LULU ambaye kwa
sasa yupo uraiani kwa dhamana huku kesi yake ya tuhuma za kuua bila
kukusudia ikiendelea, amesema kuwa hajafungua taasisi yoyote wala
kuomba
misaada kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
"Nasikia tu kwa watu eti sijui ninataka
wasanii waigizaji kwa ajili ya taasisi yangu, mara nimetoa namba ya simu
watu wanichangie ili nitengeneze filamu, sijafanya kitu kama hicho na
wala siwezi nahitaji kutulia na kuangalia mambo yangu,"alisema.
Hivi karibuni kupitia facebook kumeonekana
akaunti inayotumia picha na majina ya Lulu kwa kuwaomba wadau wa filamu
wamchangie fedha kwa njia ya m-pesa na tigo-pesa.
Lulu anatuhumiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa msanii wa filamu, Steven Kanumba