Monday, February 25, 2013
Pinda akutana na Balozi wa Canada.
Rais Kikwete aondoka Addis Ababa kuelekea Uganda kuhudhuria mazishi ya Baba yake Rais Museveni.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na maafisa mbalimbali wa ubalozi wa
Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole
jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria
hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na
Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete,
kabla ya kurejea Dar es salaam jana, alikwenda Uganda kuhudhuria
mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta,
aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake Rwakitura.
Balozi
wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati)
na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete
wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo jana jioni ya Februari 24,
2013.(PICHA NA IKULU).
By Freddy Maro, Rwakitura, Western Uganda
Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete jana ameungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika
kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais Yoweri Museveni
wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.
Rais
Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa
Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa
Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Akitoa
salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa
Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na
kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na
kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea
marehemu.
Rais
Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo
alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuithamini elimu ambapo
aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali
kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee
wengi wenye umri wake(97).
Rais
Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao
ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa
kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe
akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana
na changamoto nyingi katika maisha yao.
Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda.
Rais
Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha
waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo.
Juliet Naivasha ajishindia Tsh 5,000,000 Kupitia DStv Rewards.
Mshindi
wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha, akifurahia zawadi yake ya
kitita cha Tshs Milioni 5 kama inavyoonekana katika mfano wa hundi
aliyoishikilia.
Kwa wiki ya pili mfululizo, wateja wa DStv wanaolipia akaunti zao kila mwezi kabla hazijakatwa na hivyo kuingia katika droo maalumu inayochezeshwa kila wiki na kutoa nafasi kwa wateja kujishindia mamilioni ya fedha imeendelea tena kwa kumpata mshindi wake wa pili.
Kupitia kampeni hiyo ambayo imepewa jina la DStv Rewards, Juliet Naivasha, mfanyakazi wa National Bank Of Commerce (NBC), amekuwa mshindi wa pili na kujishindia kitita cha Tshs 5,000,000 (Milioni 5).
Mshindi
wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha ( wa pili kutoka kushoto),
akiwa na wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania (Ronald Shelukindo na
Furaha Samalu) pamoja na Mama yake mzazi, Hilder Lawrence Nyambo
(anayemfuatia katika picha) pamoja na mdogo wake Lisa (kulia)
DStv Rewards
ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania
kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka
kwao.
Akiongelea
DStv Rewards, Meneja Masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Furaha
Samalu, amesema DStv Rewards ipo wazi kwa kila mteja na hivyo
amewashauri waendeleee tu kulipia akaunti zao kabla hazijakatwa ili
wapate nafasi ya kuibuka washindi.
Wakati huo huo: Mteja wa DStv, Bwana John Komakoma,ameibuka mshindi katika droo nyingine ambayo imepewa jina la Spot The Rewards Box
ambapo pindi mteja akiwa anatizama televisheni na kufanikiwa kuona
kibox fulani chenye nembo ya DStv, anatakiwa kutuma SMS yenye majina
yake yote mawili na namba yake ya simu kwenda katika namba +27 711 745
622 ndani ya dakika tano tangu alipokiona “kibox”.
Kwa ushindi huo Bwana John Komakoma
ameshinda Subscription ya mwaka mzima (miezi 12) ya DStv.Kwa maana
hiyo, Bw.John ataendelea kufaidi DStv bila malipo yoyote kwa kipindi cha
mwaka mzima!
Mshindi
wa droo ya Spot The Rewards Box, Bw. John Komakoma (katikati)
akipongwezwa na Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Baraka
R.Shelukindo huku Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu
akishuhudia. Bw. John Komakoma amesema yeye ni shabiki wa Liverpool wa
kutupwa!
Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia DStv inawapongeza washindi wote.
Sunday, February 24, 2013
ADEN RAGE MWENYEKITI WA SIMBA KESHO KUACHAIA NGAZI?
Mwenyekiti wa Simba ismail Aden Rage |
Taarifa hizo zimedokeza kuwa, Rage atatangaza msimamo huo wa kuachia ngazi Msimbazi kesho atakapokutana na waandishi wa habari.
MICHARAZO imekuwa ikimsaka Rage mwenyewe kusikia kauli yake, lakini simu yake imekuwa haipatikani, hivyo juhudi zinaendelea ili kuthibitisha taarifa hizo na tutawajuvya mara tukibahatika kumpata.
MUIGIZAJI STEVE NYERERE ATUPWA LUPANGO
Eneo la
tukio la ajali hiyo.
Mashuhuda
wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.
Kushoto ni
gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari
lililohusika na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.
Huu ndiyo
waya wa umeme uliosababisha ajali hiyo.
