Mke wa rais Robert Mugabe, Grace Mugabe ameonya kwamba kuna uwezekano wa kufanyika kwa mapinduzi huku kukiwa kuna wasiwasi mkubwa nchini humo kuhusu harakati za kumrithi rais Mugabe.
Anasema kuwa washirika wa makamu wa rais Emmerson Mnangangwa wanatishia maisha ya wale ambao hawamuungi mkono kumrithi rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93.
Bi Mugabe yeye binafsi na bwana Mnangagwa wako kifua mbele na uadui wao umekigawanya chama tawala cha Zanu PF .
Mgogoro huo unajiri baada ya bwana Mgangagwa kudai kwamba aliwekewa sumu katika chakula chake mwezi Agosti.
Wafuasi wake wamesema kuwa wapinzani wake ndani ya Zanu PF ndio wakulaumiwa, ijapokuwa bwana Mnangagwa amejitenga na madai kama hayo.
Alikiambia chombo cha habari cha taifa hilo anasalia kuwa mtiifu kwa rais Mugabe.
Bi Grace Mugabe aliyekasirika alimshutumu bwana Mnangagwa katika hafla moja mjini Harare.
''Tunatishiwa usiku na mchana kwamba iwapo mtu fulani hatokuwa rais , tutauawa'', alisema.