Hapa mtuhumiwa huyo akikimbiziwa mahabusu ili kukwepa picha ya wanahabari leo |
Hapa akiingizwa mahakamani leo |
SAKATA
la mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa
kituo cha
Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi askari wa FFU
mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23),limeendelea
kuchukua sura mpya baada ya wanahabari kunusurika kichapo kutoka
kwa askari polisi ambao walikuwa wakiwazuia kusogea katika chumba
cha mahakama kusikiliza kesi hiyo .
Askari
polisi hao wakiwa zaidi ya 10 waliweza kutumia nguvu za ziada
katika kuwathibiti wanahabari wa vyombo mbali mbali waliofika
kusikiliza na kuripoti mwenendo wa kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2012 ya
mauwaji ya mwanahabari mwenzao ,Mwangosi aliyeuwawa septemba 2 mwaka
2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi wakati wa polisi
walipokuwa wakitumia nguvu
kuwatawanya wafuasi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
aliokuwa katika shughuli za ufunguzi wa matawi ya chama hicho.
Hata
hivyo moja kati ya mbinu waliyopata kuitumia leo wakati mtuhumiwa
huyo akifikishwa mahakamani hapo ni kuwafukuza waandishi wa habari
eneo hilo la mahakama na kumtoa mtuhumiwa huyo kwa kificho cha hali ya
juu kwa kumweka katikati ya watuhumiwa wa makosa mingine zaidi ya 8
huku mtuhumiwa akijificha sura yake kukwepa kamera za waandishi na
baadhi ya askari wakimkinga
ili kukwepa kupigwa picha.
Tukio
hilo lilitokea muda wa saa 6.10 mchana wakati mtuhumiwa huyo askari
Saimoni alipokuwa akitolewa na watuhumiwa wengine kutoka chumba cha
mahabusu ya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa na kumpeleka
katika chumba cha mahakama ya wazi kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa
tena.
Hivyo
katika hali ya kushangaza ni pale askari hao kuwataka wanahabari
hao kusongea umbali wa mita 710 kutoka eneo la Mahakamani hiyo
wakati mtuhumiwa huyo akiingizwa katika chumba hicho cha mahakama
ya wazi mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Iringa
Gladys Barthy ili kesi hiyo iweze kutajwa kwa zaidi ya mara ya
tano sasa bila upelelezi kukamilika.
Uamuzi
huo wa askari hao kuwataka wanahabari hao kusimama umbali wa
mita 710 kutoka chumba cha mahakama ulionyesha kuwashangaza hata
baadhi ya wananchi waliofika kusikiliza kesi na kuwawekea dhamana
ndugu zao na kulazimika kuungana na wanahabari kupinga uamuzi huo
na kupelekea askari hao kuwafukuza pia wananchi hao na kuwataka
waungane na wanahabari kuondoka eneo hilo la chumba cha mahakama.
Mbali
ya wanahabari
hao kunyanyasika wakati mtuhumiwa huyo akipelekwa chumba cha
mahakama kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa bado askari hao kabla ya
gari la mahabusu (karandinga) kufika na watuhumiwa eneo hilo la
mahakama mida ya saa 5.30 asubuhi bado askari hao walionyesha
kuwanyanyasa wanahabari hao na mara kwa mara kuwatawanya kwa kauli
nzito za maneno kuwataka kuondoka maeneo waliyokusanyika kwa madai
hawapaswi kusikiliza kesi hiyo kwani haipo katika mahakama ya wazi
jambo ambalo halikuwa la kweli.
Wakizungumza
juu ya uamuzi huo wa askari hao kutumia nguvu za ziada katika
kuwathibiti wanahabari hao baadhi ya wananchi walisema kuwa
kinachofanywa na jeshi la polisi mkoani Iringa ni kuzidisha jazba
zaidi kwa wananchi na kuwa hawakupaswa kuwazuia wanahabari
kutimiza wajibu wao.
Alisema
Wistone kalinga kuwa hata wao wananchi wanashindwa kujua sababu
ya polisi kumficha mtuhumiwa huyo wakati tayari amefikishwa
mahakamani
na kuwa kinachofanywa na polisi ni kuzidi kulipaka matope jeshi la
polisi na kuondoa kabisa dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi
pia uhuru wa vyombo vya habari katika kulitumikia Taifa na wananchi
wake.
Sanjari
na wananchi hao kushangazwa na tukio hilo la polisi kuzuia
wanahabari pia kwa upande wake mahakama hiyo ya hakimu mkazi mkoa
wa mkoa wa Iringa mheshimiwa Barthy alisema kuwa kitendo
kilichofanywa na polisi hao kuwazuia wanahabari si maagizo ya
mahakama na
kuwa wanahabari hao walikuwa huru kuingia kusikiliza kesi hiyo
na kuhabarisha umma kwani hakukiwa na siri wala hakuna maagizo ya
mahakama ya kuwataka polisi kuwafukuza wanahabari mahakamani hapo.
"Kwanza
nawapa pore sana kwa misukosuko mlioipata ....ila mimi nilikuwa
ndani ya mahakamani sikujua kinachoendelea huko nje ya mahakama
ila nawahakikishieni kuwa kesi hii ilikuwa ikisikilizwa katika
mahakama ya wazi na mlikuwa huru kusikiliza "
alisema hakimu huyo akiakimhoji mmoja kati ya viongozi wa polisi
kuhusu polisi hao kunyanyasa wanahabari na kuwataka kutorudia
kufanya hivyo tena.
Mwendesha
mashitaka wa serikali Blandina Manyanda aliiomba mahakama hiyo
kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo na kuwa upelelezi
bado haujakamilika na mahakama hiyo kupanga tarehe 14 machi ambapo
kesi hiyo itafikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.