Tuesday, December 29, 2015

ARSENAL YAPAA KILELENI


Wachezaji wa timu ya Arsenal

Washika bunduki wa London, Arsenal wamekaa kileleni mwa ligi ya England kwa pointi 39 baada ya kuichapa Bournemouth kwa mabao 2-0.

Arsenal walipata mabao yao kupita kwa beki Gabriel Paulista aliyefunga bao la kwanza Dakika ya 27 ya mchezo kisha kiungo wa Kijeruman Mesut Ozil, akahitimisha kazi kwa bao la pili alilolifunga katika dakika ya 63.

Nao Mashetani Wekundu wa Man United wakaenda sare ya 0-0 na mabingwa watetezi Chelsea, Everton wakicheza katika dimba lao la Goodson Park wakalala kwa kipigo cha mabao 4-3 dhidi ya Stoke city.

Matokeo mengine ni: Crystal Palace 0 – 0 Swansea Norwich 2 – 0 Aston Villa Watford 1 – 2 Tottenham West Brom 1 – 0 Newcastle West Ham 2 – 1 Southampton

Monday, December 28, 2015

MLINZI WA OSAMA BIN LADEN AFARIKI DUNIA


Al Bahri


Taarifa kutoka Yemen zinasema aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Vyanzo vya habari vya kitabibu vimesema kwamba Nasser al Bahri ambaye pia alikuwa akijulikana kama Abu Jandal alifariki siku ya Jumamosi, katika Hospitali iliyoko kwenye mji wa Mukalla kusini mwa Yemen.

Alirudi nchini humo mwishoni mwa mwaka 2008, baada ya kuachiliwa kutoka katika kizuizi alichowekewa na Marekani huko Guantanamo.

Al Bahri alijulikana kuhusika na mashambulizi yaliyofanywa na mtandao wa kigaidi katika miaka ya 90, katika nchi za Afghanistan, Somalia na Bosnia.

Thursday, December 17, 2015

MAGUFULI "ELIMU BURE ITAPATIKANA"

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kwamba elimu ya bure itapatikana kama alivyoahidi.

Akijibu swali la fedha zitapatikana wapi za kutimiza ahadi yake ya elimu ya bure, Magufuli amesema, mwezi huu wa Desemba pekee, Tanzania inatarajiwa kukusanya kiasi cha dola bilioni 1, ambazo hazijawahi kukusanywa.

Amesema kuanzia mwezi huu fedha za kusomesha wanafunzi bure zitaanza kutengwa kuanzia mwezi huu. Kwa mujibu wa Dkt Magufuli, Serikali imefikia uamuzi wa kutenga dola milioni 65.5, ambazo zitapelekwa moja kwa moja katika shule zenye uhitaji na kwamba fedha zitakapotumwa, nakala ya barua itapelekwa kwa mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi wake.

Rais Magufuli ameonya yeyote atakayetumia fedha hizo vinginevyo kwamba atachukuliwa hatua kali. Amesema fedha hizo zitasaidia katika ununuzi wa vitu kama vile chaki, maandalizi ya mitihani na vitu vingine vya muhimu shuleni.

Thursday, December 10, 2015

MH. MAGUFULI ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

BARAZA LA MAWAZIRI

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri - George Simbachawene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...