Friday, March 01, 2013

Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.Dianna Melrose awasilisha hati zake za utambulisho ikulu



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Mhe.Dianna Melrose ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi (Picha na Freddy Maro)

Hivi ndivyo Chadema walivyotikisa Mbeya jana


Mapokezi makubwa ya Mh. Freeman Mbowe katika viwanja vya Rwanda Nzovwe jijini Mbeya.



 Burudani mbalimbali pia zilikuwepo





 




Mh. Mbowe pia alimtaka waziri wa Elimu na mafunzo  ya ufundi kujiudhuru pamoja na naibu waziri wa wizara hiyo kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne  na kusema kuwa katika siku 14 alizozitoa zimebaki siku tatu za wao kuendelea kuwepo madarakani na kuongeza kuwa wasipofanya hivyo wataitisha maandamano ya nchi nzima kushinikiza waondolewe katika nafasi hizo. Mara baada ya kauli hiyo Mbowe aliwataka wananchi kuchangia fedha kwaajili ya wahanga siku ya maandamano ambapo zilichangishwa fedha kiasi cha sh. 3, 267, 550/=



 

Wakichangisha fedha kwaajili ya wahanga wa maandamano yatakayofanyika pindi mawaziri wataposhindwa kujiudhuru picha ya kwanza ni Mh. Sirinde, inayofuata ni Mh. Msingwa na ya mwisho ni Mh. Mbowe.

 

Picha na Keny Pino

JOKETI KUPAMBA UZINDUZI KAMPENI YA UNYANYASAJI




Na Mwandishi wetu

MWANAMITINDO nyota nchini, Joketi Mwegelo, anatarajiwa kunogesha uzinduzi wa kampeni ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kike, unaotarajiwa kufanyika keshokutwa, ambapo shughuli mbalimbali na mada zitatolewa.


Joketi, ambaye anawika katika tasnia mbalimbali nchini  ikiwemo urembo, mitindo, muziki na filamu, atashiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama Okoa Mtoto wa Kike Tanzania utakaofanyika katika Kata ya Nyamongo wilayani Tarime, Mara.


Taarifa ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group iliyoandaa kampeni hiyo, Mossy Magere, imesema kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika na Joketi atawasili wilayani Tarime kesho tayari kwa kushiriki na atatoa mada ya masuala ya ujasiriamali kwa washiriki wa tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa.


Mossy alisema kuwa mbali na Joketi, wasanii mbalimbali watashiriki kutoa burudani wakiwemo wasanii nyota wa bongo fleva na wale wa asili wanaotamba mkoani Mara.


'Maandalizi yote ya msingi yamekamilika na kinachosubiriwa ni muda wa uzinduzi ufike, Joketi anatarajiwa kuwasili hapa kesho tayari kwa kushiriki nasi. Atapata fursa ya kutoa mafunzo na mbinu

za kimaisha kwa washiriki ambao wengi ni wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani hapa,' alisema Mossy.


Kampeni hiyo ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi sita, itazinduliwa rasmi keshokutwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, ambaye ameshirikishwa kwa karibu na Kampuni ya Nyumbani Kwanza.
Alisema mchakato wa uundwaji wa klabu za wapinga unyanyasaji  katika shule mbalimbali za sekondari wilayani Tarime ambapo kampeni hiyo inaanzia umekamilika na wanafunzi wamevutiwa na kujiunga kwa wingi kwenye klabu hizo ambazo zitakuwa kichocheo cha kuendeleza kampeni hiyo.


Mossy aliongeza kuwa, uundwaji wa klabu hizo unalenga kukiwezesha kizazi cha sasa na kijacho kuwa mstari wa mbele kukataa vitendo vya unyanyasaji.


“Kila jambo jema huanzia ngazi za chini, kwa sasa tunaendelea kuunda klabu za wapinga unyanyasaji ambazo zitakuwa zikipewa mafunzo na mbinu mbalimbali ili kuwajenga kufahamu madhara wakiwa wangali  wadogo shuleni.

