Kumetokea shambulizi la bomu mbele ya soko lenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja na kuwauwa zaidi ya watu 21.
Taswira ya majonzi na kilio ilitanda katika mji
wa Abuja, mamia ya watu waliokuwa wakinunua bidhaa katika soko hilo
wakijikuta wakivuja damu kutokana na majeraha ya mlipuko huo na wengine
kuishia mauti.
Bomu hilo lililipuka mbele ya kituo kikubwa cha biashara, kinachotembelewa na watu wengi.
Walioshuhudia walisema sehemu za miili ya wanadamu zilitapakaa kila mahali sakafuni.
Magari yalichomeka kabisa na vioo katika
madirisha ya nyumba zilizokuwa karibu kuvunjika vyote. Watu waliokuwa na
hofu walielekea kwenye mahospitali yaliyo karibu ambapo walishuhudia
magari ya wagonjwa yakisongamana kila mahali yakiwaleta wagonjwa na
miili ya waliokufa.
John Tobi Wojioa aliwasili mahali hapo muda mfupi baadaye akimtafuta jamaa wake. Alitaja alichoona kama mafuriko ya damu:
"Kulikuwepo magari ya wagonjwa wa shirika la
FRCS (federal Road Safery Corps) na ya mashirika mengine yaliyokuwa
yakiingia na kuondoka yakibeba miili ya waathirika. Kwenye barabara
alama za damu za nyayo za wanadamu zilionekana kila mahali," alisema
Bwana Wojioa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Bahati kwa Bwana Wojioa ni kuwa jamaa wake baadaye alipatikana akiwa hai huku akiendelea kutulia kutokana na mlipuko huo.
Hii ni mara ya tatu kwa mji mkuu kulengwa na
milipuko tangu Aprili. Kundi la Waismalu waenye itikadi kali la Boko
Haramu lilidai kuhusika katika milipuko mbili ya awali ambako zaidi ya
watu 90 walifariki.
Milipuko hiyo ilitokea kando mwa jiji lakini huu
wa sasa umetokea katikati mwa jiji katika Wilaya ya Wuse 2 na hofu yake
itatanda katika mji wote.
Kwa mara nyingine tena Boko Haram watashukiwa
kuhusika katika mlipuko huu. Kundi hilo limelipua miji kadhaa nchini
Nigeria huku likiendesha kampeni yake ya kuwashambulia raia katika
maeneo ya mashambani hasa Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo.
Mnamo Jumanne watu waliokuwa wakitoroka vijiji
katika jimbo la Borno walisema kuwa makumi ya wanawake na watoto
walikuwa wametekwa nyara.
Lakini Serikali kwa upande wake ikasema kuwa hakuna ushahidi kuwa utekaji nyara ulitendeka.
Serikali ilisema vivyo hivyo wakati zaidi ya wasichana wanafunzi zaidi ya 200 walitekwa nyara na Boko Haram mnamo Aprili.
Wachunguzi wengi wanasema kuwa kwa kukanusha
kuwa kuna utovu wa usalama nchini Nigeria, Serikali imechanganyikiwa kwa
sababu milipuko ya mabomu ya mara kwa mara ni ushahidi tosha kuwa
ukosefu wa usalama ndio ukweli wa mambo nchini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment