Wednesday, February 27, 2013

Tangazo Kutoka Chadema:Shiriki Shindano la Kubuni Nembo Ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA)


Deogratias Munishi-Katibu Mkuu - BAVICHA
---

Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) liko kwenye mchato wa kutafuta nembo yake ambayo itakuwa kielelezo cha vijana ndani ya CHADEMA. Nembo hii itakuwa alama ya utambulisho na inatarajiwa kutumika katika shughuli na mambo mbali mbali ya vijana ndani ya CHADEMA.

Katika kufanikisha upatikanaji wa nembo, BAVICHA inatambua uwepo wa vipaji mbalimbali vikiwemo vya ubunifu miongoni mwa vijana wa Tanzania ambao baadhi yao ni wanachama na wafuasi wapenda mabadiliko wa Chadema.

Ili kutoa fursa kwa vijana hawa kutumia vipaji vyao na kutoa mchango wao kwa Chama na Baraza lao, BAVICHA imeandaa shindano maalumu la ubunifu wa NEMBO YA BAVICHA na hivyo kukaribisha wale wote ambao wangependa kushiriki kwa kubuni nembo hii.

VIGEZO MUHIMU VYA KUZINGATIWA
Kwa wale wote wenye kipaji cha ubunifu na wangependa kushiriki shindano hili watapaswa kuzingaztia vigezo vifuatavyo katika ubunifu wao;
1.    Rangi zitakazotumika ni lazima ziwe zinatokana na rangi kuu za CHADEMA
2.    Nembo kuu ya Chama inaweza pia kutumika kubuni nembo ya BAVICHA
3.    Mbunifu atoe maana halisi ya nembo atakayoibuni kwa mukhtadha wa vijana na maudhui mapana ya CHADEMA

MTUHUMIWA WA MAUWAJI WA MWANGOSI KUFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO



 Huyu  ndie askari anayetuhumiwa  kwa mauwaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi atafikishwa tena mahakamani  kesho Alhamisi .

MATUKIO YA ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE RUKWA


IMG_1951
 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea zawadi za kimila za kabila la Wafipa, wakati alipokutana na akina mama wa manispaa ya Sumbawanga kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo tarehe 25.2.2013.

PICHA NA JOHN LUKUWI WA MAELEZO

IMG_1969
 
Akiwa amevalia vazi la asili la akina mama wa kabila la Wafipa, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anashiriki kucheza ngoma ya kabila hilo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga tarehe 15.2.2013.

Tanzania yasaini bil 90/- za maji ili kupanua Miundombinu ya Maji katika Miji mbalimbali nchini



Wizara ya Maji imesaini mikataba ya upanuzi wa miradi ya maji katika mikoa ya Kigoma, Lindi na Halmashauri ya mji wa Sumbawanga ,makubaliano hayo yaliyofanywa kati ya wizara na Wakandarasi watano.

Akisaini mikataba hiyo jana Makao Makuu ya Wizara Ubungo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Chistopher Sayi aliwataka wakandarasi hao kutekeleza miradi hiyo kwa wakati kama mikataba inavyoeleza.


“Natumia nafasi hii kupongeza wakandarasi wote walioshinda zabuni za kutekeleza miradi hii, lakini pia ni mategemeo yangu miradi yote itafanywa kwa wakati kama ambavyo tumekubaliana katika mikataba hii”. Alisema Mhandisi Sayi.


Wakandarasi waliopata fursa ya kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo ni Spencon Services Ltd ambao watahusika na usambazaji na mifumo ya majisafi mkoani Kigoma; Jandu Plumbers na Metito Overseas watahusika na uchimbaji wa visima katika Halmashauri ya mji wa Sumbawanga. 

 Jandu Plumbers na Metito Overseas watahusika na uchimbaji wa visima mkoani Lindi na Technofab-Gammon Joint usambazaji na mifumo ya majisafi katika Halmashauri ya mji wa Sumbawanga, na Overseas Infrastructure Alliance watahusika na usambazaji wa maji na mifumo ya majisafi mkoani Lindi.

Miradi hiyo ambayo itagharimu takriban shilingi bilioni 90 za kitanzania ambayo imefadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Serikali ya Ujerumani.

CHOCOLATE ZAMPONZA WEMA SEPETU NA KUMFANYA APOTEZE "MENO"



CEO wa Endless Fame Films Wema Sepetu amelazimika kujisamilisha kwa daktari wa meno baada ya ulaji wa chocolate kumponza na hivyo kuozesha baadhi ya meno yake.
eb53b55080ba11e2bd6422000a9f12df_7
Kupitia Instagram, Miss Tanzania huyo wa zamani, ameshare picha akiwa kwenye clinic ya meno kung’oa jino lililokuwa likimsumbua.“Apparently I have 8 cavities…. oh god… does this mean no more chocolate for me,” ameandika. Kwa waliowahi kuumwa na jino wanaujua muziki wake, so get well soon Wema.

Rais Kikwete akagua Ukumbi Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam


8E9U3337Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali
8E9U3420Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali.Picha na Freddy Maro

MSANII AMTELEKEZA MTOTO STENDI YA UBUNGO



MREMBO aliyewahi kupamba video kadhaa za wasanii wa Bongo Fleva ukiwemo wimbo wa Kidato Kimoja ulioimbwa na J.I, anayekwenda kwa jina la Maya Silemwe, amedaiwa kumtelekeza mwanaye wa kumzaa aitwaye Junior Justine (3). 


Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo aliokolewa na msamaria mwema.


Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia wameumizwa sana na kitendo kilichofanywa na Maya.

KUTOKA IKULU,TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji na Balozi Mstaafu Mheshimiwa Hamis Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa BARAZA LA MAADILI.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, 26 Februari, 2013 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Februari 18, mwaka huu, 2013.
 “Mwisho”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
26 Februari, 2013

Leo ni kilele cha maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa wa vita vya majimaji nchini Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu.
Maadhimisho ya vita vya Majimaji yenye lengo la kuwakumbuka mashujaa zaidi ya 67 walionyongwa Februari 27 mwaka 1906 na kuzikwa katika kaburi moja wakiwa katika harakati za kuung’oa ukoloni wa Wajerumani yamafikia kilele leo mkoani Ruvuma.
Maadhimisho hayo yameandaliwa kitaifa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na mkoa wa Ruvuma yanafikia kilele leo katika makumbusho ya Vita vya Majimaji mjini Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu amesema wakazi wa mji wa Songea na viunga vyake pamoja na wananchi kutoka mikoa ya jirani wamejitokeza katika maadhimisho hayo.

Serikali ya Uganda yakusudia kuwanunulia wabunge wote toleo jipya la iPads kupunguza gharama za steshenari.

Chama cha Forum for Democratic Change (FDC) kimepokea na kukubali mpango wa serikali ya Uganda wa kununua toleo jipya kabisa la iPads kwa ajili ya wabunge, lakini kimesema wabunge hao wakopeshwe na sio wapewe bure.
Msemaji wa Chama hicho Wafula Oguttu ambae pia ni mbunge, amesema pendekezo la kununua iPads halikataliwi lakini hakuna sababu ya kuwapa bure na badala yake wapewe kwa mkopo.
Serikali ya Uganda imepanga kununua iPads za kisasa na kuwapatia wabunge kwa lengo la kupunguza gharama ya steshenari.
Uamuzi huo ulichukuliwa hivi karibuni na Kamati ya Bunge na unasubiri utekelezaji kwa Kamati ya Mikataba.
 

Benedict XVI to hold final papal audience in Vatican.

Crowds have begun gathering in St Peter’s Square in the Vatican for the Pope’s final general audience before his resignation on Thursday.
Papal audiences are normally held inside a Vatican hall in the winter.
But such is the level of interest that the event is being held outdoors and 50,000 tickets have been requested.
 As many as 200,000 people may attend.
After Benedict XVI steps down on Thursday, he will become known as “pope emeritus”.
There has been no papal resignation since Pope Gregory XII abdicated in 1415.
The surprise announcement of Benedict’s abdication has required the rules of electing a successor to be changed to allow the next pope to be chosen before Holy Week, which leads up to Easter.
On Wednesday, the Pope, 85, will be making one of his last public appearances – using his trademark white “popemobile” to greet pilgrims in St Peter’s Square.
 

Waziri Mkuu afanya mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kutoka Sweden.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akifurahia jambo wakati wa mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh (kushoto) na Mkaguzi  Mkuu  wa hesabu za Serikali wa Sweden  Jan Lindahr Hjelmaker. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Tuesday, February 26, 2013

CRDB yawa benki pekee Tanzania kupata cheti cha Superbrands kwa miaka miwili mfululizo.


