Wapatanishi
wanaojaribu kutatua mzozo wa kisiasa huko Jamhuri ya Kidemocrasi ya
Congo wamesema serikali ya nchi hiyo na vilevile washirika kutoka
makundi ya upinzani sasa wameafikia mwafaka.
Maaskofu kutoka
kanisa katoliki waliokuwa wakiendesha kikao hicho cha majadiliano
wanasema makubaliano ni kwamba rais Joseph Kabila anaweza kusalia
madarakani kwa mda wa mwaka mmoja, lakini ni sharti uchaguzi ufanyike
ndani ya kipindi cha miezi 12.
Sharti jingeni ni kuwa rais Kabila asiwanie tena kiti cha urais katika uchaguzi huo.
Mwafaka huo unatarajiwa kutiwa saini hii leo.
Mda
wa utawala wa rais Kabila umemalizika mwezi huu lakini kutong'atuka
kwake kumesababisha maandamano yaliyokumbwa na ghasia ambapo watu zaidi
ya 40 wamefariki.