Askari wa
usalama barabarani, akipima ajali hiyo.
Askari
akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka
kituoni Mabatini.
Gari la
Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari jingine.
Gari
husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.
Baadhi ya
warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa
washiriki wa Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio.
**********
Movie
mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive Nyerere, iliyokuwa
ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali
na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi hii.
Msanii huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo
cha Mabatini, wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki
katika Movie hoyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.
Wasanii hao pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao
iliyokuwa maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na
kufanyia mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.
Ajali hiyo ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya
washiriki wa movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo
kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo
ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa
aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.
Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo
kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni.
Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi
umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa
waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na
moto, ili kuepusha madhara zaidi.
Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa
usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva
wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo
yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.
Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote
wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo,
aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Stive alishindwa kuvumilia na
kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi
katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka
naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini.
credits:
Sufiani Mafoto
WAANDISHI WA HABARI WANUSURIKA KUTEKWA WAKITOKA KUHOJI MASWALA YA GESI MTWARA
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, walioshiriki
Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mjini Mtwara,
wakilindwa na Askari wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU),
eneo la Chuo cha VETA, mjini Lindi jana asubuhi walipopelekwa na mabasi
madogo maarufu kwa jina 'Coaster' kutoka Mtwara Mjini, walikokimbia
vitisho vya baadhi ya wakazi wa mji huo, waliopanga kuwavamia wakiwa
kwenye mabasi makubwa mawili yaliyopangwa kuwasafirisha kwenda Dar es
Salaam jana, wakiwahisi kuwa wanahabari hao walikuwepo mkoani humo
kupeleleza suala la Gesi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Na Richard Mwaikenda, Mtwara
WAANDISHI wa Habari 150 kutoka vyombo mbalimbali wamenusurika kuvamiwa na wananchi wakiwahisi kwamba walikwenda mjini Mtwara kupepepeleza suala la Gesi.
Wanahabari hao waliokuwepo Mtwara katika Kongamano la siku mbili la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lilibidi wabadili muda wa kuondoka jana badala ya saa mbili asubuhi waliondoka alfajiri saa 11.
Uamuzi huo ulitolewa baada ya kuwepo fununu kwamba wananchi hao walipanga kuwavamia na kuwadhuru waandishi wa habari wakiwa kwenye mabasi mawili ya Kampuni ya amanju yaliyotakiwa kuondoka Mtwara saa mbili asubuhi kwenda nao Dar es Salaam.
Fununu hizo ziliwapata wanahabari wakiwa kwenye hafla ya chakula cha usiku waliyoandaliwa na NHIF, kwenye Hoteli ya Makonde Beach juzi usiku, ambapo hata Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alihudhuria, lakini hakufika mwisho baada ya kusikia taarifa hizo.
WAANDISHI wa Habari 150 kutoka vyombo mbalimbali wamenusurika kuvamiwa na wananchi wakiwahisi kwamba walikwenda mjini Mtwara kupepepeleza suala la Gesi.
Wanahabari hao waliokuwepo Mtwara katika Kongamano la siku mbili la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), lilibidi wabadili muda wa kuondoka jana badala ya saa mbili asubuhi waliondoka alfajiri saa 11.
Uamuzi huo ulitolewa baada ya kuwepo fununu kwamba wananchi hao walipanga kuwavamia na kuwadhuru waandishi wa habari wakiwa kwenye mabasi mawili ya Kampuni ya amanju yaliyotakiwa kuondoka Mtwara saa mbili asubuhi kwenda nao Dar es Salaam.
Fununu hizo ziliwapata wanahabari wakiwa kwenye hafla ya chakula cha usiku waliyoandaliwa na NHIF, kwenye Hoteli ya Makonde Beach juzi usiku, ambapo hata Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alihudhuria, lakini hakufika mwisho baada ya kusikia taarifa hizo.
Hongera rais Kagame : Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mke wake Bi Jeannette Kagame wakishirikiana na wananchi wa Kanyinya wilaya ya Nyarugenge kuchimba mitaro ya maji jana( Feb 23,2013).
MDEE AONGELEA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Mheshimiwa
Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali
Mbunge wa
Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za
binafsi maarufu kama “Academia” inachangia matokeo mabovu ya kidato cha
nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la
chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati
akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano. “Kwa Mtazamo wangu
mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma,
kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu
hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo
unakuwa haupo”
SIMBA YAPIGWA KIMOJA NA MTIBWA SUGAR
Timu
ya Simba ya Dar es Salaam, leo imekubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya
Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliochezwa leo
jioni katika Uwanja wa Taifa.
Bao
la Mtibwa Sugar, limefungwa na Mshambuliaji Salvatory Mtebo, katika
dakika ya 19, baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Namba
moja wa timu hiyo, Juma Kaseja.
