Deogratias Munishi-Katibu Mkuu - BAVICHA
---
Baraza
la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) liko kwenye mchato wa kutafuta nembo
yake ambayo itakuwa kielelezo cha vijana ndani ya CHADEMA. Nembo hii
itakuwa alama ya utambulisho na inatarajiwa kutumika katika shughuli na
mambo mbali mbali ya vijana ndani ya CHADEMA.
Katika
kufanikisha upatikanaji wa nembo, BAVICHA inatambua uwepo wa vipaji
mbalimbali vikiwemo vya ubunifu miongoni mwa vijana wa Tanzania ambao
baadhi yao ni wanachama na wafuasi wapenda mabadiliko wa Chadema.
Ili
kutoa fursa kwa vijana hawa kutumia vipaji vyao na kutoa mchango wao
kwa Chama na Baraza lao, BAVICHA imeandaa shindano maalumu la ubunifu wa
NEMBO YA BAVICHA na hivyo kukaribisha wale wote ambao wangependa
kushiriki kwa kubuni nembo hii.
VIGEZO MUHIMU VYA KUZINGATIWA
Kwa
wale wote wenye kipaji cha ubunifu na wangependa kushiriki shindano
hili watapaswa kuzingaztia vigezo vifuatavyo katika ubunifu wao;
1. Rangi zitakazotumika ni lazima ziwe zinatokana na rangi kuu za CHADEMA
2. Nembo kuu ya Chama inaweza pia kutumika kubuni nembo ya BAVICHA
3. Mbunifu atoe maana halisi ya nembo atakayoibuni kwa mukhtadha wa vijana na maudhui mapana ya CHADEMA
No comments:
Post a Comment