Thursday, February 28, 2013

Rais Kikwete apokea ujumbe Maalum Kutoka Kwa Rais Omar El Bashir wa Sudan.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Omar El Bashir wa Sudan ulioletwa na Mhe.Dkt.Nafie Ali Nafie ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.(picha na Freddy Maro).

SASA WATEJA WA NMB KUWEKA PESA ZAO KUPITIA M-PESA

vodacom
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na  Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakitia sahihi katika mkataba kam ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB na Vodacom wakishuhudia.
VODACOM 2Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na  Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakibadilishana mkataba kama ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB wakishuhudia.
…………………………………………………………………
NMB leo hii  imeweka historia  kwa kuanzisha huduma mpya itakayowawezesha wateja  wake nchini kuweza kuweka amana zao kupitia mawakala zaidi ya 40,000 wa M-Pesa Nchi nzima. Pia wateja wa NMB wataweza kutuma fedha kutoka NMB kwenda MPESA.  NMB na Vodacom zimezindua huduma hiyo rasmi leo hii kwenye makao makuu ya NMB.
Sasa mtu yeyote au wateja wa NMB hawatahitaji kwenda ndani ya benki ili kuweka fedha kwenye akaunti kwani sasa wataweza kuweka fedha kwenye akaunti ya NMB bila kwenda tawini.  Pia sasa wateja zaidi ya 800,000 wa NMB mobile wataweza kutuma fedha kwenda MPESA.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bw.Mark Wiessing, “alisema “Ni huduma ya aina yake ambayo itawezesha mzunguko wa miamala baina ya wateja na benki kufanyika kwa urahisi na haraka, jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini”.

MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO-CHADEMA JOHN MNYIKA:'NCHI IMEINGIA TENA KWENYE MGAWO WA UMEME, SERIKALI IELEZE WANANCHI UKWELI NA HATUA KUHUSU UDHAIFU KWENYE UTEKELEZAJI WA MPANGO WA DHARURA.'

Mbunge wa jimbo la Ubungo-Chadema Mh John Mnyika-
---
Nchi imeingia tena katika mgawo wa umeme kinyume na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo bungeni tarehe 28 Julai 2012. 

Hali hiyo ni matokeo ya Serikali kutozingatia tahadhari niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kwa nyakati mbalimbali kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini juu ya hali tete iliyotarajiwa kuwepo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme. 

Ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuisimamia Serikali nawataka viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuacha kuficha hali ya mambo na kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu mgawo wa umeme uliojitokeza na hatua za haraka zinazochukuliwa kurekebisha hali hiyo. 

Iwapo Wizara na TANESCO hawatatoa matangazo ya ukweli kwa wananchi, kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitaeleza vyanzo vya mgawo wa umeme uliojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa wakati huu ambapo wajumbe wa kamati ya nishati na madini wenye wajibu wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya Bunge katika sekta hizo nyeti hawajateuliwa.


Aidha, pamoja na kutoa maelezo kuhusu mgawo wa umeme, Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO watumie nafasi hiyo pia kueleza hatua zilizochukuliwa kuhusu ukaguzi wa awamu ya pili kuhusu tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa vifaa na uzalishaji wa umeme wa dharura ikiwemo kuhusu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme. 

Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwezi Agosti 2012 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT) iliunda timu ya wakaguzi kufanya ukaguzi maalum wa hesabu za Shirika la Umeme (TANESCO) kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zilitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani tarehe 27 Julai 2012 na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hoja ya Serikali tarehe 28 Julai 2012. 

Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waeleze pia hatua iliyofikiwa kuhusu uchunguzi mwingine uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuanzia mwezi Agosti 2012 wa mchakato wa ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu ununuzi huo suala ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka pia tarehe 27 Julai 2012 liundiwe kamati teule ya Bunge ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika. 


Wenu katika uwakilishi wa wananchi, 

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini 

27 Februari 2013

Mtanzania apewa uwaziri Rwanda

RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.

Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).

Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija... “Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.”