Bao
hilo limedumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, jambo ambalo limezu
mtafaruku mkubwa baina na Mashabiki, Wanachama wa timu ya Simba,
walikuwa wakishinikiza kutaka kuonana na viongozi wao ili kuzungumza
falagha kuwashinikiza kuitisha mkutano mkuu wa dharula.
Aidha
mashabiki hao na wanachama wa Simba, waligoma kuondoka uwanjani hapo
hadi walipotawanywa na gari la Polisi lililoanza kutishishia kurusha
maji ya kuwasha, huku vingozi wa timu hiyo na wachezaji wakiwa
wamefungiwa ndani hadi kundi la watu hao lilipotawanyika uwanjani hapo.
Hata
hivyo katika mchezo huo Beki wa Simba, Juma Nyoso, alipewa kadi
nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vicent Barnabas, katika kipindi cha
pili.
Beki wa Simba, ambaye leo amechezeshwa
kama kiungo wa chini, Shaban Kapombe, akimchezea vibaya Rashid Gumbo.
Beki wa Simba Keita, akimdhibiti
mchezaji wa Mtibwa.
Mshambuliaji wa Mtibwa, akiwasakata
mabeki wa Simba.
credits: Sufiani Mafoto
Rais Kikwete ashiriki Utiaji Saini Mpango Wa Umoja Wa Mataifa Wa Amani, Usalama na Ushirikiano Katika DRC.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka
saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu
iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa,
Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Mhe. Ban Ki-moon akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani,
Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa
hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini
Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa
Mataifa Dkt. Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma akisaini Mpango wa Umoja
wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao
makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24,
2013.
Rais Joseph Kabila wa DRC na Rais
Paul Kagame wa Rwanda wakibadilishana mawazo kwa furaha huku Rais wa
Jamhuri ya Kongo (Brazaville) Mhe Denis Sassou Nguesso akiwa kati yao
baada ya wote kweka saini katika Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani,
Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa
hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini
Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim na wajumbe
wengine wa ujumbe wa Tanzania wakati wa uwekaji akiweka saini Mpango wa
Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao
makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4,
2013.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe
Ban Ki-moon katika picha ya pamoja na viongozi wa nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu baada ya uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa
wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa
Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akipongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon kwa kuwa
mmoja wa viongozi wa bara la Afrika walio mstari wa mbele kusimamia
amani baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani,
Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa
hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini
Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akipongezana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam
Desalegn baada uwekaji akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa
Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika
mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 4, 2013. Katikati ni
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dkt Nkosazana Clarice
Dlamini-Zuma.(PICHA NA IKULU).
Naibu Waziri wa Fedha akagua Vitega uchumi vya PSPF Jijini Dar.
SIKU
MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za
makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe
Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba
hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama
wake.
Mbene
pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35
linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam. Pichani ni
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia mchoro wa Jengo
la Kitega Uchumi cha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
ambalo linajengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam na litakuwa na
Ghorofa 35. Ndani ya jingo hilo la kutakuwa na Ofisi, maduka na nyumba
za kulala.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF),
Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo
Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa
na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.
Meneja Mradi wa Ujenzi
wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa maelezo
kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika
ujenzi huo.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani
katika moja ya vyumba katika nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF
Tower ambalo ujenzi wake bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika
zitauzwa kwa watumishi wa Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu
wakiongozana kuteremka ngazi zilizopo katika moja ya nyumba (apartment)
zilizopo katika jingo hilo la PSPF Tower ambalo linaendelea kujengwa.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akitembezwa ndani ya jengo hilo
na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF), Bwana Adam Mayingu.
Watumishi wa PSPF wakizungumza jambo ndani ya Jengo
hilo.
Awali Naibu Waziri wa
Fedha, Janet Zebedayo Mbene alipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi
wa nyumba 491 za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
zinazojengwa Buyuni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na ambazo
zimekamilika ujenzi wake na kuanza kuuzwa kwa Wanachama wa mfukjo huo.
Pichani mbele kutoka kushoto ni Gabriel Silayo, Mkurugenzi wa Uwekezaji
wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Naibu Waziri wa
Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba
wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.
Nyumba hizo
zikiwa zimekamilika ujenzi wake na kusubiri wateja tu.
Naibu Waziri wa Fedha,
Janet Mbene akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba
akimtembeza ndani ya moja ya nyumba hizo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri
wa Fedha, Janet Mbene nje ya moja ya nyumba ambazo zimejengwa na PSPF,
kwaajili ya kuwauzia wanachama wake kwa gharama nafuu.
Subscribe to:
Posts (Atom)