bw. Julius Raphael Kanza akiwa Madrid
Hispania tayari kusubiri pambano la el classico kati ya Real Madrid na
Fc Barcelona litakalofanyika kesho kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Julius Kanza akitembelea sehemu mbalimbali za jiji hilo.
DStv REWARDS YAENDELEA KUIBUA MAMILIONEA: AHMED SALIM SALEH ASHINDA Tshs.5,000,000
Ahmed
Salim Saleh, mshindi wa Tshs, 5,000,000 za DStv Rewards akiwa na uso wa
furaha huku ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa.
Katika
muendelezo wa kampeni ya DStv Rewards kampuni ya MultiChoice Tanzania
inayo furaha kumtangaza rasmi mshindi wake wa tatu. Mshindi huyo ni Ahmed Salim Saleh,
mfanyakazi wa Access Bank ya jijini Dar-es-Salaam.
Kupitia droo ya DStv Rewards, MultiChoice Tanzania inaibua baadhi ya
wateja wao kuwa “mamilionea” ambapo katika kila wiki mteja mmoja huibuka
mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni 5. (Tshs 5,000,000)
Meneja
Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, akiwa na mshindi wa DStv
Rewards kwa wiki ya tatu, Ahmed Salim Saleh, baada ya kumkabidhi mfano
wa hundi ya kitita cha Tshs. 5,000,000 alichojishindia.
DStv Rewards
ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania
kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka
kwao.
Kampeni hiyo maalumu ilianza tarehe 5 February, 2013 na inaendelea mpaka
tarehe 10 April, 2013. Wateja ambao wanakuwa na nafasi ya kuibuka
“mamilionea” ni wale ambao hulipia akaunti zao za DStv kabla
hazitajakatwa kwa kulipia kifurushi chochote kati ya DStv Access, DStv
Family, DStv Compact, DStv Compact Plus na DStv Premium.
Mshindi
wa DStv Rewards, Ahmed Salim Saleh, akisaidiwa na baadhi ya wafanyakazi
wenzake kushangilia kwa kuibuka mshindi wa Tshs, 5,000,000 alizoshinda.
WANAO DAI KUWA LULU MICHAEL KAFANYIWA SHEREHE YA KUTOKA GEREZANI NI WAONGO NA WANAMPANGO WA KUMKWAMISHA KISHERIA..:...FAMILIA YA LULU YANENA
Kulipuka
kwa habari kuwa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’
amefanyiwa sherehe na kigogo baada ya kutoka Segerea, Dar kwa dhamana,
familia yake imecharuka na kudai kuwa hakukuwa na jambo kama hilo wala
haifikirii kufanya hivyo
Habari
za uhakika zilidai kuwa Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila
kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, mara baada ya kuachiwa kwa
dhamana Januari 26, mwaka huu, kuliibuka minong’ono kutoka kwa marafiki
zake mbalimbali walioelezwa kuwa walitaka kumfanyia pati lakini ndugu
walikataa.
Ilielezwa
kuwa licha ya ndugu hao kukataa kumfanyia sherehe ndugu yao (Lulu),
bado kuna kikundi cha watu kiliendelea kueneza taarifa za kizushi kwamba
lazima kuwe na sherehe ya kumpongeza baada ya kutoka gerezani.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana ndani ya familia ya Lulu zilieleza
kuwa taarifa zilizosambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba alifanyiwa
bonge la pati na kikundi hicho kama madai ya awali yalivyokuwa, hazikuwa
na ukweli wowote na mbaya zaidi zililenga kumjengea Lulu mazingira
magumu ya kisheria.
Akizungumza
na mwandishi wetu kwa sharti la kutochorwa jina , dada wa Lulu alisema
kuwa familia ilikerwa kupita maelezo na kuwepo kwa taarifa hizo huku
akisisitiza kwamba hazina ukweli wowote.
“Sisi
kama familia hatujamfanyia wala hatufikirii kumfanyia sherehe ya aina
yoyote kwa ajili ya kumpongeza. Tunaomba ieleweke hivyo na hao
wanaoeneza habari za uongo waache haraka, hatuzipendi,” alisema dada
huyo.
HATIMAYE SERIKALI YAANZA KUJENGA KIWANDA CHA GESI MTWARA
***********
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema jana kuwa ujenzi huo
unaofanywa na Kampuni ya China Petroleum and Technology Development Co-operation
(CPTDC), ambao awali, ulipaswa kuanza wiki iliyopita, umeanza juzi baada ya
Serikali kufikia mwafaka na wananchi wa Kijiji cha Msimbati
kinapojengwa.