Naibu Makamu Mkuu - Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Profesa Makenya Maboko alisema Profesa Rwakabamba alifanya kazi katika chuo hicho na aliondoka akiwa Mkuu wa Kitivo cha Uhandisi.

“Aliondoka wakati Kagame alipoingia madarakani na alikwenda kuongoza Taasisi ya Teknolojia ya Kigali (KIST) kabla ya kwenda katika Chuo Kikuu cha Kigali,” alisema Profesa Maboko.

Msomi huyo alikwenda Rwanda mwaka 1997, baada ya kuombwa na Rais Kagame ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake baada ya kumalizika vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.

Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa kwanza wa KIST na kukifanya kuwa miongoni mwa vyuo bora barani Afrika kwa masuala ya teknolojia jambo lililomfurahisha Rais Kagame.

Baada ya mafanikio hayo, Rais Kagame alimteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, Butare ambako pia alijizolea sifa baada ya kusimamia vyema ujenzi wa mabweni kwa wingi na kiongozi huyo alimtunukia uraia wa nchi hiyo kama zawadi.

Hata hivyo, Profesa Rwakabamba atakuwa amelazimika kuukana uraia wa Tanzania kwa kuwa katiba ya nchi hairuhusu uraia wa nchi mbili.
Profesa Rwakabamba alipata elimu ya msingi huko Muleba na akajiunga na Shule ya Sekondari ya Ihungo.

Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds, Uingereza na kupata Shahada ya Uhandisi mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika fani hiyohiyo.
Chanzo: Mwananchi 

Tigo yaboresha huduma za mawasiliano na KABAANG


Meneja Chapa ya Tigo bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya  kifurushi cha KABAANG kwa ajili ya wateja wao.kulia ni bi. Jacqueline Nnunduma Mtaalam wa ubunifu wa ofa za Tigo.
Mbunifu wa ofa za Tigo bi. Jacqueline Nnunduma akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya kifurushi cha KABAANG.kushoto bw. William Mpinga Meneja Chapa ya Tigo.
Mshindi wa Tigo smartcard promotion bw. Julius Raphael Kanza akiwa uwanja wa ndege J.K Nyerere akiongea na waandishi wa habari kabla ya safari yake ya kuelekea Madrid nchini Hispania kutazama mechi kati Real Madrid na Fc Barcelona jumamosi wiki hii itakayofanyika kwenye uwanja Santiago Bernabeu.

Tigo Tanzania imezindua bidhaa mpya ijulikanayo kama "KABAANG" ambayo itawapa wateja wake fursa ya kupata muda wa maongezi wa bure, kifurushi cha intanet na ujumbe mfupi bila kikomo kwa kujumuisha huduma hizi kuu tatu kwenye kifurushi kimoja.


“KABAANG” ni kifurushi cha wiki ambacho mteja akijiunga anapata dakika 300 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, anapata kifurushi cha intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi bila kikomo.


" Tuliona kuna haja kubwa sana ya kuzindua bidhaa itakayohusisha mahitaji mbalimbali ya wateja wetu kwenye kifurushi kimoja cha bei nafuu na kitakachowapatia wateja matumizi mbalimbali. 


Kifurushi hiki cha wiki kinamruhusu mteja kutumia huduma mchanganyiko ipasavyo na kwa bei nafuu kabisa na kitawafaa sana wajasiriamali na waajiriwa wa mashirika mbalimbali kwani kitawawezesha kuwasiliana kwa simu, sms na barua pepe muda wowote wakati wakiendelea na mambo mengine kwa shilingi 9000 tu wateja wa Tigo wanapata huduma nyingi na bora zaidi ” alisema Ndg. William Mpinga, Meneja wa chapa ya Tigo.


Ndg. Mpinga aliendelea kwa kusema " kwa kutumia KABAANG wateja wetu wataweza kuwasiliana vizuri zaidi kwani itapunguza mzigo wa uhitaji wao wa kutaka kuwasiliana kila wakati kwani inawapatia bidhaa iliyojumuisha mahitaji yao makuu ya mawasiliano kikazi na kwenye biashara. Mteja anahitaji laini moja tu ya simu kufurahia bidhaa hii bora kutoka Tigo".


Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi atume neno "Kabaang" kwenda 15711, na baada ya hapo atapata ujumbe wa kuadhimisha kujiunga na kuweza kutumia kifurushi. Kabaang inapatikana kwa wateja wote wa Tigo wenye simu zinazotumia intaneti na kinagharimu shilingi 9,000 tu kwa wiki.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Akutana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania,Uganda na Burundi, Bw Philippe Dongie Ikulu Zanzibar

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania,Uganda na Burundi,Philippe Dongie,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili  ya mazungumzo na Rais,leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania,Uganda na Burundi,Philippe Dongie,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.Picha na Ramadhan Othman,ikulu-Zanzibar

MASHINDANO YA MPIRA YA MPINGA CUP YAANZA RASMI LEO


Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Saalam Suleiman Kova akijiandaa  kudaka mpira ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup  inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi  leo kwa muda wa wiki moja. Mpinga cup imedhaminiwa na  Airtel , Rotary  Club, Mr price na Shoprite  ikiwa na lengo la kutoa elimu ya usalama  barabarani kwa waendesha pikipiki na kupunguza ajali barabarani .  akishuhudia kushoto ni  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP.  Mohamed Mpinga
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akidaka mpira ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup  inayowahusisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi  leo kwa muda wa wiki moja. Mpinga cup imedhaminiwa na  Airtel , Rotary  Club, Mr price na Shoprite  ikiwa na lengo la kutoa elimu ya usalama  barabarani kwa waendesha pikipiki na kupunguza ajali barabarani .  akishuhudia kushoto ni  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP.  Mohamed Mpinga. 

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova akikagua timu wakati wa uzinduzi wa  michuano ya Mpinga Cup inayowahusisha  waendesha pikipiki maarufu kama Bodabado inayoanza rasmi leo kwa muda wa wiki moja. Michuano hii imeanza rasmi kwa mechi kati ya Kawe Tiptop na  Manzese anayefata pichani ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani   SACP. Mohamed Mpinga. 
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akikagua timu  kabla ya mechi kati ya  Kawe Tiptop na Manzese leo wakati wa uzinduzi wa michuano ya Mpinga Cup, anayefata pichani ni Meneja Uhusiano wa Airtel  Jackson Mmbando. 

kikosi cha timu ya Kawe Tiptop katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa  mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi
oyesterbay , katikati pichani ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Seleman Kova
akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga.
kikosi cha timu ya Manzese  katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa
mashindano ya mpinga Cup yaliyofanyika leo katika viwanja vya polisi
oyesterbay , katikati pichani ni Kanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es
Saalam Suleiman Kova akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha Usalama  barabarani  SACP. Mohamed Mpinga

WIZARA INAISUBIRIA TUME KUHUSU MUSTAKABALI KWA WALIOFELI KIDATO CHA NNE

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema wizara haina mpango wowote kwa sasa kuhusiana na wanafunzi waliofeli kidato cha nne mpaka pale Tume itakapomaliza kufanya kazi yake ndipo itaamua nini cha kufanya.
Mulugo aliliambia NIPASHE kuwa wizara inasubiri Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imalize kufanya kazi yake, ndipo itatoa uamuzi nini kifanyike juu ya wanafunzi hao.
“Kwa sasa siwezi nikasema chochote kwani tume imeundwa ili kulifanyia kazi jambo hilo, hivyo tunasubiri wamalize kufanya kazi yao ndipo tutatoa kauli ya nini kifanye juu ya wanafunzi walio feli kama ni kurudia tena mtihani au la,” alisema Mulugo.
Alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa wizara yake inazungumziaje juu ya mpango wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu kuandaa mafunzo ya kozi ya muda mfupi kwa vijana wote waliofeli mkoani humo ili kuwapima kama wapo wanaaoweza kusaidiwa kuendelea na elimu ya cheti.
Msambatavangu alitoa uamuzi huo baada ya makubaliano yake na baadhi ya vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha Tumaini (IUCO) na Chuo kikuu cha Ruaha (Ruco) na kukubaliana kutoa mafunzo hayo yatakayo anza Machi mwaka huu.
Mulogo alisema kuwa ni wazo lenye mpango mzuri wa kuwasaidia vijana wengi ambao ni kama wamekumbwa na tatizo kwa sasa, hivyo anacho kifanya Mwenyekiti huyo hakina madhara yoyote na anafanya kama raia mwema aliyeguswa na matokeo hayo
CHANZO: NIPASHE