Mkurugenzi kutoka taasisi ya Superbrand, Jawad Jaffer akitoa maelezo kwa wageni waalikwa juu ya kitabu cha orodha ya kampuni zilizotunukiwa hadhi ya Superbrand.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB-Uendeshaji na huduma kwa wateja Saugata Bandyopadhyay(kulia) akipokea cheti cha Superbrand kutoka kwa mkurugenzi wa Superbrands ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer.
Baadhi ya wageni walio hudhuria tafrija hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB-Uendeshaji na huduma kwa wateja Saugata Bandyopadhyay wakati wa tafrija ya kupokea cheti cha Superbrand
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza na waandishi wahabari juu ya sababu zilizoipaisha Benki ya CRDB hadi kutunikiwa cheti cha Superbrand kwa mara ya tatu mfululizo pia mikakati ya benki hiyo katika kuboresha huduma zake ili kuendeleza rekodi yake ya kupata cheti hicho kila mwaka.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE YA NCHI WA OMAN AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi Bin Abdullah,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe wake leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,ukiongozwa na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi Bin Abdullah,(wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe wake leo,kwa ajili ya Mazungumzo na Rais. Picha na Ramadhan Othman,IKulu.

Kocha wa Azam afungiwa na kupigwa faini kwa kuchojoa bukta.


Kocha Mkuu wa Azam, Stewart John Hall (pichani) amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushusha bukta yake na kumlalamikia mwamuzi msaidizi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Kagera Sugar iliyochezwa Januari 26 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
 Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana mwishoni mwa wiki kupitia ripoti za michuano ya VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 inayoendelea hivi sasa na kufanya uamuzi mbalimbali.
Naye Kocha Msaidizi wa timu ya Mgambo Shooting, Denis Mwingira ametozwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Oktoba mwaka jana katika Uwanja wa Manungu.
Ally Jangalu ambaye ni Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro naye ameangukiwa na rungu la Kamati ya Ligi kwa kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga uamuzi wa refa kwa sauti ya juu. Alitenda kosa hilo kwenye mechi kati yao na Kagera Sugar iliyochezwa Novemba 10 mwaka jana Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Matukio ya aina hiyo kwa kocha Jangalu yamekuwa ya kujirudiarudia ambapo Oktoba 13 mwaka jana katika mechi dhidi ya Azam iliyochezwa mjini Morogoro aliondolewa na mwamuzi kwenye benchi kwa kuchochea wachezaji wa timu yake wacheze rafu.
Naye Kocha wa timu ya Moro United inayoshiriki FDL, Yusuf Macho amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumtolea lugha chafu refa baada ya mechi dhidi ya Transit Camp iliyofanyika Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.
Pia Kocha wa Burkina Faso, Hasheem Mkingie amepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kutoa lugha chafu katika mechi ya FDL dhidi ya Mkamba Rangers.
Kiongozi wa Majimaji, Joseph Nswila ambaye aliingia uwanjani baada ya mechi dhidi ya Mlale JKT kumalizika na kuvamia waamuzi amefungiwa miezi sita.
Vilevile timu ya Azam imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi kati yao na JKT Oljoro iliyochezwa Novemba 7 mwaka jana katika Uwanja wao wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Pia Coastal Union imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Simba iliyochezwa Oktoba mwaka jana Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Nayo klabu ya African Lyon imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa timu yake kugoma kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mechi dhidi ya Coastal Union iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Oktoba 24 mwaka jana.
Timu ya Burkina Faso ya Morogoro imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na kuonesha vitendo vya ushirikina kabla ya mechi yao dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Oktoba 24 mwaka jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Faini ya ushirikina ya sh. 200,000 pia imepigwa timu ya Pamba baada ya kuonesha vitendo hivyo kwenye mechi yao dhidi ya Mwadui iliyochezwa Novemba 4 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Nayo Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 baada ya washabiki wake kumtolea lugha chafu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA), Hamis Semka na kumrushia chupa za maji mwamuzi wa mezani katika mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa mjini Morogoro.
Polisi Dodoma imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kuvamia uwanjani na kutaka kuwapiga waamuzi katika mechi yao dhidi ya JKT Kanembwa na kusababisha mipira miwili ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kupotea.
Pia klabu kadhaa zimeandikiwa barua za onyo kwa timu zao kuchelewa kufika uwanjani au kutofika kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (Pre-match meeting). Klabu hizo ni Coastal Union, JKT Ruvu, Toto Africans, Simba, Green Warriors, Majimaji, Mkamba Rangers, Polisi Dodoma, JKT Kanembwa, Moro United.
Mchezaji Stanley Nkomola wa JKT Ruvu baada ya mechi dhidi ya Coastal Union alikwenda jukwaani na kuanza kupigana na washabiki. Pia kipa wa timu ya Transit Camp, Baltazar Makene baada ya mechi dhidi ya Tessema aliruka uzio na kwenda kupigana na washabiki.
Kwa vile masuala ya wachezaji hao ni ya kinidhamu yamepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...