“Mkuu wa Wilaya
ya Mtwara (Wilman Ndile) na vijana wake walilazimika kufika Kijiji cha Msimbati,
ambako wananchi walikuwa na mgogoro na watu wa Marine Park,” alisema
Maswi.
KILIMANJARO MARATHON YAZINDULIWA
Maandalizi ya Mbio za
Nyika za Kilimanjaro Maarufu kama Kilimanjaro Marathon 2013 yanafikia kiele hii
leo na kesho ndio kivuvumbi na jasho wakati maelfu ya wanariadha na watu wa
kawaida wakitimua vumbi katika mbio hizo zinazofanyika katiua mji wa Moshi
mkoani Kilimanjaro.
Pichani ni baadhi ya
wakimbiaji wakijiandikisha kwaajili ya kushiriki mbio hizo zitakazo fanyika
Machi 3,2013 mjini Moshi na zitakuwa za makundi mbalimbali 42KM, 21KM na 5km Fun
Run.
Makundi mbalimbali katika
Jamiui nayo yanashiriki ikiwa ni pamoja na walemavu ambao pichani wakiwa katika
banda la kujiandikishia.
Maofisa watakao simamia
Mbio hizo Machi 3, 2013 wakiwa Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi kuchukua
vifaa.
Mbio za kujifurahisha kwa
watoto na watu wazima zipo na hapa wakijiandikisha.
Baadhi ya wadhamini wakiwa
tayari wamesha pamba mabanda yao ndani ya Uwanja wa Ushirika Mjini
Moshi.
Mitaani napo Mabango ya
Mbio hizo yamewekwa
Rais Obama awa miongoni mwa viongozi walioalikwa katika sherehe za kumuapisha rais mpya wa Kenya.
Rais
Barrack Obama wa Marekani amekuwa miongoni mwa viongozi wakubwa wa
dunia walioalikwa katika hafla ya kuapishwa kwa rais wa nne wa Kenya.
Mkuu
wa Huduma za Jamii Francis Kimemia serikali imewaalika viongozi kama
vile Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameroon na Mkuu wa Mataifa ya
umoja wa Ulaya.
Pia
wamealikwa marais wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) ikiwa ni
pamoja na rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania, rais Paul Kagame wa Rwanda na rais Pierre Nkurunziza wa
Burundi.
Rais
mpya wa Kenya anatarajiwa kuapishwa kuchukua madaraka hapo Machi 3
mwaka huu, ikiwa ni wiki tatu baada ya wakenya kufanya uchaguzi.
Wafanyakazi Ikulu Waadhimisha Siku ya Mazingira Afrika kwa Kufanya Usafi wa Mazingira.
Naibu
Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (mwenye blauzi ya kijani) na
Mkurugenzi wa Huduma Ikulu Bw. Julius Mogore(mbele) wakiongoza
shughuli za usafi kuzunguka maeneo ya Ikulu jijini Dar es salaam leo
Machi 1, 2013 katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Afrika. Siku hiyo
itaadhimishwa kitaifa siku ya Jumapili.
Picha
zingine zinaonesha Wafanyakazi wa kila kada Ikulu bila kujali nyadhifa
zao wanafanya kazi bega kwa bega kuhitimisha Siku ya Mazingira Afrika
kwa kufanya usafi.(PICHA NA IKULU).
HUYU NDIYE MSANII MAARUFU ALIYEFARIKI NIGERIA,REST IN PEACE JUSTUS ESIRI
Last Wednesday turned out to be another sad day in the annals of the
Nigerian entertainment industry. It was a day the industry recorded the
death of yet another of its legendary actors, Mr. Justus Esiri. FLORENCE
UDOH reports
The news about the death of veteran actor, Justus Esiri, threw the
Nigerian entertainment industry into mourning last week, while still
trying to recover from the shock of Lugard Onoyemu, Goldie Harvey and
Collins Ifeanyi Chukwu's deaths.
The legendary actor and father of musician, Dr. Sid died on Tuesday night at the graceful age of 71.
Late Esiri, was born on November 20, 1942, in Oria-Abraka, Delta
State. He attended Urhobo College and later went to Germany to study
Engineering before he developed interest for the theatre.
Famous for his role in the popular television series "The Village
Headmaster" in the 80's, Esiri rose to prominence playing the role of a
teacher in that long-running drama on national television. He started
his acting career in Germany and also worked for the Voice of Nigeria
(VON) and German Service as a translator. He was a recipient of the
honorary award, MON from the Federal government of Nigeria.