MAPYA YAIBUKA SAKATA LA MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI , WAANDISHI WATIMULIWA

Hapa mtuhumiwa  huyo akikimbiziwa mahabusu ili kukwepa picha ya  wanahabari leo
Hapa akiingizwa mahakamani leo

                                        
Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi

SAKATA la mtuhumiwa  wa   mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23),limeendelea  kuchukua  sura  mpya  baada ya wanahabari  kunusurika  kichapo  kutoka kwa askari  polisi ambao  walikuwa  wakiwazuia  kusogea katika  chumba  cha mahakama  kusikiliza  kesi  hiyo .

Askari  polisi hao  wakiwa  zaidi ya  10  waliweza kutumia nguvu  za  ziada katika kuwathibiti wanahabari  wa vyombo mbali mbali  waliofika  kusikiliza na kuripoti mwenendo wa kesi hiyo  namba  1 ya mwaka 2012  ya mauwaji ya mwanahabari mwenzao ,Mwangosi  aliyeuwawa septemba 2 mwaka 2012  katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi wakati wa polisi walipokuwa  wakitumia nguvu  kuwatawanya wafuasi wa chama  cha  Demokrasia na maendeleo  (CHADEMA)  aliokuwa katika shughuli za ufunguzi  wa matawi ya chama  hicho.

Hata  hivyo  moja kati ya mbinu  waliyopata  kuitumia  leo  wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa mahakamani hapo ni  kuwafukuza  waandishi  wa habari  eneo hilo la mahakama na kumtoa mtuhumiwa huyo kwa  kificho cha hali ya  juu kwa  kumweka katikati ya  watuhumiwa  wa makosa mingine zaidi ya 8 huku mtuhumiwa akijificha sura  yake  kukwepa kamera za waandishi na baadhi ya askari  wakimkinga ili  kukwepa  kupigwa  picha.

Tukio  hilo  lilitokea muda wa saa 6.10 mchana  wakati mtuhumiwa  huyo askari  Saimoni alipokuwa akitolewa na  watuhumiwa  wengine  kutoka  chumba cha mahabusu ya mahakama  ya hakimu mkazi  mkoa  wa Iringa na kumpeleka katika  chumba cha mahakama ya wazi  kwa ajili ya  kesi hiyo  kutajwa tena.

Hivyo  katika hali ya  kushangaza ni pale askari  hao  kuwataka  wanahabari hao  kusongea  umbali  wa mita  710 kutoka  eneo la Mahakamani  hiyo  wakati mtuhumiwa   huyo akiingizwa katika  chumba  hicho  cha mahakama ya  wazi  mbele ya  hakimu mkazi  wa mahakama ya  mkoa  wa Iringa  Gladys Barthy  ili  kesi  hiyo  iweze  kutajwa  kwa zaidi ya mara  ya tano  sasa bila upelelezi  kukamilika.

Uamuzi  huo  wa askari  hao  kuwataka  wanahabari  hao  kusimama  umbali  wa mita 710 kutoka chumba  cha mahakama  ulionyesha kuwashangaza  hata  baadhi ya  wananchi  waliofika  kusikiliza  kesi na kuwawekea  dhamana  ndugu  zao  na kulazimika  kuungana na  wanahabari  kupinga  uamuzi  huo na kupelekea  askari  hao  kuwafukuza  pia  wananchi hao na kuwataka waungane na  wanahabari kuondoka eneo hilo la  chumba  cha mahakama.