Polisi wanane mbaroni Afrika Kusini kwa kuhusishwa na kifo cha dereva taxi aliyeburuzwa kwenye gari ya polisi.
Maafisa
wanane wa Polisi nchini Afrika Kusini wamekamatwa kuhusiana na kifo cha
dereva taxi, ambaye anadaiwa kuburuzwa nyuma ya gari la polisi.
Uchunguzi
ulianzishwa kufuatia kutolewa kwa picha ya video, iliyomuonyesha
mwanaume mmoja akiwa amefungiwa pingu kwenye gari na kisha kuanza
kubururwa katika barabara ya Daveyton, mashariki mwa mji wa
Johannesburg.
Mtu
huyo ametajwa kuwa ni Mido Macia, raia wa Msumbiji mwenye umri wa miaka
27, ambaye alifariki baadae akiwa katika kizuizini mwa polisi.
Rais
Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameliita tukio hilo kuwa la kutisha kabisa
na lisilokubalika huku taafifa zikisema takriban maafisa wanane
watafikishwa mahakamani Machi 4, 2013 kuhusiana na tukio hilo.
MWENDESHA MASHTAKA WA ICC YUPO TANZANIA
PINDA AZINDUA TUME NA KUSEMA: TUSAIDIENI KUTAFUTA KIINI CHA KUSHUKA KWA ELIMU
Waziri Mkuu akihutubia leo asubuhi |
Azindua tume ya watu 15, aipa wiki sita kukamilisha kazi
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa
matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na
kuwataka wajumbe wa Tume hiyo watafute kiini cha mserereko wa kushuka kwa
ufaulu kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumamosi, Machi 2, 2013) wakati akizungumza na wajumbe
wa Tume hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es
Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk. Shukuru Kawambwa.
“Nimetafuta takwimu za tangu mwaka 2005, Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani na
kubaini kuwa tangu wakati huo hadi mwaka 2009 tulikuwa tukifanya vizuri, lakini
kuanzia mwaka 2010 hadi 2012 matokeo yamekuwa yakishuka sana,” aliwaambia
wajumbe wa Tume hiyo na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Alisema hali hiyo haikuwa kwenye shule za sekondari za umma (kata) peke yake bali hata
kwa shule za Serikali, za watu binafsi na kwenye seminari ambazo kwa miaka
mingi zimekuwa na sifa ya kufanya vizuri kuliko shule za kawaida.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 2/3/2013
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Academic Staff Assembly
Utangulizi
Wapendwa
waandishi wa habari. Tunaomba kupitia ninyi tuweze kuongea na
watanzania wenzetu kuhusu hali ya amani ilivyo nchini mwetu kufuatia
kila aina ya dalili ya watanzania kukosa uvumilivu wa kidini. Tunatambua
kuwa serikali yetu imefanya mambo mazuri mengi tu nchini, hilo hatuna
mashaka nalo; hata hivyo kama watanzania tunadhani kuna baadhi ya mambo
hayaendi sawa. Hivyo basi, tunaomba kuchukua nafasi hii kuelezea
wasiwasi wetu kuhusu migogoro hii ya kidini inayozidi kukua nchini.
Migogoro
hii ilianza kuvuka kama moshi lakini sasa inaanza kulipuka na kusambaa
zaidi. Tumeshuhudia uchomaji moto wa kanisa kule Mbagala, kumwagiwa
tindikali shekhe mmoja kule Zanzibar na Shekhe mwingine kuuawawa,
kuchomwa makanisa Zanzibar, kupigwa risasi viongozi wa kikristo kule
Zanzibar na pia mgogoro wa kuchinja huko Geita ambako tumeshuhudia
mchungaji mmoja akiuawa.
Mbali
na hayo, kuna matukio kadhaa kwenye shule zetu za sekondari yakihusisha
migogoro ya kidini kati ya wakristo na waislamu. Haya tumeshahudia
yakitokea sekondari za Bagamoyo, Ndanda, Kibiti, Ilboru na kwingineko.
Pia yapo malalamiko yasiyo rasmi kuhusu udini kwenye sehemu za kazi na
kwenye taasisi mbalimbali za serikali. Wapo wanaodai kuwa baadhi ya
taasisi binafsi, za kidini na hata za serikali zinazohudumia watanzania
wengi zimekuwa zikiajiri wafanyakazi kwa misingi ya kupendelea dini
fulani fulani. Jambo hili hata kama ni la kuzungumzwa tu, ni vema
likafanyiwa kazi maana hisia hizi zikipanuka hujenga chuki na
kusababisha watanzania wasielewane.
Subscribe to:
Posts (Atom)