Mbali ya  wanahabari hao  kunyanyasika  wakati mtuhumiwa  huyo akipelekwa  chumba  cha mahakama  kwa ajili ya  kesi hiyo kutajwa  bado  askari  hao  kabla ya  gari la mahabusu  (karandinga)  kufika na watuhumiwa eneo hilo la mahakama  mida ya saa 5.30 asubuhi  bado askari hao  walionyesha  kuwanyanyasa  wanahabari  hao na  mara kwa mara  kuwatawanya kwa kauli nzito za maneno kuwataka  kuondoka maeneo waliyokusanyika  kwa madai  hawapaswi  kusikiliza  kesi hiyo kwani  haipo  katika mahakama ya wazi jambo ambalo  halikuwa  la kweli.

Wakizungumza  juu ya uamuzi  huo  wa askari hao  kutumia  nguvu  za ziada katika kuwathibiti  wanahabari hao  baadhi ya  wananchi  walisema  kuwa  kinachofanywa na jeshi la  polisi mkoani Iringa ni kuzidisha jazba  zaidi kwa  wananchi na kuwa  hawakupaswa  kuwazuia  wanahabari  kutimiza  wajibu  wao.

Alisema Wistone kalinga  kuwa  hata  wao  wananchi  wanashindwa kujua  sababu ya  polisi  kumficha  mtuhumiwa  huyo wakati tayari amefikishwa mahakamani na  kuwa kinachofanywa na polisi ni  kuzidi kulipaka matope  jeshi la polisi na kuondoa kabisa  dhana ya  polisi jamii na ulinzi shirikishi pia uhuru  wa vyombo  vya habari katika  kulitumikia Taifa na  wananchi  wake.

Sanjari na  wananchi hao kushangazwa na tukio  hilo la  polisi kuzuia  wanahabari  pia kwa upande  wake mahakama  hiyo ya hakimu mkazi  mkoa  wa mkoa  wa Iringa  mheshimiwa  Barthy alisema  kuwa  kitendo  kilichofanywa na polisi hao  kuwazuia  wanahabari  si maagizo ya mahakama na kuwa  wanahabari hao  walikuwa  huru  kuingia  kusikiliza  kesi hiyo na  kuhabarisha  umma kwani  hakukiwa na siri wala hakuna maagizo ya mahakama  ya kuwataka  polisi  kuwafukuza  wanahabari mahakamani hapo.

"Kwanza  nawapa pore  sana  kwa misukosuko mlioipata  ....ila  mimi nilikuwa ndani   ya  mahakamani  sikujua  kinachoendelea  huko nje  ya  mahakama ila  nawahakikishieni  kuwa  kesi  hii ilikuwa ikisikilizwa katika mahakama ya  wazi na mlikuwa  huru   kusikiliza " alisema hakimu  huyo akiakimhoji mmoja kati ya  viongozi  wa  polisi kuhusu polisi hao  kunyanyasa  wanahabari na kuwataka  kutorudia kufanya   hivyo  tena.

Mwendesha mashitaka  wa  serikali Blandina Manyanda  aliiomba mahakama  hiyo  kupanga tarehe nyingine ya  kutajwa kwa  kesi hiyo na kuwa  upelelezi  bado haujakamilika na mahakama  hiyo  kupanga tarehe  14 machi ambapo  kesi hiyo  itafikishwa mahakamani  hapo kwa ajili ya kutajwa.

MIZINGA MELU IS A NEW NBC MANAGING DIRECTOR

Melu
The National Bank of Commerce (NBC) has today announced the appointment of Mizinga Melu as its
 
Mizinga is joining NBC from Standard Chartered Bank Zambia where until now she has been Managing Director since 2007. She takes over from Lawrence Mafuru, who left the bank in December, 2012.new Managing Director, subject to regulatory approval. The appointment is with effect from 20th May 2013.
Mizinga has previously served in senior roles at Standard Chartered, including as Global Head of Development Organisations in the United Kingdom where she was responsible for strategy development and implementation as well as Africa Regional Head of Financial Institutions in Kenya and South Africa where she led formulation of Standard Chartered’s FI business strategy in Africa. Prior, she served as Head of Treasury at Standard Chartered Bank Tanzania between 2000 and 2003.
Mizinga holds a Masters in Business Administration (MBA) from Henley Management College (UK) and is an Associate of the Chartered Institute of Bankers (A.C.I.B). She holds numerous other banking qualifications.
Commenting on the appointment, Barclays Africa Chief Executive Officer and Head of Africa Group Strategy, Kennedy Bungane said: “The appointment of Mizinga reiterates the importance of NBC to our ‘One Africa Strategy’ and we are excited that she is joining us at a time we are making steady progress towards our goal of becoming the go-to bank in Africa.”
Dr. Mussa Juma Assad, Chairman of NBC commented: “The board welcomes Mizinga to NBC and looks forward to working with her in maintaining the position of NBC as a leading bank in Tanzania.”
Commenting on her appointment, Mizinga said: “NBC has over the years proven to be an important financial services provider in Tanzania. I am privileged to have the opportunity to lead this great bank at this important moment and I am looking forward to working with every colleague in NBC as we continue on our journey of transforming the bank in the market.”
Mizinga will report directly to Kennedy Bungane, Barclays Africa Chief Executive Officer and will be a member of the Barclays Africa Executive Committee.

Wednesday, February 27, 2013

LULU AKANA KUJIHUSICHA LA SUALA LA KUOMBA MSAADA

LULU ambaye kwa sasa yupo uraiani kwa dhamana huku kesi yake ya tuhuma za kuua bila kukusudia ikiendelea, amesema kuwa hajafungua taasisi yoyote wala kuomba 
misaada kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook. 
"Nasikia tu kwa watu eti sijui ninataka wasanii waigizaji kwa ajili ya taasisi yangu, mara nimetoa namba ya simu watu wanichangie ili nitengeneze filamu, sijafanya kitu kama hicho na wala siwezi nahitaji kutulia na kuangalia mambo yangu,"alisema. 
Hivi karibuni kupitia facebook kumeonekana akaunti inayotumia picha na majina ya Lulu kwa kuwaomba wadau wa filamu wamchangie fedha kwa njia ya m-pesa na tigo-pesa. 
Lulu anatuhumiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa msanii wa filamu, Steven Kanumba

Tangazo Kutoka Chadema:Shiriki Shindano la Kubuni Nembo Ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA)


Deogratias Munishi-Katibu Mkuu - BAVICHA
---

Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) liko kwenye mchato wa kutafuta nembo yake ambayo itakuwa kielelezo cha vijana ndani ya CHADEMA. Nembo hii itakuwa alama ya utambulisho na inatarajiwa kutumika katika shughuli na mambo mbali mbali ya vijana ndani ya CHADEMA.

Katika kufanikisha upatikanaji wa nembo, BAVICHA inatambua uwepo wa vipaji mbalimbali vikiwemo vya ubunifu miongoni mwa vijana wa Tanzania ambao baadhi yao ni wanachama na wafuasi wapenda mabadiliko wa Chadema.

Ili kutoa fursa kwa vijana hawa kutumia vipaji vyao na kutoa mchango wao kwa Chama na Baraza lao, BAVICHA imeandaa shindano maalumu la ubunifu wa NEMBO YA BAVICHA na hivyo kukaribisha wale wote ambao wangependa kushiriki kwa kubuni nembo hii.

VIGEZO MUHIMU VYA KUZINGATIWA
Kwa wale wote wenye kipaji cha ubunifu na wangependa kushiriki shindano hili watapaswa kuzingaztia vigezo vifuatavyo katika ubunifu wao;
1.    Rangi zitakazotumika ni lazima ziwe zinatokana na rangi kuu za CHADEMA
2.    Nembo kuu ya Chama inaweza pia kutumika kubuni nembo ya BAVICHA
3.    Mbunifu atoe maana halisi ya nembo atakayoibuni kwa mukhtadha wa vijana na maudhui mapana ya CHADEMA

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...